Imaam Abu Bakr Kuhusu Fadhila Za Taabi´uun Na Maimamu Wa Taabi´uun

24- Baada yao ni Taabi´uun, kwa kuwafuata kwao kwa wema na matendo yao; kimaneno na vitendo wakawa wenye kufaulu 25- Na Maalik na kisha ndugu yao Abu ´Amr al-Awzaa´iy walotakasika 26- Baada yao ni ash-Shaafi´iy na Ahmad ni kiongozi wa haki na anayeifuata haki na kunasihi 27- Hawa ni watu ambao Allaah Amewasamehe hivyo basi wapende utakuja kufurahi ------------------- MAELEZO Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “Baada yao ni Taabi´uun, kwa kuwafuata kwao kwa wema”, baada ya Maswahabah kunakuja Taabi´uun. Anasema (Ta´ala): وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ “Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan.” (at-Tawbah:100) Kauli Yake: وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ “Na wale waliowafuata kwa ihsaan.” Inakusanya ndani yake kila ambaye atawafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah. Lakini inaposemwa at-Taabi´iy, makusudio ni aliyejifunza kutoka kwa Maswahabah na akapokea kutoka kwao. La sivyo ni kwamba (Aayah hiyo) inakusanya kila ambaye atawafuata (kwa wema) na akapita juu ya uongofu wa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao. Kwa ajili hii ndio maana Akasema (Jalla wa ´Alaa) – pindi alipotaja Mujaahiruun na Answaar – kisha Akasema: وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ “Na wale waliokuja baada yao (wenye) kusema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.) kwa wale walioamini; Mola wetu! Hakika Wewe ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).” (al-Hashr:10) Katika Aayah hii kuna Radd kwa Raafidhwah ambao wanawachukia Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa nyoyo zao na wanatamka kwa ndimi zao. Sivyo tu bali wanawalaani na wanawakufurisha Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hili amesema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah): “Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah al-Jamaa´ah ni wenye kusalimisha nyoyo zao na ndimi zao kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Kusalimisha nyoyo zao, kutokana na Kauli Yake: وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا “... na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.).” (al-Hashr:10) Kusalimisha ndimi zao, kutokana na Kauli Yake: يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ “Wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan.” (al-Hashr:10) katika Aayah hii kuna kuzisalimisha nyoyo na ndimi kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio Manhaj (Mfumo) wa wenye kuwafuata kwa wema. Ama yule mwenye kuwajeruhi, kuwatafuta mapungufu yao, kuwekea mashaka fadhila za Maswahabah, akawakufurisha au akawalaani, huyu anaenda kinyume na uongofu wa Uislamu na ni adui wa Uislamu na ni adui wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa wakitukanywa Maswahabah zake ndio kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile ni kuitukana Qur-aan inayowasifu na kuwatapa. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 131-132

24- Baada yao ni Taabi´uun, kwa kuwafuata kwao kwa wema

na matendo yao; kimaneno na vitendo wakawa wenye kufaulu

25- Na Maalik na kisha ndugu yao
Abu ´Amr al-Awzaa´iy walotakasika

26- Baada yao ni ash-Shaafi´iy na Ahmad

ni kiongozi wa haki na anayeifuata haki na kunasihi

27- Hawa ni watu ambao Allaah Amewasamehe

hivyo basi wapende utakuja kufurahi

——————-

MAELEZO

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “Baada yao ni Taabi´uun, kwa kuwafuata kwao kwa wema”, baada ya Maswahabah kunakuja Taabi´uun. Anasema (Ta´ala):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ
“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan.” (at-Tawbah:100)

Kauli Yake:

وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ
“Na wale waliowafuata kwa ihsaan.”

Inakusanya ndani yake kila ambaye atawafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah. Lakini inaposemwa at-Taabi´iy, makusudio ni aliyejifunza kutoka kwa Maswahabah na akapokea kutoka kwao. La sivyo ni kwamba (Aayah hiyo) inakusanya kila ambaye atawafuata (kwa wema) na akapita juu ya uongofu wa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao. Kwa ajili hii ndio maana Akasema (Jalla wa ´Alaa) – pindi alipotaja Mujaahiruun na Answaar – kisha Akasema:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Na wale waliokuja baada yao (wenye) kusema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.) kwa wale walioamini; Mola wetu! Hakika Wewe ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno – Mwenye kurehemu).” (al-Hashr:10)

Katika Aayah hii kuna Radd kwa Raafidhwah ambao wanawachukia Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa nyoyo zao na wanatamka kwa ndimi zao. Sivyo tu bali wanawalaani na wanawakufurisha Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hili amesema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

“Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah al-Jamaa´ah ni wenye kusalimisha nyoyo zao na ndimi zao kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Kusalimisha nyoyo zao, kutokana na Kauli Yake:

وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا
“… na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo (ya chuki, uadui, uhasidi, n.k.).” (al-Hashr:10)

Kusalimisha ndimi zao, kutokana na Kauli Yake:

يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ
“Wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan.” (al-Hashr:10)

katika Aayah hii kuna kuzisalimisha nyoyo na ndimi kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio Manhaj (Mfumo) wa wenye kuwafuata kwa wema.

Ama yule mwenye kuwajeruhi, kuwatafuta mapungufu yao, kuwekea mashaka fadhila za Maswahabah, akawakufurisha au akawalaani, huyu anaenda kinyume na uongofu wa Uislamu na ni adui wa Uislamu na ni adui wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa wakitukanywa Maswahabah zake ndio kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile ni kuitukana Qur-aan inayowasifu na kuwatapa.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 131-132


  • Kitengo: Uncategorized , Shiy´ah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014