Haiwezekani Ukapendwa Na Watu Wote

Mnatambua kuwa ni wajibu kwetu kujifunza mambo matatu: 1- Elimu. 2- Matendo. 3- Da´wah. 4- Kuwa na subira juu ya maudhi. Wewe unataka kuwaambia watu ni nini halali, haramu, Sunnah, Bid´ah na yasiyojuzu wakati huo huo hutaki asiwepo yeyote atayekuzungumzia? Je, haya yanaingia akilini? Unawaeleza watu ni yepi halali na ni yepi haramu. Ukimuona mtu yuko katika haramu unamuamrisha kumcha Allaah na acha kutenda madhambi na unamnukulia Qur-aan na Sunnah. Unamueleza ni nini Bid´ah na Sunnah. Sasa unataka watu wote wakupende? Je, haya yanaingia akilini? Haya hayakumpata hata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kulipatikana watu waliomuudhi, kumpiga vita na kupambana naye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka akaumia, akavunjwa magego yake na mengi mengine yalimfika. Hili haliwezekani. Yule mwenye kutaka watu wote wamuwie radhi, basi tambua kuwa huyu ni mwenye kupakana mafuta. Haiwezekani ukawaridhisha wote. Kwa nini? Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Mwenye kuwaridhisha watu kwa Khasira za Allaah, atapata Khasira za Allaah na za watu vilevile.” Hata kama watakuwa radhi na wewe hivi sasa watakukasirikia baadaye. Kwa kuwa ni jambo lisilowezekana katika kila msimamo ukawa nao. Ni lazima wakukasirikie. “Na mwenye kumridhisha Allaah kwa khasira za watu, Allaah Atakuwa radhi na yeye na watu watakuwa radhi naye pia.” Kwa kuwa wanajua kuwa ni mkweli. Ni lazima kuwa na subira katika maudhi katika kufikisha elimu hii, kuwabainishia watu haki na kuwahimiza kushikamana nayo, na kuwabainishia watu upotevu na kuwatahadharisha na hilo.

Mnatambua kuwa ni wajibu kwetu kujifunza mambo matatu:

1- Elimu.

2- Matendo.

3- Da´wah.

4- Kuwa na subira juu ya maudhi.

Wewe unataka kuwaambia watu ni nini halali, haramu, Sunnah, Bid´ah na yasiyojuzu wakati huo huo hutaki asiwepo yeyote atayekuzungumzia? Je, haya yanaingia akilini? Unawaeleza watu ni yepi halali na ni yepi haramu. Ukimuona mtu yuko katika haramu unamuamrisha kumcha Allaah na acha kutenda madhambi na unamnukulia Qur-aan na Sunnah. Unamueleza ni nini Bid´ah na Sunnah. Sasa unataka watu wote wakupende? Je, haya yanaingia akilini? Haya hayakumpata hata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kulipatikana watu waliomuudhi, kumpiga vita na kupambana naye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka akaumia, akavunjwa magego yake na mengi mengine yalimfika.

Hili haliwezekani. Yule mwenye kutaka watu wote wamuwie radhi, basi tambua kuwa huyu ni mwenye kupakana mafuta. Haiwezekani ukawaridhisha wote. Kwa nini? Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Mwenye kuwaridhisha watu kwa Khasira za Allaah, atapata Khasira za Allaah na za watu vilevile.”

Hata kama watakuwa radhi na wewe hivi sasa watakukasirikia baadaye. Kwa kuwa ni jambo lisilowezekana katika kila msimamo ukawa nao. Ni lazima wakukasirikie.

“Na mwenye kumridhisha Allaah kwa khasira za watu, Allaah Atakuwa radhi na yeye na watu watakuwa radhi naye pia.”

Kwa kuwa wanajua kuwa ni mkweli. Ni lazima kuwa na subira katika maudhi katika kufikisha elimu hii, kuwabainishia watu haki na kuwahimiza kushikamana nayo, na kuwabainishia watu upotevu na kuwatahadharisha na hilo.