Hakuna Anayemchukia Shaykh Ibn Baaz Isipokuwa Mzushi Tu

Wanachuoni wengi wamesema kuwa yule anayemchukia mtu katika Ahl-us-Sunnah ni mzushi. Kuanzia hapa nitachukulia kama mfano Shaykh wetu, baba, ´Allaamah, Muhaddith na Faqiyh ´Abdul-´Aziyz [bin Baaz]. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hakuna anayemponda isipokuwa mzushi tu na mfano wake katika Mashaykh wa Sunnah. Ninaapa kwa Allaah hakuna anayemponda isipokuwa mzushi: "Ibn Hanbal alikuwa ni jaribio linaloaminika kupitia mapenzi ya kumpenda Ahmad anajulikana ni nani anayeshikamana [na haki] Ukiona mtu anamponda Ahmad jua kuwa atakuja kujichuka" Baadhi [ya washairi wengine] wanasema: ”Ukiona mtu anamponda Ahmad basi mtuhumu Uislamu wake.” Katika alama za Ahl-ul-Bid´ah ni kuwaponda Ahl-us-Sunnah wal-Athar. Imaam na Haafidhw al-Khatwiyb al-Baghdaadiy ameandika mlango katika kitabu chake kikubwa ”Sharaf Aswhaab-il-Hadiyth” ambapo amethibitisha mtu kuwa katika Ahl-us-Sunnah ikiwa anawapenda Ahl-us-Sunanh. Rejeeni huko mtaona maneno haya.

Wanachuoni wengi wamesema kuwa yule anayemchukia mtu katika Ahl-us-Sunnah ni mzushi. Kuanzia hapa nitachukulia kama mfano Shaykh wetu, baba, ´Allaamah, Muhaddith na Faqiyh ´Abdul-´Aziyz [bin Baaz]. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hakuna anayemponda isipokuwa mzushi tu na mfano wake katika Mashaykh wa Sunnah. Ninaapa kwa Allaah hakuna anayemponda isipokuwa mzushi:

“Ibn Hanbal alikuwa ni jaribio linaloaminika
kupitia mapenzi ya kumpenda Ahmad anajulikana ni nani anayeshikamana [na haki]
Ukiona mtu anamponda Ahmad jua kuwa atakuja kujichuka”

Baadhi [ya washairi wengine] wanasema:

”Ukiona mtu anamponda Ahmad basi mtuhumu Uislamu wake.”

Katika alama za Ahl-ul-Bid´ah ni kuwaponda Ahl-us-Sunnah wal-Athar. Imaam na Haafidhw al-Khatwiyb al-Baghdaadiy ameandika mlango katika kitabu chake kikubwa ”Sharaf Aswhaab-il-Hadiyth” ambapo amethibitisha mtu kuwa katika Ahl-us-Sunnah ikiwa anawapenda Ahl-us-Sunanh. Rejeeni huko mtaona maneno haya.