Imaam Ahmad Kuhusu Hadd Duniani Ni Kafara

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: “Mwenye kukutana Naye (Allaah) na kishasimamishiwa hadd (adhabu) ya dhambi hiyo duniani, basi ndio kafara yake kama zilivyokuja khabari juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba huduud ina kafara, lakini ijulikana kuwa hili lina vizuizi. Huduud ina kafara maadamu mtu hayajahalalisha kitendo cha haramu na akafa juu ya uhalalishaji huyo. Kwa mfano amekusudia kumuua muumini na akahalalisha kumuua na akafa juu ya ´Aqiydah hiyo mbovu. Amehalalisha jambo la haramu ambalo linajulikana fika katika Dini kuwa ni haramu – hata kama atasimamishiwa hadd ya kuuawa – hadd hii haimkafirii dhambi yake. Dhambi inayokafiriwa ni ya Muislamu ambaye ni mtenda dhambi ambaye amesimamishiwa hadd na yeye ni mwenye kukubali maasi yake, sio mwenye kuhalalisha yaliyoharamishwa na Allaah na sio mwenye kuharamisha Aliyohalalisha Allaah. Huduud ni kafara. Akiua mtu na akasimamishiwa hadd ya kuua na akawa ni mwenye kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy Chanzo: Usuul-us-Sunnah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1000&size=2h&ext=.rm

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mwenye kukutana Naye (Allaah) na kishasimamishiwa hadd (adhabu) ya dhambi hiyo duniani, basi ndio kafara yake kama zilivyokuja khabari juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba huduud ina kafara, lakini ijulikana kuwa hili lina vizuizi. Huduud ina kafara maadamu mtu hayajahalalisha kitendo cha haramu na akafa juu ya uhalalishaji huyo. Kwa mfano amekusudia kumuua muumini na akahalalisha kumuua na akafa juu ya ´Aqiydah hiyo mbovu. Amehalalisha jambo la haramu ambalo linajulikana fika katika Dini kuwa ni haramu – hata kama atasimamishiwa hadd ya kuuawa – hadd hii haimkafirii dhambi yake. Dhambi inayokafiriwa ni ya Muislamu ambaye ni mtenda dhambi ambaye amesimamishiwa hadd na yeye ni mwenye kukubali maasi yake, sio mwenye kuhalalisha yaliyoharamishwa na Allaah na sio mwenye kuharamisha Aliyohalalisha Allaah. Huduud ni kafara. Akiua mtu na akasimamishiwa hadd ya kuua na akawa ni mwenye kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy
Chanzo: Usuul-us-Sunnah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=1000&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 30th, March 2014