Imaam Abu Bakr Kuhusu Kuamini Qadar

28- Kwa Qadar iliyokadiriwa amini, kwani hakika ndio nguzo ya Dini na Dini ni wasaa (pana) ------------------------- MAELEZO Kuamini Qadar ni nguzo ya sita miongoni mwa nguzo za imani. Alikuja Jibriyl (´alayhis-Salaam) na kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nieleze juu ya imani: “Akasema “Imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya kuamini Qadar ni nguzo ya sita katika nguzo za imani. Kuamini Qadhwaa na Qadar ni kuamini Elimu ya Allaah (Jalla wa ´Alaa), Qadar Yake, mambo kabla ya kuwa kwake, Matendo ya Allaah (Jalla wa ´Alaa), Aliyotaka Allaah, Utashi Wake, Uumbaji Wake na kufanya Kwake kupatikana kwa vitu. Hili ni jambo kubwa. Katika Qur-aan Kauli Yake (Ta´ala): وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا “Na Ameumba kila kitu; kisha Akakikadiria kipimo sawa sawa.” (al-Furqaan:02) إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ”Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa makadirio.” (al-Qamar:49) yaani maana yake tumekadiria kutokea kwake na kutaka kutoka kwake na Akaviumba, Akakadiria sifa zake na wakati wake ambapo vitatokea. Kila kitu kimekadiriwa katika njia zake zote mbali mbali: 1- Kwa njia ya kuvijua. 2- Kwa njia ya kuviandika katika Lawh al-Mahfuudhw. 3- Kwa njia ya Kuvitaka Allaah (kutokea kwake) kwa wakati wake. 4- Kwa njia ya kuviumba na kufanya kupatikana kwake. Kila kitu kina sifa zake ambazo Amezijaalia kwa kitu hicho, hakizidi hapo na wala hakipungui. Ni kitu kilichokadiriwa. Kama Alivyosema Allaah juu ya mvua: وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ “Na Hatukiteremshi isipokuwa kwa kadiri maalumu.” (al-Hijr:21) Mvua ni maalum kiasi chake, mahala itapoteremka na wakati itateremka. Ameamua (Jalla wa ´Alaa) kwa njia zake zote. Hakuna kitu isipokuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amekijua, Akakiumba na Akakikadiria. Hakikupatikana bila ya kuumbwa, pasina kutanguliwa kukadiriwa, pasina kuandika katika Lawh al-Mahfuudhw, pasina Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kukitaka. Mambo ambayo yamepatikana sio mambo ya vurugu, isipokuwa ni mambo yaliyodhibitiwa kwa Kukadiriwa na Allaah, kufanya yakapatikana na kutaka yapatikane kwa sifa zake zinazopatikana katika kitu hicho. Hili ni jambo muhimu sana. Kuamini Qadhwaa na Qadar kuna wengi wenye fahamu wamepotea miongoni mwa wenye fahamu na elimu katika watu ambao hawakutazama Aayah za Qur-aan na katika Hadiyth za Mtume, isipokuwa walitegemea akili yao na fikira zao, hivyo wakachanganyikiwa katika mambo ya Qadhwaa na Qadar. Allaah Akawaongoza Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakaiamini kwa njia ambayo Ametaka Allaah na kupanga juu ya waja Wake kwa mujibu wa maandiko ya Kitabu na Sunnah, kama ilivo ada yao katika kila mlango wa mambo ya ´Aqiydah. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 134-137

28- Kwa Qadar iliyokadiriwa amini, kwani hakika

ndio nguzo ya Dini na Dini ni wasaa (pana)

————————-

MAELEZO

Kuamini Qadar ni nguzo ya sita miongoni mwa nguzo za imani. Alikuja Jibriyl (´alayhis-Salaam) na kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nieleze juu ya imani: “Akasema

“Imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya kuamini Qadar ni nguzo ya sita katika nguzo za imani. Kuamini Qadhwaa na Qadar ni kuamini Elimu ya Allaah (Jalla wa ´Alaa), Qadar Yake, mambo kabla ya kuwa kwake, Matendo ya Allaah (Jalla wa ´Alaa), Aliyotaka Allaah, Utashi Wake, Uumbaji Wake na kufanya Kwake kupatikana kwa vitu. Hili ni jambo kubwa. Katika Qur-aan Kauli Yake (Ta´ala):

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا
“Na Ameumba kila kitu; kisha Akakikadiria kipimo sawa sawa.” (al-Furqaan:02)

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ
”Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa makadirio.” (al-Qamar:49)

yaani maana yake tumekadiria kutokea kwake na kutaka kutoka kwake na Akaviumba, Akakadiria sifa zake na wakati wake ambapo vitatokea. Kila kitu kimekadiriwa katika njia zake zote mbali mbali:

1- Kwa njia ya kuvijua.
2- Kwa njia ya kuviandika katika Lawh al-Mahfuudhw.
3- Kwa njia ya Kuvitaka Allaah (kutokea kwake) kwa wakati wake.
4- Kwa njia ya kuviumba na kufanya kupatikana kwake.

Kila kitu kina sifa zake ambazo Amezijaalia kwa kitu hicho, hakizidi hapo na wala hakipungui. Ni kitu kilichokadiriwa. Kama Alivyosema Allaah juu ya mvua:

وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ
“Na Hatukiteremshi isipokuwa kwa kadiri maalumu.” (al-Hijr:21)

Mvua ni maalum kiasi chake, mahala itapoteremka na wakati itateremka. Ameamua (Jalla wa ´Alaa) kwa njia zake zote.

Hakuna kitu isipokuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amekijua, Akakiumba na Akakikadiria. Hakikupatikana bila ya kuumbwa, pasina kutanguliwa kukadiriwa, pasina kuandika katika Lawh al-Mahfuudhw, pasina Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kukitaka. Mambo ambayo yamepatikana sio mambo ya vurugu, isipokuwa ni mambo yaliyodhibitiwa kwa Kukadiriwa na Allaah, kufanya yakapatikana na kutaka yapatikane kwa sifa zake zinazopatikana katika kitu hicho. Hili ni jambo muhimu sana.

Kuamini Qadhwaa na Qadar kuna wengi wenye fahamu wamepotea miongoni mwa wenye fahamu na elimu katika watu ambao hawakutazama Aayah za Qur-aan na katika Hadiyth za Mtume, isipokuwa walitegemea akili yao na fikira zao, hivyo wakachanganyikiwa katika mambo ya Qadhwaa na Qadar. Allaah Akawaongoza Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakaiamini kwa njia ambayo Ametaka Allaah na kupanga juu ya waja Wake kwa mujibu wa maandiko ya Kitabu na Sunnah, kama ilivo ada yao katika kila mlango wa mambo ya ´Aqiydah.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 134-137


  • Kitengo: Uncategorized , Qadar
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014