Elimu Ni Sifa Ya Dhati Ya Allaah (´Azza wa Jalla)

Katika Aayah tukufu – Aayah ya 02:255 – kuna uthibitisho Allaah kuwa na Sifa ya Elimu. Ni Sifa ya Dhati inayolingana na Ukubwa na Utukufu wa Allaah. Kuna Aayah nyingi katika Qur-aan ambazo zimekuja kwa Jina hili ´Aliym. Wakati fulani zinakuja kwa njia ya ishara na wakati mwingine zinakuja kwa njia ya Jina. ´Aliym ni Jina katika Majina ya Allaah (´Azza wa Jalla). Anajua. Anajua kwa Elimu: لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ “Hakifichiki Kwake (chochote kile hata kiwe na) uzito wa atomu (au sisimizi) mbinguni wala ardhini, na wala kidogo zaidi kuliko hicho, na wala kikubwa zaidi kuliko hicho isipokuwa (kimeshaandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (mambo yote – Lawhum-Mahfuudhw).” (34:03) Himidi zote ni za Allaah Ambaye Amewafunza waja yale ambayo walikuwa hawayajui kwa kumtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kuteremsha Kitabu na Sunnah kwao na kuwabainishia viumbe hawa wawili (majini na wanaadamu). Mwandishi: Imaam Abu Ja´far al-Warraaq at-Twahaawiy al-Muswriy Chanzo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=960&size=2h&ext=.rm

Katika Aayah tukufu – Aayah ya 02:255 – kuna uthibitisho Allaah kuwa na Sifa ya Elimu. Ni Sifa ya Dhati inayolingana na Ukubwa na Utukufu wa Allaah. Kuna Aayah nyingi katika Qur-aan ambazo zimekuja kwa Jina hili ´Aliym. Wakati fulani zinakuja kwa njia ya ishara na wakati mwingine zinakuja kwa njia ya Jina. ´Aliym ni Jina katika Majina ya Allaah (´Azza wa Jalla). Anajua. Anajua kwa Elimu:

لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ
“Hakifichiki Kwake (chochote kile hata kiwe na) uzito wa atomu (au sisimizi) mbinguni wala ardhini, na wala kidogo zaidi kuliko hicho, na wala kikubwa zaidi kuliko hicho isipokuwa (kimeshaandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (mambo yote – Lawhum-Mahfuudhw).” (34:03)

Himidi zote ni za Allaah Ambaye Amewafunza waja yale ambayo walikuwa hawayajui kwa kumtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kuteremsha Kitabu na Sunnah kwao na kuwabainishia viumbe hawa wawili (majini na wanaadamu).

Mwandishi: Imaam Abu Ja´far al-Warraaq at-Twahaawiy al-Muswriy
Chanzo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=960&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Elimu (Ujuzi) wa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 4th, April 2014