´Ibaadah Haithibiti Isipokuwa Kwa Mambo Haya Matatu

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema: "Kinachofuatwa katika kuthibitisha Ahkaam za Allaah ni Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na njia ya waliotangulia." ´Ibaadah haithibiti isipokuwa kwa mambo haya: 1- Kitabu cha Allaah, nayo ni Qur-aan tukufu. 2- Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), au 3- Ijmaa´ ya wanachuoni wa Waislamu na yale waliyomo Salaf wa Ummah huu katika Maswahabah, Taabi´uun na waliokuja baada yao. Allaah (Ta´ala) Amesema: وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ “Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye.” (09:100) Anaendelea kusema (Rahimahu Allaah): “Haijuzu kuthibitisha hukumu ya Kishari´ah bila ya misingi hii mitatu, na Instinbaatw kwa hali yoyote.” Yanayokwenda kinyume na misingi hii mitatu basi ni batili na sio sahihi kwa hali yoyote hata kama jambo hili watalipamba kwa utata, ni batili. Kwa kuwa batili haiwezi kuwa haki kamwe. Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2245 Toleo la: 16-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kinachofuatwa katika kuthibitisha Ahkaam za Allaah ni Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na njia ya waliotangulia.”

´Ibaadah haithibiti isipokuwa kwa mambo haya:

1- Kitabu cha Allaah, nayo ni Qur-aan tukufu.

2- Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), au

3- Ijmaa´ ya wanachuoni wa Waislamu na yale waliyomo Salaf wa Ummah huu katika Maswahabah, Taabi´uun na waliokuja baada yao. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ
“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye.” (09:100)

Anaendelea kusema (Rahimahu Allaah):

“Haijuzu kuthibitisha hukumu ya Kishari´ah bila ya misingi hii mitatu, na Instinbaatw kwa hali yoyote.”

Yanayokwenda kinyume na misingi hii mitatu basi ni batili na sio sahihi kwa hali yoyote hata kama jambo hili watalipamba kwa utata, ni batili. Kwa kuwa batili haiwezi kuwa haki kamwe.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2245
Toleo la: 16-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 16th, May 2014