Hukumu Ya Kuvaa Pete Ya Ndoa

Ad-Dublah ni ibara ya pete; ni pete ambayo mume humpa mke wake. Katika watu kuna wanaomvalisha mwanamke anapotaka kuoa au anapooa. Ada hii sio maarufu kwetu. Shaykh Albaaniy (Allaah Amuwafikishe) kasema kuwa asli yake imechukuliwa kutoka kwa Manaswara. Na kwamba wachungaji wanawavalisha wanandoa kanisani na mwanamke huvalishwa pete kwenye kidole chake cha nne au kwenye kidole cha katikati, mimi sijui inakuweje lakini kasema kuwa imechukuliwa kutoka kwa Manaswara. Hivyo kuachana nayo bila shaka itakuwa aula zaidi, ili tusije kujifananisha na wasiokuwa sisi (Waislamu). Mbali na hilo ni kwamba baadhi ya watu huitakidi (huamini) kitu kwa jambo hili. Mume haundika jina lake kwenye pete ambayo anataka kumpa mkewe, na yeye mke huandika jina lake kwenye pete ambayo anataka kumpa mumewe. Na wanaamini maadamu pete bado iko mkononi mwa mume na ina jina la mkewe, na pete ya mke ina jina la mumewe kwamba hawatofarakana. ´Aqiydah (kuamini huku) ni aina ya Shirki. Isitoshe ni katika at-Tiwalah, ambacho ni kitu kinachomuambatanisha mke kwa mumewe, na mume kwa mke wake . Kuwa na ´Aqiydah (kuamini namna hii) ni Haramu. Hapa kuna masuala mawili kuhusiana na pete. Jambo la kwanza ni kwamba imechukuliwa kutoka kwa Manaswara. Jambo la pili ni kwamba akiamini mume kwamba (pete) ni sababu ya kuambatana yeye na mke wake itakuwa ni aina ya Shirki. Hivyo tunaona kuiacha ni bora.

Ad-Dublah ni ibara ya pete; ni pete ambayo mume humpa mke wake. Katika watu kuna wanaomvalisha mwanamke anapotaka kuoa au anapooa. Ada hii sio maarufu kwetu.

Shaykh Albaaniy (Allaah Amuwafikishe) kasema kuwa asli yake imechukuliwa kutoka kwa Manaswara. Na kwamba wachungaji wanawavalisha wanandoa kanisani na mwanamke huvalishwa pete kwenye kidole chake cha nne au kwenye kidole cha katikati, mimi sijui inakuweje lakini kasema kuwa imechukuliwa kutoka kwa Manaswara. Hivyo kuachana nayo bila shaka itakuwa aula zaidi, ili tusije kujifananisha na wasiokuwa sisi (Waislamu).
Mbali na hilo ni kwamba baadhi ya watu huitakidi (huamini) kitu kwa jambo hili. Mume haundika jina lake kwenye pete ambayo anataka kumpa mkewe, na yeye mke huandika jina lake kwenye pete ambayo anataka kumpa mumewe. Na wanaamini maadamu pete bado iko mkononi mwa mume na ina jina la mkewe, na pete ya mke ina jina la mumewe kwamba hawatofarakana. ´Aqiydah (kuamini huku) ni aina ya Shirki. Isitoshe ni katika at-Tiwalah, ambacho ni kitu kinachomuambatanisha mke kwa mumewe, na mume kwa mke wake . Kuwa na ´Aqiydah (kuamini namna hii) ni Haramu.

Hapa kuna masuala mawili kuhusiana na pete. Jambo la kwanza ni kwamba imechukuliwa kutoka kwa Manaswara. Jambo la pili ni kwamba akiamini mume kwamba (pete) ni sababu ya kuambatana yeye na mke wake itakuwa ni aina ya Shirki. Hivyo tunaona kuiacha ni bora.