Imaam al-Albaaniy Kuhusu Ibaadhiyyah

Tutawabainishia kama wako katika uongofu au wako katika upotevu mkubwa. Bila ya shaka Ibaadhiyyah na kila ambaye anakubaliana na rai yao na ´Aqiydah yao ya kuwa Maneno ya Allaah (´Azza wa Jalla) yameumbwa - nayo ni hii Qur-aan Tukufu - na pia anayepinga waumini kumuona Mola wa walimwengu siku ambayo haitofaa mali wala watoto ila yule aliekuja kwa Allaah kwa moyo msafi. Bila shaka watu hawa wanaopinga kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah ya kihakika na hayakuumbwa. Kupinga huku kuna upotevu - yaani wa wazi kabisa. Ama kusema kuwa upotevu huu ni ukafiri na kuritadi kutoka katika Dini au hapana, tunasema, atakayebainikiwa na hoja (dalili) kisha akapinga, basi huyu ni kafiri karitadi katika Dini ya Kiislamu. Lakini mwenye kupinga hilo (kwa ujinga), atakuwa katika upotevu. Sisi sio muhimu kwetu kusema fulani katika watu au kundi fulani katika watu ni makafiri. Yatosha kusema kuwa ni wapotevu. Kwa kuwa sisi makusudio yetu ni wao waongoke na wajue kuwa wako makosani na kwenye upotevu mpaka warudi katika usawa.

Tutawabainishia kama wako katika uongofu au wako katika upotevu mkubwa. Bila ya shaka Ibaadhiyyah na kila ambaye anakubaliana na rai yao na ´Aqiydah yao ya kuwa Maneno ya Allaah (´Azza wa Jalla) yameumbwa – nayo ni hii Qur-aan Tukufu – na pia anayepinga waumini kumuona Mola wa walimwengu siku ambayo haitofaa mali wala watoto ila yule aliekuja kwa Allaah kwa moyo msafi. Bila shaka watu hawa wanaopinga kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah ya kihakika na hayakuumbwa. Kupinga huku kuna upotevu – yaani wa wazi kabisa.

Ama kusema kuwa upotevu huu ni ukafiri na kuritadi kutoka katika Dini au hapana, tunasema, atakayebainikiwa na hoja (dalili) kisha akapinga, basi huyu ni kafiri karitadi katika Dini ya Kiislamu. Lakini mwenye kupinga hilo (kwa ujinga), atakuwa katika upotevu. Sisi sio muhimu kwetu kusema fulani katika watu au kundi fulani katika watu ni makafiri. Yatosha kusema kuwa ni wapotevu. Kwa kuwa sisi makusudio yetu ni wao waongoke na wajue kuwa wako makosani na kwenye upotevu mpaka warudi katika usawa.