Fadhila Za Kufanya Da´wah

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaapa: ”Ninaapa kwa Allaah... ” Anatilia nguvu ili kusiwepo kitu kama mashaka au wasiwasi. ”Ninaapa kwa Allaah lau Allaah Atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.” yaan kwa sababu Da´wah yako, nasaha zako, maelekezo yako, uvumilivu wako na elimu yako. Mlinganizi anahitajia kuwa na subira, ustahamilivu na elimu ili aweze kulingania kwa elimu. Anayelinganiwa anaweza kuwa na utata na ubabainishaji na hivyo wewe ukawa umemuondoshea utata na ubabaishaji huu. ”... lau Allaah Atamuongoza mtu mmoja... ” Ametukuka Allaah! Mtu mmoja tu. Vipi lau itakuwa ni makumi na mamia na maelfu ya watu, wewe mbele ya Allaah utakuwa na ujira mkubwa wa kiasi gani! Jifikirie lau Allaah wote hawa anawaongoza kupitia kwako, basi yanawekwa katika mizani ya mazuri yako. Wewe matendo yako ni madogo. Vovyote ambavyo mtu atajitahidi kufanya matendo mema pamoja na mapungufu yake, bado yatakuwa ni madogo. Lakini lau Allaah Atawaongoza wale Anaowataka kupitia kwako, basi matendo yao yote yatawekwa katika mizani ya mazuri yako na wao hakutopunguzwa kitu katika ujira wao. Ujira wao utabaki kikamilifu kama jinsi ulivo, ujira wa matendo yao na mema yao. Lakini kwa vile wewe ndiye sababu baada ya Allaah katika kuongoka kwao, basi Allaah Anakukirimu na Kukupa ujira na thawabu mfano wa za kila mmoja watazopata wao. Wewe hutopunguziwa kitu kama jinsi na wao pia hawatopunguziwa kitu chochote. ”Mwenye kuelekeza katika uongofu ana ujira mfano wa yule mwenye kutenda... ” ”... ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.” Katika wakati huo ngamia ndio ilikuwa mali kubwa ya waarabu. Wakati huo hawakuwa na mandege, magari na aina mbali mbali ya mipando mikubwa mikubwa ya kifakhari kama ya leo. Kwa hii leo unaeza kuambiwa: ”... ni bora kwako kuliko mandege na aina mbali mbali ya mipando mikubwa ya kifakhari.” Vilevile linamuhusu mwanamke lau Allaah Atamuongoza mwanamke mmoja kupitia kwake. Vipi lau watakuwa wengi! Mfano wa matendo kama haya mazuri washindane wale wenye kushindana kwa kuwa ni katika thawabu kubwa kabisa. Wewe pengine hukujaaliwa kwenda Hajj katika mwaka moja wapo na yule ambaye Allaah Amemuongoza kupitia kwako amejaaliwa kwenda Hajj. Basi wewe unapata ujira sawa sawa na ujira wake. Unahesabika ni kama vile wewe ndiye umemuhijisha. Vipi lau wataenda Hajj watu mia ambao Allaah Amewaongoza kupitia kwako! Jifikirie utakua na ujira wa kiasi gani katika mwaka mmoja. Utahesabika umefanya Hajj mia. Pengine hukujaaliwa kwenda ´Umrah na yule ambaye Allaah Amemuongoza kupitia kwako ameenda ´Umrah. Basi wewe una ujira sawa sawa na ´Umrah yake na yeye anapata ujira wa ´Umrah yake kikamilifu. Vipi lau makumi ya watu wote watafanya ´Umrah miongoni mwa wale ambao Allaah Amewaongoza kupitia mikono yako! Unahesabika umefanya makumi ya ´Umrah kwa kulingana na idadi yake [walioenda]. Vipi basi katika mlango huu – wa Da´wah – wasishindane wale wenye kushindana!

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaapa:

”Ninaapa kwa Allaah… ”

Anatilia nguvu ili kusiwepo kitu kama mashaka au wasiwasi.

”Ninaapa kwa Allaah lau Allaah Atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”

yaan kwa sababu Da´wah yako, nasaha zako, maelekezo yako, uvumilivu wako na elimu yako. Mlinganizi anahitajia kuwa na subira, ustahamilivu na elimu ili aweze kulingania kwa elimu. Anayelinganiwa anaweza kuwa na utata na ubabainishaji na hivyo wewe ukawa umemuondoshea utata na ubabaishaji huu.

”… lau Allaah Atamuongoza mtu mmoja… ”

Ametukuka Allaah! Mtu mmoja tu. Vipi lau itakuwa ni makumi na mamia na maelfu ya watu, wewe mbele ya Allaah utakuwa na ujira mkubwa wa kiasi gani! Jifikirie lau Allaah wote hawa anawaongoza kupitia kwako, basi yanawekwa katika mizani ya mazuri yako.

Wewe matendo yako ni madogo. Vovyote ambavyo mtu atajitahidi kufanya matendo mema pamoja na mapungufu yake, bado yatakuwa ni madogo. Lakini lau Allaah Atawaongoza wale Anaowataka kupitia kwako, basi matendo yao yote yatawekwa katika mizani ya mazuri yako na wao hakutopunguzwa kitu katika ujira wao. Ujira wao utabaki kikamilifu kama jinsi ulivo, ujira wa matendo yao na mema yao. Lakini kwa vile wewe ndiye sababu baada ya Allaah katika kuongoka kwao, basi Allaah Anakukirimu na Kukupa ujira na thawabu mfano wa za kila mmoja watazopata wao. Wewe hutopunguziwa kitu kama jinsi na wao pia hawatopunguziwa kitu chochote.

”Mwenye kuelekeza katika uongofu ana ujira mfano wa yule mwenye kutenda… ”

”… ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.”

Katika wakati huo ngamia ndio ilikuwa mali kubwa ya waarabu. Wakati huo hawakuwa na mandege, magari na aina mbali mbali ya mipando mikubwa mikubwa ya kifakhari kama ya leo. Kwa hii leo unaeza kuambiwa:

”… ni bora kwako kuliko mandege na aina mbali mbali ya mipando mikubwa ya kifakhari.”

Vilevile linamuhusu mwanamke lau Allaah Atamuongoza mwanamke mmoja kupitia kwake. Vipi lau watakuwa wengi! Mfano wa matendo kama haya mazuri washindane wale wenye kushindana kwa kuwa ni katika thawabu kubwa kabisa.

Wewe pengine hukujaaliwa kwenda Hajj katika mwaka moja wapo na yule ambaye Allaah Amemuongoza kupitia kwako amejaaliwa kwenda Hajj. Basi wewe unapata ujira sawa sawa na ujira wake. Unahesabika ni kama vile wewe ndiye umemuhijisha. Vipi lau wataenda Hajj watu mia ambao Allaah Amewaongoza kupitia kwako! Jifikirie utakua na ujira wa kiasi gani katika mwaka mmoja. Utahesabika umefanya Hajj mia. Pengine hukujaaliwa kwenda ´Umrah na yule ambaye Allaah Amemuongoza kupitia kwako ameenda ´Umrah. Basi wewe una ujira sawa sawa na ´Umrah yake na yeye anapata ujira wa ´Umrah yake kikamilifu. Vipi lau makumi ya watu wote watafanya ´Umrah miongoni mwa wale ambao Allaah Amewaongoza kupitia mikono yako! Unahesabika umefanya makumi ya ´Umrah kwa kulingana na idadi yake [walioenda]. Vipi basi katika mlango huu – wa Da´wah – wasishindane wale wenye kushindana!