Hukumu Ya Kuwapongeza Makafiri Kwa Sherehe Zao

Ikiwa makafiri hawa wataoa, watapata mtoto, kupata mtu ambaye alikuwa amepotea, kusalimika na khatari yoyote au mfano wa hayo, kumepokelewa maoni mengi kutoka kwa Ahmad kama inaruhusiwa kuwapongeza kwa hilo au hapana. Mara anaruhusu hilo na mara nyingine anakataza hilo. Katika mambo yanayohusiana na suala hili ni sawa kabisa na kuwapa mkono wa pole (taazia) [kwa kafiri] na kumtembelea mgonjwa [kafiri]. Hakuna tofauti kati yayo. Hivyo mtu anatakiwa atahadhari asianguke katika yale ambayo watu wajinga huanguka wakati wanapotamka kwa njia ambayo inaashiria kwamba wameridhika na Dini yao. Mfano wa hili ni kama mtu kusema: "Allaah Akufurahishe kwa Dini yako", "Allaah Akuimarishe" au "Allaah Awe juu yako." Kinachoruhusiwa ni mtu kusema tu badala yake: "Allaah Akuimarishe kwa Uislamu", "Allaah Awe juu yako kwa Uislamu" na mfano wa hayo. Hata hivyo, wamekubaliana wanachuoni ya kwamba ni haramu kuwapongeza makafiri kwa sikukuu zao kama sherehe na kufunga. Mfano wa hilo ni kusema: "Uwe na Sikukuu njema!.” Ikiwa kauli hii si Kufuru, basi angalau ni dhambi kubwa. Dhambi hii ni kubwa kama ambavyo mtu anavyowapongeza wanapoanguka (kufanya sujudu) kwa nyuso zao kwenye misalaba. Ukweli ni kwamba Allaah Anaona hili kuwa ni baya zaidi kuliko mtu kuwapongeza kwa kunywa pombe, na kuua mtu, zinaa na mfano wa hayo. Watu wengi wasiojua thamani ya Dini wanaanguka katika kosa hili. Hawajui jinsi ya dhambi hii inavyotisha. Yule anayempongeza mtu kwa dhambi, Bid´ah au kufuru, amejisababishia mwenyewe hasira na ghadhabu za Allaah." Mwandishi: Imaam Ibn al-Qayyim al-Jawziy Chanzo: Ahkaam Ahl-Idh-Dhimmah (1/441)

Ikiwa makafiri hawa wataoa, watapata mtoto, kupata mtu ambaye alikuwa amepotea, kusalimika na khatari yoyote au mfano wa hayo, kumepokelewa maoni mengi kutoka kwa Ahmad kama inaruhusiwa kuwapongeza kwa hilo au hapana. Mara anaruhusu hilo na mara nyingine anakataza hilo. Katika mambo yanayohusiana na suala hili ni sawa kabisa na kuwapa mkono wa pole (taazia) [kwa kafiri] na kumtembelea mgonjwa [kafiri]. Hakuna tofauti kati yayo. Hivyo mtu anatakiwa atahadhari asianguke katika yale ambayo watu wajinga huanguka wakati wanapotamka kwa njia ambayo inaashiria kwamba wameridhika na Dini yao. Mfano wa hili ni kama mtu kusema:
“Allaah Akufurahishe kwa Dini yako”, “Allaah Akuimarishe” au “Allaah Awe juu yako.”

Kinachoruhusiwa ni mtu kusema tu badala yake:
“Allaah Akuimarishe kwa Uislamu”, “Allaah Awe juu yako kwa Uislamu” na mfano wa hayo.

Hata hivyo, wamekubaliana wanachuoni ya kwamba ni haramu kuwapongeza makafiri kwa sikukuu zao kama sherehe na kufunga. Mfano wa hilo ni kusema:
“Uwe na Sikukuu njema!.”

Ikiwa kauli hii si Kufuru, basi angalau ni dhambi kubwa. Dhambi hii ni kubwa kama ambavyo mtu anavyowapongeza wanapoanguka (kufanya sujudu) kwa nyuso zao kwenye misalaba. Ukweli ni kwamba Allaah Anaona hili kuwa ni baya zaidi kuliko mtu kuwapongeza kwa kunywa pombe, na kuua mtu, zinaa na mfano wa hayo.

Watu wengi wasiojua thamani ya Dini wanaanguka katika kosa hili. Hawajui jinsi ya dhambi hii inavyotisha. Yule anayempongeza mtu kwa dhambi, Bid´ah au kufuru, amejisababishia mwenyewe hasira na ghadhabu za Allaah.”

Mwandishi: Imaam Ibn al-Qayyim al-Jawziy
Chanzo: Ahkaam Ahl-Idh-Dhimmah (1/441)


  • Kitengo: Uncategorized , Krismasi
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013