Ibn Baaz Kuhusu Kuzunguka Kwa Jua Katika Ardhi

Qur-aan, Sunnah, maafikiano (Ijmaa´) na uhakika unatolea dalili kwamba jua linazunguka katika mhimili wake kama jinsi Allaah Alivyolazimisha kuwa hivyo na kwamba ardhi imesimama. Allaah (Ta´ala) Amesema: أَوَلَمْ يَرَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ “Je, hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, Tukaziambua (Tukazipambanua mbali mbali); na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai. Je, basi hawaamini? Na Tukajaalia katika ardhi milima (ili) isiwayumbiye yumbiye, na Tukajaalia humo njia pana baina yake wapite ili wapate kuongoza njia. Na Tukajaalia mbingu kuwa ni sakafu ilohifadhiwa. Lakini wao wanazikengeuka Aayah zake. Naye Ndiye Ambaye Ameumba usiku na mchana, na jua na mwezi; vyote vinaelea angani.” (21:30-33) Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُم بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا ”Allaah Ambaye Ameinua mbingu bila ya nguzo mnaziona; kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). Na Akavitiisha jua na mwezi, vyote vinakwenda (na kuendelea kuzunguka) kwa muda maalumu uliopangwa. Anadabiri amri, Anazifasili Aayah ili mpate kuwa na yakini (kuhusu) kukutana na Mola wenu. Na Yeye Ndiye Yule Aliyetandaza ardhi na Akajaalia humo milima na mito.” (13:02-03) Allaah (Ta´ala) Amesema: وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ “Na Ameweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbeyumbe kwenu, na (Akaweka) mito na njia ili mpate kujiongoza.” (16:15) Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ “Anauingiza usiku katika mchana, na Anauingiza mchana katika usiku, na Anaitisha jua na mwezi; kila kimoja (vyote) kinakwenda mpaka muda maalumu uliopangwa. Huyo (basi) Ndiye Allaah Mola wenu.” (35:13) Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ “Na jua linatembea kwa muda wake (uliopangwa) wa kustakiri (kituoni) kwake. Hayo ni makadirio ya Al-‘Aziyzil-‘Aliym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mjuzi wa yote daima). Na mwezi (pia) Tumeukadiria vituo (unatembea) mpaka unarudi (kudhihirika mwembamba) kama kwamba ni shina la mtende lilopinda la zamani. Halipasi jua kuudiriki mwezi, na wala usiku (haupaswi) kuutangulia mchana; na kila kimoja (vyote) katika falaki vinaelea.” (36:38-40) Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ “Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki, Anaufunika usiku juu ya mchana, na Anafunika mchana juu ya usiku, na Anatiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliopangwa. Tanabahi! Yeye Ndiye Al-‘Aziyzul-Ghaffaar (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwingi wa kughufuria).” (39:05) Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema: وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِّنْهُ “Na (ungelikuweko) ungeliona jua linapochomoza linaelemea pango lao kwa upande wa kulia; na linapokuchwa linawakwepa upande wa kushoto, nao wamo katika uwazi wa humo.” (18:17) Aayah hizi tukufu zinaonesha dalili kwamba jua ni lenye kuzunguka na halikusimama na kwamba ardhi ni yenye kusimama. Allaah Ameiweka milima ili isiyumbeyumbe chini ya watu na Akawakunjulia nayo ili waweze kukaa imara juu yake na kunufaika kwa yale ambayo Allaah Amewaumbia. Wafasiri wa Qur-aan kama Ibn Jariyr, al-Baghawiy, Ibn Kathiyr, al-Qurtwubiy na wengine wamethibitisha kwamba jua ni lenye kuzunguka na kwamba linaenda juu na chini wakati ardhi ni yenye kusimama na iko imara. Kadhalika wanasema hivyo wanachuoni wengine ambao maoni yao ni yenye kujulikana katika madai hii. Wanazungumza kwa mujibu wa Qur-aan na kwamba jua na mwezi vinaenda kwenye mzunguko wake kama jinsi Allaah Alivyoamua kwa hayo wakati ardhi imesimama na iko imara. Yule mwenye kudai mengine na kusema kwamba jua limesimama na kuwa ardhi inazunguka amemkadhibisha Allaah na Kitabu chake kitukufu. Mwenye kusema hivo amekufuru na ni mpotevu kwa kuwa amemkadhibisha Allaah na Qur-aan na kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Ahaadiyth Swahiyh kwamba jua ni lenye kuzunguka na kwamba linapoenda chini, linaenda katika Sujuud mbele ya Mola Wake (´Azza wa Jalla) chini ya Kursiy. Kuhusu mwenye kusema kwamba ardhi na jua vyote viwili ni vyenye kuzunguka, kauli hii ni sahali kuliko ile ya kwanza. Hata hivyo ni ya makosa na inaenda kinyume na Aayah zilizotangulia, dalili kamili na uhakika (kauli hii) inapelekea katika kusema kwamba jua ni lenye kusimama. Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz Chanzo: al-Adillah an-Naqliyyah wal-Hissiyyah ´alaa Jarayaan-ish-Shams wa Sukuun-il-Ardhw, uk. 21-25

Qur-aan, Sunnah, maafikiano (Ijmaa´) na uhakika unatolea dalili kwamba jua linazunguka katika mhimili wake kama jinsi Allaah Alivyolazimisha kuwa hivyo na kwamba ardhi imesimama. Allaah (Ta´ala) Amesema:

أَوَلَمْ يَرَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
“Je, hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, Tukaziambua (Tukazipambanua mbali mbali); na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai. Je, basi hawaamini? Na Tukajaalia katika ardhi milima (ili) isiwayumbiye yumbiye, na Tukajaalia humo njia pana baina yake wapite ili wapate kuongoza njia. Na Tukajaalia mbingu kuwa ni sakafu ilohifadhiwa. Lakini wao wanazikengeuka Aayah zake. Naye Ndiye Ambaye Ameumba usiku na mchana, na jua na mwezi; vyote vinaelea angani.” (21:30-33)

Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُم بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا
”Allaah Ambaye Ameinua mbingu bila ya nguzo mnaziona; kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). Na Akavitiisha jua na mwezi, vyote vinakwenda (na kuendelea kuzunguka) kwa muda maalumu uliopangwa. Anadabiri amri, Anazifasili Aayah ili mpate kuwa na yakini (kuhusu) kukutana na Mola wenu. Na Yeye Ndiye Yule Aliyetandaza ardhi na Akajaalia humo milima na mito.” (13:02-03)

Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
“Na Ameweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbeyumbe kwenu, na (Akaweka) mito na njia ili mpate kujiongoza.” (16:15)

Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ
“Anauingiza usiku katika mchana, na Anauingiza mchana katika usiku, na Anaitisha jua na mwezi; kila kimoja (vyote) kinakwenda mpaka muda maalumu uliopangwa. Huyo (basi) Ndiye Allaah Mola wenu.” (35:13)

Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
“Na jua linatembea kwa muda wake (uliopangwa) wa kustakiri (kituoni) kwake. Hayo ni makadirio ya Al-‘Aziyzil-‘Aliym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mjuzi wa yote daima). Na mwezi (pia) Tumeukadiria vituo (unatembea) mpaka unarudi (kudhihirika mwembamba) kama kwamba ni shina la mtende lilopinda la zamani. Halipasi jua kuudiriki mwezi, na wala usiku (haupaswi) kuutangulia mchana; na kila kimoja (vyote) katika falaki vinaelea.” (36:38-40)

Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ
“Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki, Anaufunika usiku juu ya mchana, na Anafunika mchana juu ya usiku, na Anatiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliopangwa. Tanabahi! Yeye Ndiye Al-‘Aziyzul-Ghaffaar (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima – Mwingi wa kughufuria).” (39:05)

Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِّنْهُ
“Na (ungelikuweko) ungeliona jua linapochomoza linaelemea pango lao kwa upande wa kulia; na linapokuchwa linawakwepa upande wa kushoto, nao wamo katika uwazi wa humo.” (18:17)

Aayah hizi tukufu zinaonesha dalili kwamba jua ni lenye kuzunguka na halikusimama na kwamba ardhi ni yenye kusimama. Allaah Ameiweka milima ili isiyumbeyumbe chini ya watu na Akawakunjulia nayo ili waweze kukaa imara juu yake na kunufaika kwa yale ambayo Allaah Amewaumbia.

Wafasiri wa Qur-aan kama Ibn Jariyr, al-Baghawiy, Ibn Kathiyr, al-Qurtwubiy na wengine wamethibitisha kwamba jua ni lenye kuzunguka na kwamba linaenda juu na chini wakati ardhi ni yenye kusimama na iko imara. Kadhalika wanasema hivyo wanachuoni wengine ambao maoni yao ni yenye kujulikana katika madai hii. Wanazungumza kwa mujibu wa Qur-aan na kwamba jua na mwezi vinaenda kwenye mzunguko wake kama jinsi Allaah Alivyoamua kwa hayo wakati ardhi imesimama na iko imara.

Yule mwenye kudai mengine na kusema kwamba jua limesimama na kuwa ardhi inazunguka amemkadhibisha Allaah na Kitabu chake kitukufu. Mwenye kusema hivo amekufuru na ni mpotevu kwa kuwa amemkadhibisha Allaah na Qur-aan na kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Ahaadiyth Swahiyh kwamba jua ni lenye kuzunguka na kwamba linapoenda chini, linaenda katika Sujuud mbele ya Mola Wake (´Azza wa Jalla) chini ya Kursiy.

Kuhusu mwenye kusema kwamba ardhi na jua vyote viwili ni vyenye kuzunguka, kauli hii ni sahali kuliko ile ya kwanza. Hata hivyo ni ya makosa na inaenda kinyume na Aayah zilizotangulia, dalili kamili na uhakika (kauli hii) inapelekea katika kusema kwamba jua ni lenye kusimama.

Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: al-Adillah an-Naqliyyah wal-Hissiyyah ´alaa Jarayaan-ish-Shams wa Sukuun-il-Ardhw, uk. 21-25


  • Kitengo: Uncategorized , Tawhiyd na ´Aqiydah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 30th, March 2014