Imaam al-Albaaniy Kuhusu Maadhimisho Ya Maulidi

Imaam al-Albaaniy: Maulidi yanayofanywa Iraaq, Oman au Syria, kwa hakika ni katika mambo yaliyozuliwa. Kule kutenga siku maalum, na kuiita “Sherehe ya Maulidi ya Mtume”, hili bila ya shaka ni katika mambo yaliyozuliwa. Isitoshe, kuna mukhaalafah mwingi katika yanayofanywa katika sherehe hii. Kwa mfano kunatokea mukhaalafah wa Kishari´ah mwingine, mukhaalafah unazidi. Ama kwa mfano kunafanywa mihadhara, katika mihadhara hii wakakumbushana kitu katika Siyrah na Sunnah ya Mtume, hili bila ya shaka ingekuwa ni kheri kubwa kuliko kutenga siku ya Maulidi [kuzaliwa kwake]. Lakini pamoja na hivyo, haijuzu kutenga mwezi maalum au siku maalum kusherehekea Maulidi hata kama itakuwa sherehe hii haina ndani yake mukhaalafah unaokwenda kinyume na Shari´ah. Muulizaji: Katika sherehe hii huletwa vyakula Shaykh. Imaam al-Albaaniy: Kila kinachofanywa katika mwezi huu, ni katika mambo yaliyozuliwa.

Imaam al-Albaaniy:
Maulidi yanayofanywa Iraaq, Oman au Syria, kwa hakika ni katika mambo yaliyozuliwa. Kule kutenga siku maalum, na kuiita “Sherehe ya Maulidi ya Mtume”, hili bila ya shaka ni katika mambo yaliyozuliwa.

Isitoshe, kuna mukhaalafah mwingi katika yanayofanywa katika sherehe hii. Kwa mfano kunatokea mukhaalafah wa Kishari´ah mwingine, mukhaalafah unazidi. Ama kwa mfano kunafanywa mihadhara, katika mihadhara hii wakakumbushana kitu katika Siyrah na Sunnah ya Mtume, hili bila ya shaka ingekuwa ni kheri kubwa kuliko kutenga siku ya Maulidi [kuzaliwa kwake]. Lakini pamoja na hivyo, haijuzu kutenga mwezi maalum au siku maalum kusherehekea Maulidi hata kama itakuwa sherehe hii haina ndani yake mukhaalafah unaokwenda kinyume na Shari´ah.

Muulizaji:
Katika sherehe hii huletwa vyakula Shaykh.

Imaam al-Albaaniy:
Kila kinachofanywa katika mwezi huu, ni katika mambo yaliyozuliwa.