Hukumu Ya Kuwa Na Wake Wawili Kwenye Nyumba Moja

Mwanaume hana haki ya kuwa na wake wawili kwenye nyumba moja bila ridhaa yao. Hili ni sawa nyumba ikiwa ndogo au kubwa. Kwa sababu ni kwamba linaleta uadui na chuki kati ya wake wawili. Ikiwa watakubaliana kuwa ndani ya nyumba moja, litapelekea katika ugomvi na kupigana. Aidha, inaweza kutokea kwamba mke mmoja akasikia jinsi huyu mwingine anavyostarehe wakati wa maingiliano na yeye, au hata akaona hilo. Hata hivyo, ikiwa wake watakubaliana hilo, inazingatiwa kuwa inaruhusu kwa sababu ni haki yao na kwa ajili hiyo wana haki ya kukubaliana juu ya hilo. Hali kadhalika (inaruhusu) ikiwa wote wawili watakubaliana kulala na mume (wao) kati yao ndani ya shuka hiyo hiyo moja. Lakini kama watakubaliana mume kumwingilia mke mmoja wakati huku huyu mwingine anatazama, hili huzingatiwa kuwa haijuzu, kwa sababu ndani yake kuna ujinga na tabia mbaya.

Mwanaume hana haki ya kuwa na wake wawili kwenye nyumba moja bila ridhaa yao. Hili ni sawa nyumba ikiwa ndogo au kubwa. Kwa sababu ni kwamba linaleta uadui na chuki kati ya wake wawili. Ikiwa watakubaliana kuwa ndani ya nyumba moja, litapelekea katika ugomvi na kupigana. Aidha, inaweza kutokea kwamba mke mmoja akasikia jinsi huyu mwingine anavyostarehe wakati wa maingiliano na yeye, au hata akaona hilo.

Hata hivyo, ikiwa wake watakubaliana hilo, inazingatiwa kuwa inaruhusu kwa sababu ni haki yao na kwa ajili hiyo wana haki ya kukubaliana juu ya hilo.

Hali kadhalika (inaruhusu) ikiwa wote wawili watakubaliana kulala na mume (wao) kati yao ndani ya shuka hiyo hiyo moja.

Lakini kama watakubaliana mume kumwingilia mke mmoja wakati huku huyu mwingine anatazama, hili huzingatiwa kuwa haijuzu, kwa sababu ndani yake kuna ujinga na tabia mbaya.


  • Author: Shaykh-ul-Islaam Ibn Qudaamah al-Maqdisiy. al-Mughniy (10/234) Daar ´Aalam-il-Kutub
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 16th, December 2013