Ibn Khuzaymah Kuhusu Uso Wa Allaah

Mlango: Yanayothibitisha Uso wa Allaah ambao Ameuelezea kwa enzi na utukufu: ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام "Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.” Amethibitisha kwamba Yeye Atabaki wakati vyengine vyote atavyoaumua vitatoweka, kuangamia. Ametakasika Yeye katika utukufu Wake ambaye hakuna chochote katika Sifa Zake kitachotoweka. Anasema (Jalla wa ´Alaa): ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام "Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.” Kasema: كل شيء هالك إلا وجهه "Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.” Anasema (Ta´ala) kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): واصبر نفسك مع الذين يدعون ربهم بالغداة والعشي يريدون وجهه "Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao asubuhi na jioni, wanataka Uso Wake.” Kasema (Ta´ala): ولله المشرق والمغرب فأينما تولوا فثم وجه الله "Na ni (milki) ya Allaah Mashariki na Magharibi; basi popote mnapogeuka kuna Uso wa Allaah.” Kwa hivyo, Kajithibitishia Yeye Mwenyewe Uso na Kaueleza kwa enzi na utukufu. Kathibitisha kwamba Uso Wake utabakia na kukanusha kuwa vitatoweka. Sisi na wanachuoni wengine wote wa Hijaaz, Tuhaamah, Yemen, Iraaq, Shaam na Misri tunamthibitishia Allaah yale Aliyojithibitishia Yeye Mwenyewe. Tunathibitisha hilo kwa ndimi zetu na kuuamini hilo kwa mioyo yetu. Tunatakiwa kufanya hilo bila ya kufananisha Uso wa Muumba Wetu na viumbe. Ametakasika Allaah kwa kufanana na viumbe Vyake. Ametakasika Allaah kuwa kama jinsi wakanushaji wanavyosema. Ametakasika Allaah kwa kutokuwa kitu, wasemalo waongo. Kwa kuwa kinachokosa sifa si lolote si chochote. Ametakasika Allaah kwa yale wayasemayo Jahmiyyah. Wanakanusha kabisa Sifa za Mola Wetu Alizojithibitishia Yeye Mwenyewe katika maandiko Yake na kupitia Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Mwandishi: Imaam Abu Bakr bin Khuzaymah (d. 311) Chanzo: Kitaab-ut-Tawhiyd (1/24-26)

Mlango: Yanayothibitisha Uso wa Allaah ambao Ameuelezea kwa enzi na utukufu:

ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام
“Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”

Amethibitisha kwamba Yeye Atabaki wakati vyengine vyote atavyoaumua vitatoweka, kuangamia. Ametakasika Yeye katika utukufu Wake ambaye hakuna chochote katika Sifa Zake kitachotoweka. Anasema (Jalla wa ´Alaa):

ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام
“Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”

Kasema:

كل شيء هالك إلا وجهه
“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.”

Anasema (Ta´ala) kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
واصبر نفسك مع الذين يدعون ربهم بالغداة والعشي يريدون وجهه
“Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao asubuhi na jioni, wanataka Uso Wake.”

Kasema (Ta´ala):

ولله المشرق والمغرب فأينما تولوا فثم وجه الله
“Na ni (milki) ya Allaah Mashariki na Magharibi; basi popote mnapogeuka kuna Uso wa Allaah.”

Kwa hivyo, Kajithibitishia Yeye Mwenyewe Uso na Kaueleza kwa enzi na utukufu. Kathibitisha kwamba Uso Wake utabakia na kukanusha kuwa vitatoweka.

Sisi na wanachuoni wengine wote wa Hijaaz, Tuhaamah, Yemen, Iraaq, Shaam na Misri tunamthibitishia Allaah yale Aliyojithibitishia Yeye Mwenyewe. Tunathibitisha hilo kwa ndimi zetu na kuuamini hilo kwa mioyo yetu. Tunatakiwa kufanya hilo bila ya kufananisha Uso wa Muumba Wetu na viumbe. Ametakasika Allaah kwa kufanana na viumbe Vyake. Ametakasika Allaah kuwa kama jinsi wakanushaji wanavyosema. Ametakasika Allaah kwa kutokuwa kitu, wasemalo waongo. Kwa kuwa kinachokosa sifa si lolote si chochote. Ametakasika Allaah kwa yale wayasemayo Jahmiyyah. Wanakanusha kabisa Sifa za Mola Wetu Alizojithibitishia Yeye Mwenyewe katika maandiko Yake na kupitia Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr bin Khuzaymah (d. 311)
Chanzo: Kitaab-ut-Tawhiyd (1/24-26)


  • Kitengo: Uncategorized , Uso wa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013