Ibn Uthaymiyn Kuhusu Uso Wa Allaah

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anasema: "Kitu pekee ambacho mtu huomba kwacho Uso wa Allaah ni Pepo." Hapa kunathibitishwa Uso wa Allaah ('Azza wa Jalla). Limethibiti katika Qur-aan, Sunnah na Ijmaa´. Katika Qur-aan miongoni mwazo kuna: كل شيء هالك إلا وجهه “Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.” والذين صبروا ابتغاء وجه ربهم ”Na ambao wamesubiri kutaka Uso wa Mola wao.” Kuna Aayah nyingi mfano wa hizi. Ama kuhusu Sunnah, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anasema: "Naomba kinga kwa Uso wako." Watu wametofautiana juu ya Uso ambao Allaah Amejithibitishia Kwake Mwenyewe. Je, ni kweli au ni muelezo wa Chake kwa vile hana Uso au ni usemi wa kitu ambacho mtu anataka kukipata kwa ajili ya Uso Wake, au ni mwelekeo Wake au ujira? Kuna Ikhtilaaf, lakini Allaah Kawaongoza waumini waliosema kuwa Uso ni wa halisi kwa sababu Allaah (Ta´ala) Kasema: ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام "Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.” Kasema pia: تبارك اسم ربك ذي الجلال والإكرام "Limetukuka Jina la Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.” ذي ni Sifa ya Mola (Allaah) na si jina. ذو ni Sifa ya Uso na si ya Bwana. Ikiwa ni Uso ndio umeelezwa kwa ukuu na utukufu, hivyo haiwezi kuwa na maana ya thawabu, mwelekeo au kiini tu kwa vile Uso sio kiini. Wanaokanusha wanasema kwamba Uso unamaanisha kiini, mwelekeo au thawabu. Wanasema kwamba ikiwa mtu atamthibitishia Uso halisi, itakuwa na maana ya kwamba Allaah ana mwili na miili yote inafanana. Kwa hivyo, itakuwa na maana kwamba mtu anafanana na Allaah wakati Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema: ليس كمثله شيء وهو السميع البصير "Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” Kusema kwamba kuna mtu kama Allaah ina maana Qur-aan inadanganya. Isitoshe wanasema kuwa sisi, Ahl-us-Sunnah, tunasema kwamba yule anayemfananisha Allaah ni kafiri. Wanarapigwa Radd namna hii: Kwanza: Mnamaanisha nini kwa "mwili" mnaoukimbia [kuuthibitisha]? Je, mnamaanisha mwili uliojumuisha miguu, mifupa na damu vinavyohitajiana baadhi yavyo? Ikiwa ni hili ndio mnalomaanisha, tunakubaliana na nyinyi ya kwamba Allaah Hayuko namna hiyo. Ni jambo lisilowezekana Yeye kuwa namna hiyo. Na kama mnamaanisha Dhati halisi (iliyo) na Sifa kamilifu, hakuna ubaya kwa hilo. Pili: Ikiwa mnasema ya kwamba miili yote inafanana, basi huu ni uongo mkubwa sana. Je, mwili wa dubu na mdudu chungu vinafanana? Kuna tofauti kubwa kati ya hivyo viwili tunapokuja katika kipimo, uzito, wembamba, n.k. Ikiwa hoja hii imeanguka, basi hali kadhalika matukio pia yameanguka, nayo ni kuwa Allaah Anafanana na viumbe Vyake. Isitoshe, tunaona jinsi hata binadamu wana nyuso tofauti. Huwezi kupata watu wawili na nyuso za kufanana kabisa hata kama watakuwa ni mapacha. Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd (2/357)

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) anasema:

“Kitu pekee ambacho mtu huomba kwacho Uso wa Allaah ni Pepo.”

Hapa kunathibitishwa Uso wa Allaah (‘Azza wa Jalla). Limethibiti katika Qur-aan, Sunnah na Ijmaa´. Katika Qur-aan miongoni mwazo kuna:

كل شيء هالك إلا وجهه
“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.”

والذين صبروا ابتغاء وجه ربهم
”Na ambao wamesubiri kutaka Uso wa Mola wao.”

Kuna Aayah nyingi mfano wa hizi.

Ama kuhusu Sunnah, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) anasema:

“Naomba kinga kwa Uso wako.”

Watu wametofautiana juu ya Uso ambao Allaah Amejithibitishia Kwake Mwenyewe. Je, ni kweli au ni muelezo wa Chake kwa vile hana Uso au ni usemi wa kitu ambacho mtu anataka kukipata kwa ajili ya Uso Wake, au ni mwelekeo Wake au ujira? Kuna Ikhtilaaf, lakini Allaah Kawaongoza waumini waliosema kuwa Uso ni wa halisi kwa sababu Allaah (Ta´ala) Kasema:

ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام
“Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”

Kasema pia:

تبارك اسم ربك ذي الجلال والإكرام
“Limetukuka Jina la Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”

ذي ni Sifa ya Mola (Allaah) na si jina. ذو ni Sifa ya Uso na si ya Bwana. Ikiwa ni Uso ndio umeelezwa kwa ukuu na utukufu, hivyo haiwezi kuwa na maana ya thawabu, mwelekeo au kiini tu kwa vile Uso sio kiini.
Wanaokanusha wanasema kwamba Uso unamaanisha kiini, mwelekeo au thawabu. Wanasema kwamba ikiwa mtu atamthibitishia Uso halisi, itakuwa na maana ya kwamba Allaah ana mwili na miili yote inafanana. Kwa hivyo, itakuwa na maana kwamba mtu anafanana na Allaah wakati Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema:

ليس كمثله شيء وهو السميع البصير
“Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.”

Kusema kwamba kuna mtu kama Allaah ina maana Qur-aan inadanganya. Isitoshe wanasema kuwa sisi, Ahl-us-Sunnah, tunasema kwamba yule anayemfananisha Allaah ni kafiri. Wanarapigwa Radd namna hii:

Kwanza: Mnamaanisha nini kwa “mwili” mnaoukimbia [kuuthibitisha]? Je, mnamaanisha mwili uliojumuisha miguu, mifupa na damu vinavyohitajiana baadhi yavyo? Ikiwa ni hili ndio mnalomaanisha, tunakubaliana na nyinyi ya kwamba Allaah Hayuko namna hiyo. Ni jambo lisilowezekana Yeye kuwa namna hiyo. Na kama mnamaanisha Dhati halisi (iliyo) na Sifa kamilifu, hakuna ubaya kwa hilo.

Pili: Ikiwa mnasema ya kwamba miili yote inafanana, basi huu ni uongo mkubwa sana. Je, mwili wa dubu na mdudu chungu vinafanana? Kuna tofauti kubwa kati ya hivyo viwili tunapokuja katika kipimo, uzito, wembamba, n.k. Ikiwa hoja hii imeanguka, basi hali kadhalika matukio pia yameanguka, nayo ni kuwa Allaah Anafanana na viumbe Vyake.

Isitoshe, tunaona jinsi hata binadamu wana nyuso tofauti. Huwezi kupata watu wawili na nyuso za kufanana kabisa hata kama watakuwa ni mapacha.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd (2/357)


  • Kitengo: Uncategorized , Uso wa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013