Imaam Abu Bakr Kuhusu Kupinga Kwa Jahmiyyah Waja Kumuona Mola Wao

8- Hakika Jahmiyyah wanapinga hili, na kwetu sisi kwa tuliyoyasema ya kweli kuna Hadiyth zilizo wazi wazi 9- Amepokea Jariyr kutoka katika maneno ya Muhammad sema mfano wa yale waliyosema katika hilo utaokoka ------------------------- MAELEZO Hakika Jahmiyyah wanapinga kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jalla) Aakhirah. Hawana mapokezi juu ya hilo. Sisi katika kuthibitisha kuwa ataonekana (Aakhirah) tuna Hadiyth nyingi Mutawaatir, zilizopokelewa kwa mapokezi mengi kutoka katika mapokezi ya kundi la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amezikusanya katika kitabu chake “Haadiy al-Arwaah ilaa bilaadil-Afraah”. Ni kitabu kinachozungumzia Pepo, sifa zake na yaliyomo humo. Akataja kuhusu kuonekana kwa Allaah na Hadiyth ambazo zimepokelewa kwa mapokezi mengi kwa njia zake, isnadi zake na wapokezi wake. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 89

8- Hakika Jahmiyyah wanapinga hili, na kwetu sisi

kwa tuliyoyasema ya kweli kuna Hadiyth zilizo wazi wazi

9- Amepokea Jariyr kutoka katika maneno ya Muhammad

sema mfano wa yale waliyosema katika hilo utaokoka

————————-

MAELEZO

Hakika Jahmiyyah wanapinga kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jalla) Aakhirah. Hawana mapokezi juu ya hilo. Sisi katika kuthibitisha kuwa ataonekana (Aakhirah) tuna Hadiyth nyingi Mutawaatir, zilizopokelewa kwa mapokezi mengi kutoka katika mapokezi ya kundi la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amezikusanya katika kitabu chake “Haadiy al-Arwaah ilaa bilaadil-Afraah”. Ni kitabu kinachozungumzia Pepo, sifa zake na yaliyomo humo. Akataja kuhusu kuonekana kwa Allaah na Hadiyth ambazo zimepokelewa kwa mapokezi mengi kwa njia zake, isnadi zake na wapokezi wake.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 89


  • Kitengo: Uncategorized , Jahmiyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 15th, February 2014