Huyu Ndiye Shaytwaan Bubu

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “Wala usiwe ni mwenye kusimama juu ya Qur-aan”, miongoni mwa Jahmiyyah kuko ambao wanaweka wazi kabisa ya kwamba Qur-aan imeumbwa. Hawa ni wale vigogo wa Jahmiyyah. Miongoni mwao pia kuko ambao wanasema ya kwamba mimi sisemi kuwa imeumbwa wala haikuumbwa. Mimi ninasimama. Huyu ni Shaytwaan alie bubu. Kwa kuwa ukisimama watu watafikiria kuwa Qur-aan imeumbwa. Ni lazima kubainisha. Wakisema kuwa imeumbwa, wewe hutakiwi kusimama. Kwa kuwa ukifanya hivyo maana yake ni kwamba unawasapoti lakini hutaki kuonesha hilo wazi. Haijuzu kusimama katika hili. Haya ni madhehebu ya al-Waqfiyyah ambao wanasema sisi tunasimama na hatusemi kuwa imeumbwa au haikuumbwa. Hili maana yake ni kuficha kuibainisha haki na huku ina maana kusapoti kauli ya Jahmiyyah kwamba ni sahihi kwa vile hakuwakatalia na kuweka wazi na hakufichua. Yule mwenye kuwa na mashaka ya kwamba Qur-aan imeumbwa au haikuumbwa na akanyamaza, huyu ni Jahmiy na anajificha tu. Kwa kuwa lau ingelikuwa sio Jahmiy angelikuwa muwazi na kusema haikuumbwa. Lakini anataka kujificha kwa kusimama. Sivyo tu bali huyu kwa hakika ni mbaya zaidi kuliko Jahmiyyah, kwa kuwa wao wameweka wazi na yamejulikana madhehebu yao. Ama huyu anataka kuwadanganya watu ya kwamba ni mnyenyekevu sana na wala hawezi kuzungumzia jambo hili. Haitoshi kusimama, bali ni lazima kuwa muwazi kuibatilisha kauli hii. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 74-75

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “Wala usiwe ni mwenye kusimama juu ya Qur-aan”, miongoni mwa Jahmiyyah kuko ambao wanaweka wazi kabisa ya kwamba Qur-aan imeumbwa. Hawa ni wale vigogo wa Jahmiyyah.

Miongoni mwao pia kuko ambao wanasema ya kwamba mimi sisemi kuwa imeumbwa wala haikuumbwa. Mimi ninasimama. Huyu ni Shaytwaan alie bubu. Kwa kuwa ukisimama watu watafikiria kuwa Qur-aan imeumbwa. Ni lazima kubainisha. Wakisema kuwa imeumbwa, wewe hutakiwi kusimama. Kwa kuwa ukifanya hivyo maana yake ni kwamba unawasapoti lakini hutaki kuonesha hilo wazi. Haijuzu kusimama katika hili. Haya ni madhehebu ya al-Waqfiyyah ambao wanasema sisi tunasimama na hatusemi kuwa imeumbwa au haikuumbwa. Hili maana yake ni kuficha kuibainisha haki na huku ina maana kusapoti kauli ya Jahmiyyah kwamba ni sahihi kwa vile hakuwakatalia na kuweka wazi na hakufichua.

Yule mwenye kuwa na mashaka ya kwamba Qur-aan imeumbwa au haikuumbwa na akanyamaza, huyu ni Jahmiy na anajificha tu. Kwa kuwa lau ingelikuwa sio Jahmiy angelikuwa muwazi na kusema haikuumbwa. Lakini anataka kujificha kwa kusimama. Sivyo tu bali huyu kwa hakika ni mbaya zaidi kuliko Jahmiyyah, kwa kuwa wao wameweka wazi na yamejulikana madhehebu yao. Ama huyu anataka kuwadanganya watu ya kwamba ni mnyenyekevu sana na wala hawezi kuzungumzia jambo hili. Haitoshi kusimama, bali ni lazima kuwa muwazi kuibatilisha kauli hii.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 74-75


  • Kitengo: Uncategorized , Jahmiyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 14th, February 2014