Ibn Taymiyyah Kuhusu Manyoa Ya Mbwa Ni Masafi

Kuhusu manyoa ya mbwa na kama ni najisi au hapana, wanachuoni wana rai mbili juu ya hilo na hali kadhalika Ahmad. Je, ni lazima kuondosha [maji ya] kisima ikiwa mbwa itatupa manyoa yake ndani? Ni lazima kuyaondosha kwa mujibu wa wale ambao wanaonelea kuwa manyoa imeyanajisi [imeyachafua] maji. Wanachuoni wa Kuufah wana rai hii kama Abu Haniyfah. Wanachuoni wengine wanasema kuwa maji yanakuwa najisi tu pale ambapo yanabadilika. Rai hii ni ya jamhuri (wanachuoni wengi). Katika hali hiyo, inaruhusiwa kuyatumia [hayo maji] hata kama yatakuwa na manyoa ya mbwa. Rai hii ni yale wanaosema kuwa manyoa ya mbwa ni masafi. Inaonekana kuwa rai sahihi zaidi ni kwamba manyoa ya mbwa ni masafi kwa kule kutokuwa na dalili yoyote ya kuthibitisha juu ya hilo kutoka katika Shari'ah. Mwandishi: Shaykh-ul-Islâm Ahmad bin Taymiyyah Chanzo: Mukhtasar-ul-Fataawaa al-Misriyyah (1/77) Ufupisho: Imaam Badr-ud-Diyn Muhammad bin ´Aliy al-Hanbaliy al-Ba´liy (d. 777)

Kuhusu manyoa ya mbwa na kama ni najisi au hapana, wanachuoni wana rai mbili juu ya hilo na hali kadhalika Ahmad.

Je, ni lazima kuondosha [maji ya] kisima ikiwa mbwa itatupa manyoa yake ndani? Ni lazima kuyaondosha kwa mujibu wa wale ambao wanaonelea kuwa manyoa imeyanajisi [imeyachafua] maji. Wanachuoni wa Kuufah wana rai hii kama Abu Haniyfah.

Wanachuoni wengine wanasema kuwa maji yanakuwa najisi tu pale ambapo yanabadilika. Rai hii ni ya jamhuri (wanachuoni wengi). Katika hali hiyo, inaruhusiwa kuyatumia [hayo maji] hata kama yatakuwa na manyoa ya mbwa. Rai hii ni yale wanaosema kuwa manyoa ya mbwa ni masafi.

Inaonekana kuwa rai sahihi zaidi ni kwamba manyoa ya mbwa ni masafi kwa kule kutokuwa na dalili yoyote ya kuthibitisha juu ya hilo kutoka katika Shari’ah.

Mwandishi: Shaykh-ul-Islâm Ahmad bin Taymiyyah
Chanzo: Mukhtasar-ul-Fataawaa al-Misriyyah (1/77)
Ufupisho: Imaam Badr-ud-Diyn Muhammad bin ´Aliy al-Hanbaliy al-Ba´liy (d. 777)


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 19th, December 2013