Imaam Abu Bakr Kuhusu Kuwatukana Ahl-ul-Hadiyth

Imaam Abu Bakr (Rahimahu Allaah) amesema: 39- Usiwe miongoni mwa watu wanaocheza na Dini yao kuwatukana Ahl-ul-Hadiyth na kuwaponda ---------------------- MAELEZO Kauli ya mwandishi “Usiwe miongoni mwa watu wanaocheza na Dini yao”, yaani usiichukulie (usiifanye) Dini pumbao na mchezo. Hichi ni kitendo cha wanafiki na mafusaki. Bali ni juu yako kushikamana na kuheshimu Dini na kuadhimisha maamrisho ya Dini na watu wake. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) kuhusu wanafiki na mafusaki: اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا “Wameifanya dini yao pumbao na mchezo, na yakawaghururi maisha ya dunia.” (al-A´araaf:51) Wanaingia katika hili Suufiyyah ambao wanafanya kucheza, dufu na nyimbo kuwa ni katika Dini. Wanaita kuwa ni Anashiyd, Maraathiy na Qaswiydah na wanaziimba huku wakijikurubisha kwa Allaah kwa hilo. Ni katika nyimbo na taarabu zilizoharamishwa. Ni katika upuuzi ulioharamishwa. Wanaingia vilevile katika hili, nao ni aula zaidi, wale ambao wamemili katika mambo ya shahawa na yale ambayo nafsi zao inatamani na wanazipa nafsi vile inavyopenda hata kama jambo hilo litakuwa linakwenda kinyume na Dini, huku ni kuichukua Dini pumbao na mchezo. Wanaingia katika hili mafusaki ambao hawajali mambo ya Dini na wanafuata yale ambayo nafsi zao inatamani na matakwa yao. Wanaingia katika hili pia wafanya ´ibaadah katika Suufiyyah ambao wameingiza katika ´ibaadah yale yasiyokuwemo, bali wameingiza ndani yake yanayokwenda kinyume nayo, katika kupiga ngoma na kucheza na Qaswiydah zilizopangwa, kama wafanyavyo manaswara kwa nyimbo zao. Haya yote ni katika kufanya Dini pumbao na mchezo. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 198-199

Imaam Abu Bakr (Rahimahu Allaah) amesema:

39- Usiwe miongoni mwa watu wanaocheza na Dini yao

kuwatukana Ahl-ul-Hadiyth na kuwaponda
———————-

MAELEZO

Kauli ya mwandishi “Usiwe miongoni mwa watu wanaocheza na Dini yao”, yaani usiichukulie (usiifanye) Dini pumbao na mchezo. Hichi ni kitendo cha wanafiki na mafusaki. Bali ni juu yako kushikamana na kuheshimu Dini na kuadhimisha maamrisho ya Dini na watu wake. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) kuhusu wanafiki na mafusaki:

اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا
“Wameifanya dini yao pumbao na mchezo, na yakawaghururi maisha ya dunia.” (al-A´araaf:51)

Wanaingia katika hili Suufiyyah ambao wanafanya kucheza, dufu na nyimbo kuwa ni katika Dini. Wanaita kuwa ni Anashiyd, Maraathiy na Qaswiydah na wanaziimba huku wakijikurubisha kwa Allaah kwa hilo. Ni katika nyimbo na taarabu zilizoharamishwa. Ni katika upuuzi ulioharamishwa.

Wanaingia vilevile katika hili, nao ni aula zaidi, wale ambao wamemili katika mambo ya shahawa na yale ambayo nafsi zao inatamani na wanazipa nafsi vile inavyopenda hata kama jambo hilo litakuwa linakwenda kinyume na Dini, huku ni kuichukua Dini pumbao na mchezo. Wanaingia katika hili mafusaki ambao hawajali mambo ya Dini na wanafuata yale ambayo nafsi zao inatamani na matakwa yao.

Wanaingia katika hili pia wafanya ´ibaadah katika Suufiyyah ambao wameingiza katika ´ibaadah yale yasiyokuwemo, bali wameingiza ndani yake yanayokwenda kinyume nayo, katika kupiga ngoma na kucheza na Qaswiydah zilizopangwa, kama wafanyavyo manaswara kwa nyimbo zao. Haya yote ni katika kufanya Dini pumbao na mchezo.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 198-199


  • Kitengo: Uncategorized , Da´wah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 1st, March 2014