Hawa Hapa Wanaume Wetu – Wako Wapi Wanaume Wenu? (1)

1) Hammaad bin Zayd kasema: "Nilimsikia Ayyuub as-Sikthiyaaniy akisema kuwa Mu'tazilah wamesema: "Mtazamo wao umezunguka kwa kusema kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu.'" 2) al-Awzaa'iy kasema: "Tuliishi wakati wa Taabi'uun walikuwa wengi kabisa na tulikuwa tukisema: "Allaah ('Azza wa Jalla) Yuko juu ya ´Arshi Yake na tunaamini Sifa zimezotajwa katika Sunnah.”" 3) Imaam Ibn Qudaamah kasema: "Nilipata khabari kwamba Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) kasema: "Yule ambaye anakanusha ya kwamba Allaah Yuko juu ya mbingu amekufuru."" 4) Maalik kasema: "Allaah Yuko juu ya mbingu, na elimu Yake iko kila mahali." Kasema pia: "Kuwa kwake juu kunajulikana na namna yake haijulikani. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo.” 5) Hammaad bin Zayd kasema kuhusu Jahmiyyah: "Wanachotaka kusema ni kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu.” 6) ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq kasema: "Nilimuuliza Ibn-ul-Mubaarak: “Vipi tutamjua Mola Wetu?" Akasema:" [Ya kwamba Yeye Yuko] juu ya mbingu saba juu ya ´Arshi Yake. Hatusemi kama wanavosema Jahmiyyah: "Yuko hapa duniani.”" 7) 'Abdur-Rahmaan bin Mahdiy kasema: "Jahmiyyah wanataka kukataa kwamba Allaah alizungumza na Muusa na kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Naona wanatakiwa kutubia. Aidha watubie la sivyo wanyongwe". 8) Imaam ash-Shaafi'iy kasema: "Sunnah tunayofuata sisi na ambayo nimeona Ahl-ul-Hadiyth wanaifuata kama Sufyaan, Maalik na wengine ni kuthibitisha hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah... " ... mpaka aliposema: " ... na kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake. Anawakurubia viumbe Vyake vile Apendavyo, na kushuka kwenye mbingu ya chini vile Apendavyo." 9) 'Aasim bin 'Aliy – mwalimu wa al-Bukhaariy - kasema: "Nilijadiliana na Jahmiy na kukuta kuwa haamini ya kwamba kuna mola juu ya mbingu." Yahyaa bin Ma'iyn kasema: "´Aasim alikuwa bingwa wa Waislamu." 10) al-'Abbaas ad-Dawriy kasema: "Nilimsikia Abu 'Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema baada ya kutaja Suurah inayozungumzia kuhusu kuonekana kwa Allaah, Kursiy, Kucheka kwa Mola Wetu na wapi Alipokuwa Mola Wetu [kabla ya uumbaji]: "Hadiyth hizi ni Swahiyh. Wanachuoni katika Hadiyth na Fiqh wamezielezana wao kwa wao. Sina shaka yoyote kwamba ni za kweli. Lakini ikiwa tutaulizwa, "Vipi Ameweka Miguu Yake [kwenye Kursiy]? Vipi Anacheka" "tunasema ya kwamba hatufafanui wala hatujasikia mtu yeyote anafafanua.”” Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (d. 744) Chanzo: al-Istiwaa´ alaal-´Arsh, uk. 50-52

1) Hammaad bin Zayd kasema:
“Nilimsikia Ayyuub as-Sikthiyaaniy akisema kuwa Mu’tazilah wamesema: “Mtazamo wao umezunguka kwa kusema kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu.'”

2) al-Awzaa’iy kasema:
“Tuliishi wakati wa Taabi’uun walikuwa wengi kabisa na tulikuwa tukisema: “Allaah (‘Azza wa Jalla) Yuko juu ya ´Arshi Yake na tunaamini Sifa zimezotajwa katika Sunnah.””

3) Imaam Ibn Qudaamah kasema:
“Nilipata khabari kwamba Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) kasema: “Yule ambaye anakanusha ya kwamba Allaah Yuko juu ya mbingu amekufuru.””

4) Maalik kasema:
“Allaah Yuko juu ya mbingu, na elimu Yake iko kila mahali.”
Kasema pia:
“Kuwa kwake juu kunajulikana na namna yake haijulikani. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo.”

5) Hammaad bin Zayd kasema kuhusu Jahmiyyah:
“Wanachotaka kusema ni kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu.”

6) ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq kasema:
“Nilimuuliza Ibn-ul-Mubaarak: “Vipi tutamjua Mola Wetu?” Akasema:” [Ya kwamba Yeye Yuko] juu ya mbingu saba juu ya ´Arshi Yake. Hatusemi kama wanavosema Jahmiyyah: “Yuko hapa duniani.””

7) ‘Abdur-Rahmaan bin Mahdiy kasema:
“Jahmiyyah wanataka kukataa kwamba Allaah alizungumza na Muusa na kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Naona wanatakiwa kutubia. Aidha watubie la sivyo wanyongwe”.

8) Imaam ash-Shaafi’iy kasema:
“Sunnah tunayofuata sisi na ambayo nimeona Ahl-ul-Hadiyth wanaifuata kama Sufyaan, Maalik na wengine ni kuthibitisha hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah… ” … mpaka aliposema: ” … na kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake. Anawakurubia viumbe Vyake vile Apendavyo, na kushuka kwenye mbingu ya chini vile Apendavyo.”

9) ‘Aasim bin ‘Aliy – mwalimu wa al-Bukhaariy – kasema:
“Nilijadiliana na Jahmiy na kukuta kuwa haamini ya kwamba kuna mola juu ya mbingu.”

Yahyaa bin Ma’iyn kasema:
“´Aasim alikuwa bingwa wa Waislamu.”

10) al-‘Abbaas ad-Dawriy kasema:
“Nilimsikia Abu ‘Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema baada ya kutaja Suurah inayozungumzia kuhusu kuonekana kwa Allaah, Kursiy, Kucheka kwa Mola Wetu na wapi Alipokuwa Mola Wetu [kabla ya uumbaji]: “Hadiyth hizi ni Swahiyh. Wanachuoni katika Hadiyth na Fiqh wamezielezana wao kwa wao. Sina shaka yoyote kwamba ni za kweli. Lakini ikiwa tutaulizwa, “Vipi Ameweka Miguu Yake [kwenye Kursiy]? Vipi Anacheka” “tunasema ya kwamba hatufafanui wala hatujasikia mtu yeyote anafafanua.””

Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (d. 744)
Chanzo: al-Istiwaa´ alaal-´Arsh, uk. 50-52


  • Kitengo: Uncategorized , Kuwa juu kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013