Imaam Abu Bakr Kuhusu Kuonekana Kwa Allaah Aakhirah

6- Sema “Atajionyesha Allaah kwa viumbe wazi kabisa kama jinsi mwezi haufichikani basi na Mola Wako (ataonekana) wazi wazi.” ---------------------- MAELEZO Haya ni masuala ya kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Je, viumbe watamuona Allaah (´Azza wa Jalla) au hawatomuona? Jahmiyyah na Mu´tazilah wote wanapinga kuonekana kwa Allaah na wanasema kwamba Allaah Haonekani kwa kuwa kuonekana inakuwa kwa miili na Allaah sio mwili. Kwa hivyo hatoonekana. Wanapinga kuonekana kwa Allaah moja kwa moja, si duniani wala Aakhirah na tunamuomba Allaah afya. Kuko watu pia wanaosema kwamba Allaah Anaonekana duniani na Aakhirah. Hii ni kauli ya baadhi ya Suufiyyah. Kauli ya tatu – na ndio kauli ya haki – ni kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ataonekana Aakhirah. Watamuona watu wa Peponi kama jinsi Hadiyth kwa wingi zilivyothibiti juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama duniani hawezi kuonekana kwa kuwa watu hawana uwezo wa kumuona (Subhaanahu) duniani. Pindi Muusa (´alayhis-Swalaat was-Salaam) alipomuomba kumuona Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) duniani: قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ “Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Mola wako Alipojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika; na Muwsaa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Subhaanak! (Utakaso ni Wako!) Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini” (al-A´raaf:143) jibali liligeuka kuwa udongo kutokana na Ukubwa wa Allaah (´Azza wa Jalla). Vipi itakuwa kwa mwanaadamu kumuona Allaah? Hili ni kuhusu duniani. Ama Aakhirah Allaah Atawapa watu wa Peponi nguvu ambazo wataweza kwa nguvu hizo kumuona Mola wao (´Azza wa Jalla). Hii ni ikram kwao. Pale ambapo walimuamini duniani na wala hawajamuona, Allaah Akawapa ikram na Atajionyesha Peponi ili wapate ladha ya kumuona. Kama jinsi hilo lilivyotolewa dalili na Qur-aan na Sunnah al-Mutawaatir. Ama makafiri pale ambapo hawakumuamini duniani, Allaah Atajizuia wasimuone siku ya Qiyaamah. Anasema (Ta´ala): كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ “Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi (wasimuone) Mola wao.” (al-Mutwaffifiyn:15) Ikiwa makafiri wamewekewa kizuizi wasimuone Allaah, hapa inapata kufahamika ya kwamba waumini hawatozuiwa kumuona Mola wao. La sivyo ingelikuwa makafiri na waumini wote wawili ni sawa sawa Aakhirah. Allaah Ametofautisha kati yao. Amewapa ikram waumini ya kwamba Atajionyesha kwao na Kudhihiri kwao (Subhaanahu wa Ta´ala) kama inavyolingana na Utukufu na Ukubwa Wake. Watamuona kwa macho yao. Hawatosongamana kwa kumuona, yaani bi maana hawatokuwa na zahma wakati wa kumuona. Watamuona kwa macho yao kama jinsi wanavyoona jua kwenye anga lililo wazi bila ya mawingu, na hali kadhalika kama wauonavyo mwezi usiku wa mng´aro. Kama Hadiyth Swahiyh zilivyokuja juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya kumuona Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَة “Kwa wale waliofanya wema watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa (Jannah) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).” (Yuunus:26) “al-Husnaa” ni Pepo. “az-Ziyaadah” ni kuona Uso wa Allaah. Kama ilivyokuja katika Swahiyh Muslim. Kama Alivyosema tena (Ta´ala): لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ “Watapata humo wayatakayo, na Kwetu kuna yaliyo ziada (ya neema za Pepo na kumuona Allaah عز وجل ).” (Qaaf:35) “Watapata humo wayatakayo” yaani Peponi. “...na Kwetu kuna yaliyo ziada”, nako ni kumuona Allaah (´Azza wa Jalla). Kauli yake (Ta´ala): وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ ”(Baadhi ya) Nyuso siku hiyo zitanawiri.” (al-Qiyaamah:22) inatokana na neno “an-Nadhwrah”, nako ni kungaa. إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ ”Zikimtazama Mola wake.” (al-Qiyaamah:23) kwa macho yao. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 79-81

6- Sema “Atajionyesha Allaah kwa viumbe wazi kabisa

kama jinsi mwezi haufichikani basi na Mola Wako (ataonekana) wazi wazi.”

———————-

MAELEZO

Haya ni masuala ya kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Je, viumbe watamuona Allaah (´Azza wa Jalla) au hawatomuona? Jahmiyyah na Mu´tazilah wote wanapinga kuonekana kwa Allaah na wanasema kwamba Allaah Haonekani kwa kuwa kuonekana inakuwa kwa miili na Allaah sio mwili. Kwa hivyo hatoonekana. Wanapinga kuonekana kwa Allaah moja kwa moja, si duniani wala Aakhirah na tunamuomba Allaah afya.

Kuko watu pia wanaosema kwamba Allaah Anaonekana duniani na Aakhirah. Hii ni kauli ya baadhi ya Suufiyyah.

Kauli ya tatu – na ndio kauli ya haki – ni kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ataonekana Aakhirah. Watamuona watu wa Peponi kama jinsi Hadiyth kwa wingi zilivyothibiti juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama duniani hawezi kuonekana kwa kuwa watu hawana uwezo wa kumuona (Subhaanahu) duniani. Pindi Muusa (´alayhis-Swalaat was-Salaam) alipomuomba kumuona Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) duniani:

قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ
“Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.” Basi Mola wako Alipojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika; na Muwsaa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Subhaanak! (Utakaso ni Wako!) Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini” (al-A´raaf:143)

jibali liligeuka kuwa udongo kutokana na Ukubwa wa Allaah (´Azza wa Jalla). Vipi itakuwa kwa mwanaadamu kumuona Allaah? Hili ni kuhusu duniani.

Ama Aakhirah Allaah Atawapa watu wa Peponi nguvu ambazo wataweza kwa nguvu hizo kumuona Mola wao (´Azza wa Jalla). Hii ni ikram kwao. Pale ambapo walimuamini duniani na wala hawajamuona, Allaah Akawapa ikram na Atajionyesha Peponi ili wapate ladha ya kumuona. Kama jinsi hilo lilivyotolewa dalili na Qur-aan na Sunnah al-Mutawaatir.

Ama makafiri pale ambapo hawakumuamini duniani, Allaah Atajizuia wasimuone siku ya Qiyaamah. Anasema (Ta´ala):

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ
“Hapana! Hakika wao siku hiyo watawekewa kizuizi (wasimuone) Mola wao.” (al-Mutwaffifiyn:15)

Ikiwa makafiri wamewekewa kizuizi wasimuone Allaah, hapa inapata kufahamika ya kwamba waumini hawatozuiwa kumuona Mola wao. La sivyo ingelikuwa makafiri na waumini wote wawili ni sawa sawa Aakhirah. Allaah Ametofautisha kati yao. Amewapa ikram waumini ya kwamba Atajionyesha kwao na Kudhihiri kwao (Subhaanahu wa Ta´ala) kama inavyolingana na Utukufu na Ukubwa Wake. Watamuona kwa macho yao. Hawatosongamana kwa kumuona, yaani bi maana hawatokuwa na zahma wakati wa kumuona. Watamuona kwa macho yao kama jinsi wanavyoona jua kwenye anga lililo wazi bila ya mawingu, na hali kadhalika kama wauonavyo mwezi usiku wa mng´aro. Kama Hadiyth Swahiyh zilivyokuja juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya kumuona Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَة
“Kwa wale waliofanya wema watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa (Jannah) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).” (Yuunus:26)

“al-Husnaa” ni Pepo. “az-Ziyaadah” ni kuona Uso wa Allaah. Kama ilivyokuja katika Swahiyh Muslim. Kama Alivyosema tena (Ta´ala):

لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ
“Watapata humo wayatakayo, na Kwetu kuna yaliyo ziada (ya neema za Pepo na kumuona Allaah عز وجل ).” (Qaaf:35)

“Watapata humo wayatakayo” yaani Peponi.

“…na Kwetu kuna yaliyo ziada”, nako ni kumuona Allaah (´Azza wa Jalla).

Kauli yake (Ta´ala):

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ
”(Baadhi ya) Nyuso siku hiyo zitanawiri.” (al-Qiyaamah:22)

inatokana na neno “an-Nadhwrah”, nako ni kungaa.

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ
”Zikimtazama Mola wake.” (al-Qiyaamah:23)

kwa macho yao.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 79-81


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 14th, February 2014