Faida Tatu Za Kuamini Qadar

Daraja ya kwanza: Faida za kuamini Qadhwaa na Qadar Kuamini Qadhwaa na Qadar kuna faida kubwa: 1- Faida ya kwanza – na ni kubwa – ni kukamilisha nguzo za imani. Yule mwenye kupinga Qadhwaa na Qadar anakuwa hakukamilisha nguzo za imani ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezifasiri ikiwemo: “Imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.” 2- Faida ya piili: Mtu anakuwa imara na wala hababaishwi na wasiwasi na khofu. Bali anakuwa imara na kusema: “Yale ambayo Allaah Amenikadiria yatakuwepo sawa nikikaa au nisikae.” Kwa ajili hii Allaah Anasimulia kuhusu wanafiki waliposema siku ya Uhud: الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ “Wale ambao waliwaambia ndugu zao nao wakakaa (hawakwenda vitani): “Lau wangelitutii basi wasingeliuawa.” Sema: “Basi ziondoleeni (jiepusheni) nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli.” (al-´Imraan:168) Kukaa nyumbani hakuzuii mauti kama jinsi kutoka pia kwenda katika Jihaad hakuleti mauti na kufanya mtu kufa ikiwa Allaah Hakuyakadiria. Ni sababu, lakini ikiwa Allaah Hakukadiria hivyo hakuna athari yoyote na hakuna natija yake. Ni wangapi ambao wameingia katika uwanja wa vita na wanatoka hali ya kuwa wako salama na afya. Khaalid bin Waliyd (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati mauti yalipomjia, akasema: “Hakuna katika mwili wangu sehemu kiasi cha shibri isipokuwa kuna (athari ya makovu) ya kipigo.” Alikuwa anatamani shahadah na akapitia vita vikubwa na anatamani auwe katika njia ya Allaah, lakini Allaah Hakumkadiria hivyo. Hivyo, kuamini Qadhwaa na Qadar kunamfanya mtu kuwa na ujasiri na ushujaa na kumtegemea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama kukwepa hilo hakufidishi kitu. Anasema (Ta´ala): لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale ambao wameandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia.” (al-´Imraan:154) أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ “Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika ngome madhubuti.” (an-Nisaa:78) Qadhwaa ni lazima itimie na kutokea. Hakuna faida yoyote ya mtu kushindwa kufanya sababu zenye kuleta manufaa na kukomeka (kujiepusha) na sababu mbaya. Hili linamfanya mtu kuwa na nguvu, ushujaa na kumuamini Allaah (´Azza wa Jalla) na yanamwepusha mtu kuwa na mashaka, wasiwasi na utata unaowakumbuka watu wengi. Yanamwepusha mtu na wasiwasi. Kwa ajili hii watu wa imani walikuwa hawajiweki nyuma kutafuta yaliyo na kheri na faida. Kwa kuwa wanaamini Qadhwaa na Qadar. Hawakuwa wanasema kwamba wanaogopa mauti na kuuawa. Ikiwa mauti yamekadiriwa kwako yatakujia hata kama hukuyaendea kama jinsi ikiwa hayakukadiriwa kwako hayatokujia hata kama utakuwa katika khatari ilokubwa. 3- Faida ya nne: Mtu anapofikwa na msiba hakati tamaa. Kwa kuwa anaamnini kuwa hili limetokana na Qadhwaa na Qadar ya Allaah. Hili linawepesisha kukabiliana na misiba na wala mtu hakati tamaa kwa kupiga mayowe, kujipiga na kutamka maneno ya Kijaahiliyyah. Kinyume chake anakuwa ni mwenye subira na kutaraji malipo kwa Allaah. Kama Alivyosema (Ta´ala): وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ “Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Innaa liLLaahi wa Innaa Ilayhi Raaji’uwn” (Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake tutarejea). Hao juu yao zitakuwa Baraka kutoka kwa Mola wao na Rahmah, na hao ndio wenye kuongoka.” (al-Baqarah:155-157) Wanapofikwa na misiba hawazilaumu nafsi zao na kusema ni kwa sababu ya kadhaa, bali wanaridhia Qadhwaa na Qadar ya Allaah na kwamba msiba unafika sawa kwa hali yoyote ikiwa kama Allaah Amekadiria hilo. Makadirio yanafika kwa idhini ya Allaah. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 149-151

Daraja ya kwanza: Faida za kuamini Qadhwaa na Qadar

Kuamini Qadhwaa na Qadar kuna faida kubwa:

1- Faida ya kwanza – na ni kubwa – ni kukamilisha nguzo za imani. Yule mwenye kupinga Qadhwaa na Qadar anakuwa hakukamilisha nguzo za imani ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezifasiri ikiwemo:

“Imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.”

2- Faida ya piili: Mtu anakuwa imara na wala hababaishwi na wasiwasi na khofu. Bali anakuwa imara na kusema: “Yale ambayo Allaah Amenikadiria yatakuwepo sawa nikikaa au nisikae.” Kwa ajili hii Allaah Anasimulia kuhusu wanafiki waliposema siku ya Uhud:

الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
“Wale ambao waliwaambia ndugu zao nao wakakaa (hawakwenda vitani): “Lau wangelitutii basi wasingeliuawa.” Sema: “Basi ziondoleeni (jiepusheni) nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli.” (al-´Imraan:168)

Kukaa nyumbani hakuzuii mauti kama jinsi kutoka pia kwenda katika Jihaad hakuleti mauti na kufanya mtu kufa ikiwa Allaah Hakuyakadiria. Ni sababu, lakini ikiwa Allaah Hakukadiria hivyo hakuna athari yoyote na hakuna natija yake. Ni wangapi ambao wameingia katika uwanja wa vita na wanatoka hali ya kuwa wako salama na afya. Khaalid bin Waliyd (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati mauti yalipomjia, akasema:

“Hakuna katika mwili wangu sehemu kiasi cha shibri isipokuwa kuna (athari ya makovu) ya kipigo.”

Alikuwa anatamani shahadah na akapitia vita vikubwa na anatamani auwe katika njia ya Allaah, lakini Allaah Hakumkadiria hivyo.

Hivyo, kuamini Qadhwaa na Qadar kunamfanya mtu kuwa na ujasiri na ushujaa na kumtegemea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ama kukwepa hilo hakufidishi kitu. Anasema (Ta´ala):

لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ
“Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale ambao wameandikiwa kuuwawa kwenye mahali pa kuangukia.” (al-´Imraan:154)

أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ
“Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika ngome madhubuti.” (an-Nisaa:78)

Qadhwaa ni lazima itimie na kutokea. Hakuna faida yoyote ya mtu kushindwa kufanya sababu zenye kuleta manufaa na kukomeka (kujiepusha) na sababu mbaya. Hili linamfanya mtu kuwa na nguvu, ushujaa na kumuamini Allaah (´Azza wa Jalla) na yanamwepusha mtu kuwa na mashaka, wasiwasi na utata unaowakumbuka watu wengi. Yanamwepusha mtu na wasiwasi. Kwa ajili hii watu wa imani walikuwa hawajiweki nyuma kutafuta yaliyo na kheri na faida. Kwa kuwa wanaamini Qadhwaa na Qadar. Hawakuwa wanasema kwamba wanaogopa mauti na kuuawa. Ikiwa mauti yamekadiriwa kwako yatakujia hata kama hukuyaendea kama jinsi ikiwa hayakukadiriwa kwako hayatokujia hata kama utakuwa katika khatari ilokubwa.

3- Faida ya nne: Mtu anapofikwa na msiba hakati tamaa. Kwa kuwa anaamnini kuwa hili limetokana na Qadhwaa na Qadar ya Allaah. Hili linawepesisha kukabiliana na misiba na wala mtu hakati tamaa kwa kupiga mayowe, kujipiga na kutamka maneno ya Kijaahiliyyah. Kinyume chake anakuwa ni mwenye subira na kutaraji malipo kwa Allaah. Kama Alivyosema (Ta´ala):

وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ
“Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri. Wale ambao unapowafika msiba husema: “Innaa liLLaahi wa Innaa Ilayhi Raaji’uwn” (Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake tutarejea). Hao juu yao zitakuwa Baraka kutoka kwa Mola wao na Rahmah, na hao ndio wenye kuongoka.” (al-Baqarah:155-157)

Wanapofikwa na misiba hawazilaumu nafsi zao na kusema ni kwa sababu ya kadhaa, bali wanaridhia Qadhwaa na Qadar ya Allaah na kwamba msiba unafika sawa kwa hali yoyote ikiwa kama Allaah Amekadiria hilo. Makadirio yanafika kwa idhini ya Allaah.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 149-151


  • Kitengo: Uncategorized , Qadar
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014