Imaam Abu Bakr bin Abiy Daawuud Kuhusu Imani

Kauli ya mwandishi - Imaam Abu Bakr - (Rahimahu Allaah) “Sema “Hakika ya Imani ni Kauli na nia”, hii ni kauli ya tatu, yaani achana na rai ya Khawaarij na achana na rai ya Murji-ah na badala yake sema kauli ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah: “Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo; inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi.” Hii ndio tafsiri kamilifu iliyochukuliwa kutoka katika dalili na sio kutoka katika matamanio na mawazo. Imani inakuwa kwa mambo haya matatu: 1- Kutamka kwa ulimi. 2- Kuamini moyoni. 3- Matendo ya viungo. 4- Inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. - Imani haiwi moyoni tu, kama wanavyosema ´Ashaa´irah. - Au wanaosema kwamba imani inakuwa kwa kuamini moyoni pamoja na kutamka kwa ulimi, kama wanavyosema Hanafiyyah. - Au ni kutamka kwa ulimi tu, kama wanavyosema Karraamiyyah. - Au ni kule kuwa na maarifa (utambuzi), kama wanavyosema Jahmiyyah. Katika madhehebu haya machafu yanalazimisha Fir´awn kuwa muumini, kwa kuwa anajua kwa moyo wake kwa yale yaliyokuja na Muusa (´alayhis-Salaam): لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ “Kwa yakini umekwishajua kwamba hakuna Aliyeteremsha haya isipokuwa Mola wa mbingu na ardhi.” (al-Israa´:102) Fir´awn anajua hili ndani ya moyo wake, lakini alilipinga kwa ulimi wake kwa ajili ya kiburi na kwa ajili ya kutaka kubaki katika ufalme wake na akawekea kiburi yale yaliyokuja na Muusa (´alayyhis-Salaam). Hali kadhalika washirikina wanatambua kwa mioyo yao ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah na kwamba yuko juu ya haki. Anasema (Ta´ala): قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖفَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ “Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha (kwa ujeuri) Aayah za Allaah.” (al-An´aam:33) Wao hawamkadhibishi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini linalowafanya kwenda kinyume ni kufuru, kiburi, kuwa na jeuri juu ya haki na kasumba kwa batili kama ilivyokuwa kwa Abu Twaalib ami ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 187-189

Kauli ya mwandishi – Imaam Abu Bakr – (Rahimahu Allaah) “Sema “Hakika ya Imani ni Kauli na nia”, hii ni kauli ya tatu, yaani achana na rai ya Khawaarij na achana na rai ya Murji-ah na badala yake sema kauli ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah:

“Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo; inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi.”

Hii ndio tafsiri kamilifu iliyochukuliwa kutoka katika dalili na sio kutoka katika matamanio na mawazo. Imani inakuwa kwa mambo haya matatu:

1- Kutamka kwa ulimi.
2- Kuamini moyoni.
3- Matendo ya viungo.
4- Inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi.

– Imani haiwi moyoni tu, kama wanavyosema ´Ashaa´irah.

– Au wanaosema kwamba imani inakuwa kwa kuamini moyoni pamoja na kutamka kwa ulimi, kama wanavyosema Hanafiyyah.

– Au ni kutamka kwa ulimi tu, kama wanavyosema Karraamiyyah.

– Au ni kule kuwa na maarifa (utambuzi), kama wanavyosema Jahmiyyah. Katika madhehebu haya machafu yanalazimisha Fir´awn kuwa muumini, kwa kuwa anajua kwa moyo wake kwa yale yaliyokuja na Muusa (´alayhis-Salaam):

لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ
“Kwa yakini umekwishajua kwamba hakuna Aliyeteremsha haya isipokuwa Mola wa mbingu na ardhi.” (al-Israa´:102)

Fir´awn anajua hili ndani ya moyo wake, lakini alilipinga kwa ulimi wake kwa ajili ya kiburi na kwa ajili ya kutaka kubaki katika ufalme wake na akawekea kiburi yale yaliyokuja na Muusa (´alayyhis-Salaam). Hali kadhalika washirikina wanatambua kwa mioyo yao ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah na kwamba yuko juu ya haki. Anasema (Ta´ala):

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖفَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ
“Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha (kwa ujeuri) Aayah za Allaah.” (al-An´aam:33)

Wao hawamkadhibishi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini linalowafanya kwenda kinyume ni kufuru, kiburi, kuwa na jeuri juu ya haki na kasumba kwa batili kama ilivyokuwa kwa Abu Twaalib ami ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 187-189


  • Kitengo: Uncategorized , Ashaa´irah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 27th, February 2014