Hawa Ndio Wenye Kuwasengenya Waislamu

Lau utawapeleleza watu hawa ambao kazi yao ni kusengenya na kueneza uvumi, utaona kuwa wao ndio waovu zaidi na tunaomba kinga kwa Allaah. Wanawajeruhi Waislamu wazuri ilihali wao ndio waovu zaidi. Wanawasemea uongo Waislamu na wanazisahau aibu zao na maovu walionayo. Lililo la wajibu ni kutahadhari nao, kupeana nasaha na Waislamu wabaki kuwa na udugu. Wewe kama jinsi hupendi yeyote akuzungumzie kwa ubaya na kukusengenya, vipi basi utaridhia hili kwa wengine? Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendee ndugu yake yale anayojipendea juu ya nafsi yake.” Vipi nafsi yako unaipendea kheri na unaridhia juu ya ndugu yako shari? Hili ni jambo la khatari sana na maradhi mabaya ikiwa hayakutibiwa na watu hawa wakachukuliwa hatua.

Lau utawapeleleza watu hawa ambao kazi yao ni kusengenya na kueneza uvumi, utaona kuwa wao ndio waovu zaidi na tunaomba kinga kwa Allaah. Wanawajeruhi Waislamu wazuri ilihali wao ndio waovu zaidi. Wanawasemea uongo Waislamu na wanazisahau aibu zao na maovu walionayo.

Lililo la wajibu ni kutahadhari nao, kupeana nasaha na Waislamu wabaki kuwa na udugu.

Wewe kama jinsi hupendi yeyote akuzungumzie kwa ubaya na kukusengenya, vipi basi utaridhia hili kwa wengine? Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendee ndugu yake yale anayojipendea juu ya nafsi yake.”

Vipi nafsi yako unaipendea kheri na unaridhia juu ya ndugu yako shari? Hili ni jambo la khatari sana na maradhi mabaya ikiwa hayakutibiwa na watu hawa wakachukuliwa hatua.