Imaam Abu Bakr Kuhusu Kukufurisha Kwa Maasi

33- Wala usiwakufurishe watu wema hata kama wataasi (kufanya madhambi) wote wanafanya maasi na Dhul-´Arshiy Anawasamehe ----------------------------- MAELEZO Haya ni masuala ya Takfiyr (kukufurisha) watu wenye madhambi makubwa ambayo ni chini ya Shirki. Kumetokea tofauti kubwa baina ya Khawaarij na Murji-ah na baina ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Khawaarij wanakufurisha kwa madhambi makubwa ambayo ni chini ya Shirki, wanawadumisha wenye nayo Motoni na wanahalalisha damu na mali yao kwa kuzingatia ya kwamba ni makafiri. Wanatumia dalili kwa Aayah za matishio ambazo zimethibiti kutoa matishio juu ya madhambi na maasi, wanazitumia kuwakufurisha wale wenye kutenda maasi hayo. Mu´tazilah wanasema (mtenda dhambi kubwa) sio kafiri wala muumini, bali yuko katika manzilah baina ya manzilah mbili. Murji-ah wao wako kinyume. Dhambi kubwa kwao wanaonelea kuwa haidhuru imani na wala haiipunguzi. Mtenda dhambi kubwa kwao wanaonelea kuwa ni muumini mwenye imani kamilifu. Wanasema “Imani haidhuru pamoja na maasi kama ambavyo utiifu pamoja na kufuru haunufaishi”. Haya ndio madhehebu ya Murji-ah kwa njia ya ufupi. Kwa kuwa wao hawaingizi matendo katika imani. Mwenye kuacha wajibu, akafanya ya haramu au akafanya maasi makubwa au madogo chini ya Shirki, huyu ni mwenye imani kamilifu na wala maasi hayaipunguzi na wala wanaonelea kuwa hayamzidishii utiifu. Kwa kuwa imani kwao wanavyoonelea ni kitu kimoja, haizidi na wala haipungui. Haya ndio madhehebu ya Murji-ah ambayo yako kinyume na madhehebu ya Khawaarij. Wao wamechukua Aayah za ahadi na matarajio na wakaacha Aayah za matishio. Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wao wako katika haki na ukati na kati. Hawamkufurishi mtenda dhambi kubwa na wala hawasemi kuwa ana imani kamilifu, bali wanasema kuwa ni muumini lakini ni mwenye imani pungufu au ni muumini Faasiq. Ni muumini kwa imani yake na Faasiq kwa dhambi yake kubwa. Yuko chini ya Matakwa, bi maana Allaah Akipenda Atamsamehe na Akipenda Atamuadhibu. Kama Alivosema (Ta´ala): إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ “Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa; lakini Anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.” (an-Nisaa:48) Hata ikiwa Atamuadhibu hatomdumisha Motoni – kama wanavosema Khawaarij na Mu´tazilah – Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamejumuisha baina ya Aayah za ahadi (matarajio) na Aayah za matishio. Hawasemi kuwa maasi hayadhuru – kama wanavosema Murji-ah – na wala hawasemi kuwa (maasi) yanakufurisha – kama wanavosema Khawaarij. Wanasema kwamba maasi yanadhuru na yanaipunguza imani, lakini hata hivyo hayamtoi mwenye nayo katika Dini. Wamejumuisha baina ya maandiko. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya yule mwenye kutenda dhambi kubwa. Hii ndio maana ya kauli ya mwandishi “Wala usiwakufurishe watu wema”, yaani Ahl-ul-Qiblah katika waumini na waislamu. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 181-182

33- Wala usiwakufurishe watu wema hata kama wataasi (kufanya madhambi)

wote wanafanya maasi na Dhul-´Arshiy Anawasamehe

—————————–

MAELEZO

Haya ni masuala ya Takfiyr (kukufurisha) watu wenye madhambi makubwa ambayo ni chini ya Shirki. Kumetokea tofauti kubwa baina ya Khawaarij na Murji-ah na baina ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Khawaarij wanakufurisha kwa madhambi makubwa ambayo ni chini ya Shirki, wanawadumisha wenye nayo Motoni na wanahalalisha damu na mali yao kwa kuzingatia ya kwamba ni makafiri. Wanatumia dalili kwa Aayah za matishio ambazo zimethibiti kutoa matishio juu ya madhambi na maasi, wanazitumia kuwakufurisha wale wenye kutenda maasi hayo.

Mu´tazilah wanasema (mtenda dhambi kubwa) sio kafiri wala muumini, bali yuko katika manzilah baina ya manzilah mbili.

Murji-ah wao wako kinyume. Dhambi kubwa kwao wanaonelea kuwa haidhuru imani na wala haiipunguzi. Mtenda dhambi kubwa kwao wanaonelea kuwa ni muumini mwenye imani kamilifu. Wanasema “Imani haidhuru pamoja na maasi kama ambavyo utiifu pamoja na kufuru haunufaishi”. Haya ndio madhehebu ya Murji-ah kwa njia ya ufupi. Kwa kuwa wao hawaingizi matendo katika imani. Mwenye kuacha wajibu, akafanya ya haramu au akafanya maasi makubwa au madogo chini ya Shirki, huyu ni mwenye imani kamilifu na wala maasi hayaipunguzi na wala wanaonelea kuwa hayamzidishii utiifu. Kwa kuwa imani kwao wanavyoonelea ni kitu kimoja, haizidi na wala haipungui. Haya ndio madhehebu ya Murji-ah ambayo yako kinyume na madhehebu ya Khawaarij. Wao wamechukua Aayah za ahadi na matarajio na wakaacha Aayah za matishio.

Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wao wako katika haki na ukati na kati. Hawamkufurishi mtenda dhambi kubwa na wala hawasemi kuwa ana imani kamilifu, bali wanasema kuwa ni muumini lakini ni mwenye imani pungufu au ni muumini Faasiq. Ni muumini kwa imani yake na Faasiq kwa dhambi yake kubwa. Yuko chini ya Matakwa, bi maana Allaah Akipenda Atamsamehe na Akipenda Atamuadhibu. Kama Alivosema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa; lakini Anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.” (an-Nisaa:48)

Hata ikiwa Atamuadhibu hatomdumisha Motoni – kama wanavosema Khawaarij na Mu´tazilah – Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamejumuisha baina ya Aayah za ahadi (matarajio) na Aayah za matishio. Hawasemi kuwa maasi hayadhuru – kama wanavosema Murji-ah – na wala hawasemi kuwa (maasi) yanakufurisha – kama wanavosema Khawaarij. Wanasema kwamba maasi yanadhuru na yanaipunguza imani, lakini hata hivyo hayamtoi mwenye nayo katika Dini. Wamejumuisha baina ya maandiko. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya yule mwenye kutenda dhambi kubwa. Hii ndio maana ya kauli ya mwandishi “Wala usiwakufurishe watu wema”, yaani Ahl-ul-Qiblah katika waumini na waislamu.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 181-182


  • Kitengo: Uncategorized , Khawaarij
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 24th, February 2014