Imaam Abu Bakr Kuhusu Kushuka Kwa Allaah (´Azza wa Jalla)

11- Sema “Anashuka Jabbaar katika kila usiku bila ya Kayf (namna gani) Mwenye Ukuu Mmoja Mhimidiwa” ----------------- MAELEZO “Sema”, yaani sema ewe Sunniy – ambaye ameshikama na Kitabu na Sunnah – sema na wala usisite “Anateremka Jabbaar”, Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anashuka katika mbingu ya dunia. “Katika kila usiku”, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema hivyo na yeye ndiye mjuzi zaidi kumjua Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) na yanayolingana na Yeye. Kwa hivyo sema aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mthibitishie kushuka Allaah (´Azza wa Jalla). Kushuka ni katika Sifa za Matendo ambayo Anaifanya Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa Matakwa Yake na Kupenda Kwake pale Anapotaka. Kushuka huku kumepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wamelipokea kundi kutoka kwa Maswahabah na linapatikana katika vitabu Swahiyh. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu akisherehesha Hadiyth ya kuhusu kushuka na kimechapishwa kipekee na pamoja na Majmuu´. Kwa anuani “Sharh Hadiyth-un-Nuzuul”. Ni wajibu kumthibitishia Allaah ushukaji kama alivyomthibitishia hilo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba ni katika kila siku pale ambapo kunabaki theluthi ya mwisho ya usiku. Hili linawaraddi Mu´attwilah. Kwa kuwa limepokelewa kwa mapokezi mengi. Pengine wangelileta kisingizio ya kusema kuwa hii ni Hadiyth Ahaad na haifidishi yakini. Lakini kwa hapa hawana njia kwa kuwa ni kitu kimepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo kushuka huku ni kama Sifa Zake zingine zote, sio kama kushuka kwa viumbe Vyake, bali huku ni kushuka kwa Jabbaar (Jalla wa ´Alaa) ambako kunalingana na Utukufu na Ukubwa Wake. Hatujui namna yake, bali sisi tunathibitisha hilo kama lilivyokuja hali ya kuwa ni wenye kuliamini na hatulitilii taawili, hatulikanushi na wala hatulifananishi na kushuka kwa viumbe. Ni kushuka ambako kunalingana na Utukufu na Ukubwa wa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 97-98

11- Sema “Anashuka Jabbaar katika kila usiku

bila ya Kayf (namna gani) Mwenye Ukuu Mmoja Mhimidiwa”
—————–

MAELEZO

“Sema”, yaani sema ewe Sunniy – ambaye ameshikama na Kitabu na Sunnah – sema na wala usisite “Anateremka Jabbaar”, Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anashuka katika mbingu ya dunia.

“Katika kila usiku”, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema hivyo na yeye ndiye mjuzi zaidi kumjua Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) na yanayolingana na Yeye. Kwa hivyo sema aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mthibitishie kushuka Allaah (´Azza wa Jalla). Kushuka ni katika Sifa za Matendo ambayo Anaifanya Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa Matakwa Yake na Kupenda Kwake pale Anapotaka. Kushuka huku kumepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wamelipokea kundi kutoka kwa Maswahabah na linapatikana katika vitabu Swahiyh. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu akisherehesha Hadiyth ya kuhusu kushuka na kimechapishwa kipekee na pamoja na Majmuu´. Kwa anuani “Sharh Hadiyth-un-Nuzuul”.

Ni wajibu kumthibitishia Allaah ushukaji kama alivyomthibitishia hilo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba ni katika kila siku pale ambapo kunabaki theluthi ya mwisho ya usiku. Hili linawaraddi Mu´attwilah. Kwa kuwa limepokelewa kwa mapokezi mengi. Pengine wangelileta kisingizio ya kusema kuwa hii ni Hadiyth Ahaad na haifidishi yakini. Lakini kwa hapa hawana njia kwa kuwa ni kitu kimepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo kushuka huku ni kama Sifa Zake zingine zote, sio kama kushuka kwa viumbe Vyake, bali huku ni kushuka kwa Jabbaar (Jalla wa ´Alaa) ambako kunalingana na Utukufu na Ukubwa Wake. Hatujui namna yake, bali sisi tunathibitisha hilo kama lilivyokuja hali ya kuwa ni wenye kuliamini na hatulitilii taawili, hatulikanushi na wala hatulifananishi na kushuka kwa viumbe. Ni kushuka ambako kunalingana na Utukufu na Ukubwa wa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 97-98


  • Kitengo: Uncategorized , Kushuka (kuteremka) kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 16th, February 2014