Ibn Hajar Kuhusu Bid´ah Nzuri Ya Maadhimisho Ya Maulidi

Vilevile kama alivyonukuu as-Suyuutwiy, anasema Ibn Hajar kwanza kuwa sherehe ya Maulidi ni Bid´ah ambayo haikuthibiti kutoka kwa Salaf yoyote. Sentensi hii ya Ibn Hajar inatosha kuyahukumu Maulidi. Yangelikuwa mazuri, Maswahabah, waliokuja baada yao, na maimamu baada yao wangeliyasherehekea. Kisha Ibn Hajar akasema: "Lakini ikiwa jambo hili lina mazuri na mabaya, hivyo ni Bid´ah nzuri ikiwa mtu atafanya hayo mambo mazuri na kuepuka hayo mabaya na vinginevyo hapana." Kasema pia: "Naamini ya kwamba jambo hili lina msingi imara. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alipoenda al-Madiynah, alikuta mayahudi wanafunga siku ya Aashuura´. Akawauliza kuhusu hilo na wao wakasema wanafunga siku hiyo kumshukuru Allaah kwa kumuokoa Muusa na kumuangamiza Fir´awn siku hiyo. Kutokana na hili, tunapata kujua ya kwamba ni sahihi kumshukuru Allaah kwa siku fulani Kaneemesha au Kuondosha mabaya na kwamba inaweza kufanywa siku hiyo hiyo mwaka baada ya mwaka. " Ambayo anasema Ibn Hajar yanaradiwa na maneno yake ya kwanza, nayo ni kwamba sherehe ya Maulidi ni Bid´ah ambayo haikuthibiti kutoka kwa Salaf yoyote. Nimekwishataja Aayah na Hadiyth zinazokataza na kutahadharisha Bid´ah na kubainisha kwamba hayakubaliwi. Kuna Radd ya kutosha kwa maneno ya mwisho ya Ibn Hajar. Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy ar-Radd al-Qawiy, uk. 30-31

Vilevile kama alivyonukuu as-Suyuutwiy, anasema Ibn Hajar kwanza kuwa sherehe ya Maulidi ni Bid´ah ambayo haikuthibiti kutoka kwa Salaf yoyote. Sentensi hii ya Ibn Hajar inatosha kuyahukumu Maulidi. Yangelikuwa mazuri, Maswahabah, waliokuja baada yao, na maimamu baada yao wangeliyasherehekea. Kisha Ibn Hajar akasema:

“Lakini ikiwa jambo hili lina mazuri na mabaya, hivyo ni Bid´ah nzuri ikiwa mtu atafanya hayo mambo mazuri na kuepuka hayo mabaya na vinginevyo hapana.”
Kasema pia:

“Naamini ya kwamba jambo hili lina msingi imara. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea ya kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipoenda al-Madiynah, alikuta mayahudi wanafunga siku ya Aashuura´. Akawauliza kuhusu hilo na wao wakasema wanafunga siku hiyo kumshukuru Allaah kwa kumuokoa Muusa na kumuangamiza Fir´awn siku hiyo. Kutokana na hili, tunapata kujua ya kwamba ni sahihi kumshukuru Allaah kwa siku fulani Kaneemesha au Kuondosha mabaya na kwamba inaweza kufanywa siku hiyo hiyo mwaka baada ya mwaka. ”

Ambayo anasema Ibn Hajar yanaradiwa na maneno yake ya kwanza, nayo ni kwamba sherehe ya Maulidi ni Bid´ah ambayo haikuthibiti kutoka kwa Salaf yoyote. Nimekwishataja Aayah na Hadiyth zinazokataza na kutahadharisha Bid´ah na kubainisha kwamba hayakubaliwi. Kuna Radd ya kutosha kwa maneno ya mwisho ya Ibn Hajar.

Mwandishi: ‘Allaamah Hamuud bin ‘Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 30-31


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013