Ibn Battah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah

Shikamaneni na elimu yenu – Allaah Awarehemu – ya kwamba ni katika sifa ya watu wa haki kumthibitishia na kukubali mapokezi sahihi bila ya kupinga kwa kulinganisha na maoni na matamanio. Imani ni kuthibitisha na muumini anathibitisha. Allaah ('Azza wa Jalla) kasema: فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ”Basi Naapa kwa Mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu (mwamuzi) katika yale wanayotofautiana baina yao, kisha wasione katika nyoyo zao uzito katika uliyohukumu na wajisalimishe kwa unyenyekevu.” Katika sifa ya waumini ni kwamba wanamsifia Allaah kama jinsi Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Alivyojisifia Yeye Mwenyewe na kama jinsi Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomsifia kupitia yale ambayo yamesimuliwa na wanachuoni na kupokelewa na wapokezi waaminifu. Wanatoa dalili kwa yale waliyopokea kwa yale mazuri na yasiokuwa mazuri, ya mila na mapokezi. Hakusemwi kwa yale ya sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) "Vipi?" au "Kwa nini?". Wanafuata na hawazushi. Wanajisalimisha na hawana kipingamizi. Wametosheka na hawana shaka. Katika mambo ya sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kupitia wapokezi waaminifu na ambayo waumini ni lazima wayaamini na ni Haramu kwenda kinyume chake, ni [kuamini kwamba] Allaah (Ta´ala) Anacheka. Linakanushwa na analikanusha tu mtu wa Bid´ah ambaye hali yake imehukumiwa na wanachuoni. Huyu ni katika yale mapote yaliyopotea na maoni kutelekezwa na maoni yaliyokataliwa – Allaah Atulinde sisi na nyinyi na Bid´ah zote na upotevu. 67 - Abu Raziyn al-'Uqayliy (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Mola Wetu Anacheka kwa maelezo ya waja Wake wakati kubadilika Kwake kwa kweli kuko karibu." Nikasema: “Je Mola Wetu Anacheka ewe Mtume wa Allaah?" Akasema: "Ndiyo." Kisha akasema: "Basi Mola Ambaye Anacheka hatotunyima kamwe kitu kizuri." 68 - Abu Muusa al-Ash'ariy (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Mola Wetu Atajidhihirisha kwetu siku ya Qiyaamah Akicheka.” Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Allaah (Ta´ala) Anawacheka watu wawili. Mmoja wao anamuua mwenzake na wote wawili wanaingia Peponi. Yule aliyeuawa anapigana katika njia ya Allaah na yule aliyeua Atasamehewa na ('Azza wa Jalla). Kisha atapigana yule aliyeua katika njia ya Allaah na kufa shahidi". Mwandishi: Imaam ´Ubaydullaah bin Muhammad bin Battah al-´Ukbariy (d. 387) Chanzo: al-Ibaanah al-Kubraa (3/3/91)

Shikamaneni na elimu yenu – Allaah Awarehemu – ya kwamba ni katika sifa ya watu wa haki kumthibitishia na kukubali mapokezi sahihi bila ya kupinga kwa kulinganisha na maoni na matamanio. Imani ni kuthibitisha na muumini anathibitisha. Allaah (‘Azza wa Jalla) kasema:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا
”Basi Naapa kwa Mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu (mwamuzi) katika yale wanayotofautiana baina yao, kisha wasione katika nyoyo zao uzito katika uliyohukumu na wajisalimishe kwa unyenyekevu.”

Katika sifa ya waumini ni kwamba wanamsifia Allaah kama jinsi Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) Alivyojisifia Yeye Mwenyewe na kama jinsi Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomsifia kupitia yale ambayo yamesimuliwa na wanachuoni na kupokelewa na wapokezi waaminifu. Wanatoa dalili kwa yale waliyopokea kwa yale mazuri na yasiokuwa mazuri, ya mila na mapokezi. Hakusemwi kwa yale ya sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) “Vipi?” au “Kwa nini?”. Wanafuata na hawazushi. Wanajisalimisha na hawana kipingamizi. Wametosheka na hawana shaka.

Katika mambo ya sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kupitia wapokezi waaminifu na ambayo waumini ni lazima wayaamini na ni Haramu kwenda kinyume chake, ni [kuamini kwamba] Allaah (Ta´ala) Anacheka. Linakanushwa na analikanusha tu mtu wa Bid´ah ambaye hali yake imehukumiwa na wanachuoni. Huyu ni katika yale mapote yaliyopotea na maoni kutelekezwa na maoni yaliyokataliwa – Allaah Atulinde sisi na nyinyi na Bid´ah zote na upotevu.

67 – Abu Raziyn al-‘Uqayliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Mola Wetu Anacheka kwa maelezo ya waja Wake wakati kubadilika Kwake kwa kweli kuko karibu.” Nikasema: “Je Mola Wetu Anacheka ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ndiyo.” Kisha akasema: “Basi Mola Ambaye Anacheka hatotunyima kamwe kitu kizuri.”

68 – Abu Muusa al-Ash’ariy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Mola Wetu Atajidhihirisha kwetu siku ya Qiyaamah Akicheka.”

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Allaah (Ta´ala) Anawacheka watu wawili. Mmoja wao anamuua mwenzake na wote wawili wanaingia Peponi. Yule aliyeuawa anapigana katika njia ya Allaah na yule aliyeua Atasamehewa na (‘Azza wa Jalla). Kisha atapigana yule aliyeua katika njia ya Allaah na kufa shahidi”.

Mwandishi: Imaam ´Ubaydullaah bin Muhammad bin Battah al-´Ukbariy (d. 387)
Chanzo: al-Ibaanah al-Kubraa (3/3/91)


  • Kitengo: Uncategorized , Kucheka kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013