Hii Ndio Sababu Ibn Baaz Hakujadiliana Na al-Khaliyliy

Hatimaye as-Sayyaabiy akamalizia maneno yake ya kuchosha kwa kumtaja Shaykh wake na Muftiy wa Oman al-Khaliyliy mkutano wake na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na masuala waliyoongelea na kusema: "Shaykh Ibn Baaz akaanza kusema vibaya na kulaani, kuonelea kuwa wengine ndio wapotevu na makafiri, kuwa na hasira na kughadhibika. Wakati al-Khaliyliy alimpa changamoto kuomba laana ya Allaah imshukiye yule ambaye yuko katika makosa, akakimbia." Vovyote utakavyomueleza kwa ubaya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, watu wanamjua, tabia yake tukufu na elimu yake iliobobea. Wanajua kuwa yeye na kwa nguvu za Allaah Ameweza kumchoma Shaykh wako na wengine kwa haki. Hili na khaswa masuala haya ambayo hata wanafunzi wetu wanayajua. Shaykh Ibn Baaz ameeleza kwa nini hakutaka kujadiliana. Alikuwa anachukia mijadala ya hadharani ambayo inaweza kuwadhuru baadhi ya watu na kuwatia mashaka. Hata hivyo - Alhamduli Allaah - yuko katika mazingira ambayo hawa wapotevu walopinda hawana. Hakutaka kuanzisha kwa watu shari ambayo wamesalimika nayo. Ni hakima bora. Ikiwa as-Sayyaabiy na Shaykh wake al-Khaliyliy wanaweza kuradi yale ambayo wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wameandika kuhusiana na masuala haya, nayo ni kuhusu waumini kumuona Allaah siku ya Qiyaamah, kwamba waumini wafanya madhambi hawatodumishwa Motoni milele, kwamba Qur-aan haikuumbwa na masuala mengine ambayo Ibaadhiyyah wamekwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wafanye hivyo sasa. Lakini vipi wataweza kufanya hivyo wakati wanachuoni wako katika ulinzi wao?

Hatimaye as-Sayyaabiy akamalizia maneno yake ya kuchosha kwa kumtaja Shaykh wake na Muftiy wa Oman al-Khaliyliy mkutano wake na Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na masuala waliyoongelea na kusema:

“Shaykh Ibn Baaz akaanza kusema vibaya na kulaani, kuonelea kuwa wengine ndio wapotevu na makafiri, kuwa na hasira na kughadhibika. Wakati al-Khaliyliy alimpa changamoto kuomba laana ya Allaah imshukiye yule ambaye yuko katika makosa, akakimbia.”

Vovyote utakavyomueleza kwa ubaya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, watu wanamjua, tabia yake tukufu na elimu yake iliobobea. Wanajua kuwa yeye na kwa nguvu za Allaah Ameweza kumchoma Shaykh wako na wengine kwa haki. Hili na khaswa masuala haya ambayo hata wanafunzi wetu wanayajua.

Shaykh Ibn Baaz ameeleza kwa nini hakutaka kujadiliana. Alikuwa anachukia mijadala ya hadharani ambayo inaweza kuwadhuru baadhi ya watu na kuwatia mashaka. Hata hivyo – Alhamduli Allaah – yuko katika mazingira ambayo hawa wapotevu walopinda hawana. Hakutaka kuanzisha kwa watu shari ambayo wamesalimika nayo. Ni hakima bora.

Ikiwa as-Sayyaabiy na Shaykh wake al-Khaliyliy wanaweza kuradi yale ambayo wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wameandika kuhusiana na masuala haya, nayo ni kuhusu waumini kumuona Allaah siku ya Qiyaamah, kwamba waumini wafanya madhambi hawatodumishwa Motoni milele, kwamba Qur-aan haikuumbwa na masuala mengine ambayo Ibaadhiyyah wamekwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, wafanye hivyo sasa. Lakini vipi wataweza kufanya hivyo wakati wanachuoni wako katika ulinzi wao?


  • Author: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan. al-Bayaan li Akhtwaa' Ba´dh-il-Kuttaab, uk. 238-239
  • Kitengo: Uncategorized , al-Khaliyliy, Ahmad bin Hamad
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 14th, January 2014