´Ibaadah Ya Kuyaabudu Makaburi

Wengi katika watu wanawategemea maiti waliomo kwenye makaburi. Wanawaomba badala ya Allaah, wanawataka msaada, wanatufu kwenye makaburi yao, wanaomba uokovu, msaada na kuwanusuru. Hii ni Shirki kubwa. Hii ndio dini ya washirikina. Ni lazima kwa wanachuoni wawafunze watu na wawafunze. Hii ndio dhambi kubwa na uovu mkubwa. Si mwingine ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla). Kadhalika kuwaomba majini, maiti, Mitume na kuwaomba msaada. Hii ndio Shirki kubwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala wa Jalla wa ´Alaa) Anasema: "Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa Yeye Pekee." (17:23) "Na hawakuamrishwa (chochote kile) isipokuwa wamwabudu Allaah wakiwa wenye kumtakasia Dini, Hunafaa (wakielemea haki na kujiengua na upotofu)." (98:05) "Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote." (04:36) "Na yeyote yule anayeomba (Du’aa au kuabudu) pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri." (23:117) "Na kwamba Misikiti ni (kwa ajili) ya Allaah, basi msiombe (msimuabudu) yeyote pamoja na Allaah." (72:18) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: "Du´aa ndio ´ibaadah."

Wengi katika watu wanawategemea maiti waliomo kwenye makaburi. Wanawaomba badala ya Allaah, wanawataka msaada, wanatufu kwenye makaburi yao, wanaomba uokovu, msaada na kuwanusuru. Hii ni Shirki kubwa. Hii ndio dini ya washirikina.

Ni lazima kwa wanachuoni wawafunze watu na wawafunze. Hii ndio dhambi kubwa na uovu mkubwa. Si mwingine ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla). Kadhalika kuwaomba majini, maiti, Mitume na kuwaomba msaada. Hii ndio Shirki kubwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala wa Jalla wa ´Alaa) Anasema:

“Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa Yeye Pekee.” (17:23)

“Na hawakuamrishwa (chochote kile) isipokuwa wamwabudu Allaah wakiwa wenye kumtakasia Dini, Hunafaa (wakielemea haki na kujiengua na upotofu).” (98:05)

“Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (04:36)

“Na yeyote yule anayeomba (Du’aa au kuabudu) pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri.” (23:117)

“Na kwamba Misikiti ni (kwa ajili) ya Allaah, basi msiombe (msimuabudu) yeyote pamoja na Allaah.” (72:18)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Du´aa ndio ´ibaadah.”