Haiwezekani Kumuona Allaah Katika Maisha Haya

Kuhusu kuwa yawezekana kuonekana kwa Allaah katika maisha haya, wamesema baadhi kwamba kuna kauli mbili katika suala hili wakati wengine wanasema ya kwamba kuna uwezekano wa kuonekana kwa Allaah katika maisha haya. Maoni yote haya mawili ni upotofu. Maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa'ah wamekubaliana ya kwamba hakuna yeyote awezae kumuona Allaah katika maisha haya kwa macho. Wametofautiana tu ya kuwa Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alimuona [Allaah Mi´raaj] au hapana. Kumepokelewa kutoka sehemu mbalimbali kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuwa amesema haiwezekani kumuona Allaah katika maisha haya. Miongoni mwao, amepokea Muslim katika "as-Swahiyh" yake ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema wakati alipomtaja ad-Dajjaal: "Jueni ya kwamba hakuna mtu yeyote katika nyinyi ambaye atamuona Mola Wake mpaka pale atapokufa." Wakati Muusa bin ´Imraan ('alayhis-Salaam) alipomuomba Allaah kuweza kumuona, Allaah (Subhanahu wa Ta'ala) Akamjibu: لن تراني “Hutoniona!” Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 122

Kuhusu kuwa yawezekana kuonekana kwa Allaah katika maisha haya, wamesema baadhi kwamba kuna kauli mbili katika suala hili wakati wengine wanasema ya kwamba kuna uwezekano wa kuonekana kwa Allaah katika maisha haya. Maoni yote haya mawili ni upotofu. Maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa’ah wamekubaliana ya kwamba hakuna yeyote awezae kumuona Allaah katika maisha haya kwa macho. Wametofautiana tu ya kuwa Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimuona [Allaah Mi´raaj] au hapana. Kumepokelewa kutoka sehemu mbalimbali kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa amesema haiwezekani kumuona Allaah katika maisha haya. Miongoni mwao, amepokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema wakati alipomtaja ad-Dajjaal:

“Jueni ya kwamba hakuna mtu yeyote katika nyinyi ambaye atamuona Mola Wake mpaka pale atapokufa.”

Wakati Muusa bin ´Imraan (‘alayhis-Salaam) alipomuomba Allaah kuweza kumuona, Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Akamjibu:

لن تراني
“Hutoniona!”

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 122


  • Kitengo: Uncategorized , Kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013