Fadhila Za Kula Daku

Mtu ni mwenye haja ya kula na kunywa. Kwa ajili hii Allaah Hakumkataza mfungaji kula, kunywa na kufanya jimaa wakati wa usiku isipokuwa tu wakati wa mchana, kuanzia pale ambapo alfajiri inapoingia mpaka wakati jua linapozama. Allaah Anapenda watu wale daku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu daku: “Kuleni daku. Hakika katika kula daku kuna baraka.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Allaah (´Azza wa Jalla) na Malaika Wake wanawaswalia wenye kula daku.” (Ibn Hibbaan (3467), atw-Twabaraaniy i ”al-Awsatw” (6434) na Abu Nu´aym (8/320). Hasan kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb” (1070)) Kwa nini? Daku si ni chakula tu ambacho mtu anakula kwa matamanio. Kwa sababu nia yake ni kutekeleza maamrisho ya Allaah ili aweze kupata nguvu za kumwabudu Allaah. Kwa ajili hio kila ambavyo daku itacheleweshwa ndio bora zaidi: وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ”Na kuleni na kunyweni mpaka ibainike kwenu weupe (wa Afajiri) kutokana na weusi (wa usiku).” (02:187) Ama yule anayekula usiku mzima na kujaza tumbo lake kisha analala nyuma na wala haamki kula daku pamoja na Waislamu wenzake na wala haswali hata al-Fajr, huyu kwa hakika hakutekeleza maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Amechofanya ni kutekeleza maamrisho na hawaa ya nafsi yake. Yuko macho usiku mzima ambapo anakesha kwa kumuasi Allaah na analala wakati ambapo anatakiwa kumtii Allaah (´Azza wa Jalla).

Mtu ni mwenye haja ya kula na kunywa. Kwa ajili hii Allaah Hakumkataza mfungaji kula, kunywa na kufanya jimaa wakati wa usiku isipokuwa tu wakati wa mchana, kuanzia pale ambapo alfajiri inapoingia mpaka wakati jua linapozama. Allaah Anapenda watu wale daku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu daku:

“Kuleni daku. Hakika katika kula daku kuna baraka.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jalla) na Malaika Wake wanawaswalia wenye kula daku.” (Ibn Hibbaan (3467), atw-Twabaraaniy i ”al-Awsatw” (6434) na Abu Nu´aym (8/320). Hasan kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb” (1070))

Kwa nini? Daku si ni chakula tu ambacho mtu anakula kwa matamanio. Kwa sababu nia yake ni kutekeleza maamrisho ya Allaah ili aweze kupata nguvu za kumwabudu Allaah. Kwa ajili hio kila ambavyo daku itacheleweshwa ndio bora zaidi:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ
”Na kuleni na kunyweni mpaka ibainike kwenu weupe (wa Afajiri) kutokana na weusi (wa usiku).” (02:187)

Ama yule anayekula usiku mzima na kujaza tumbo lake kisha analala nyuma na wala haamki kula daku pamoja na Waislamu wenzake na wala haswali hata al-Fajr, huyu kwa hakika hakutekeleza maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Amechofanya ni kutekeleza maamrisho na hawaa ya nafsi yake. Yuko macho usiku mzima ambapo anakesha kwa kumuasi Allaah na analala wakati ambapo anatakiwa kumtii Allaah (´Azza wa Jalla).