Dalili Zinazotumiwa Na Wale Wanaopinga Kuonekana Kwa Allaah Aakhirah

Ama Kauli Yake (Ta´ala): لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ “Macho hayamdiriki (hayamzunguki) bali Yeye Anayadiriki macho.” (al-An´aam:103) “al-Idraak” sio kuona. Wewe unaliona jua lakini huwezi “al-Idraak”, bi maana huwezi kulizunguka lote. Huwezi kuliona katika kila pande. Hata hivyo unaliona. Kadhalika waumini watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah, lakini hata hivyo hawatomzunguka kutokana na Ukubwa Wake (Jalla wa ´Alaa) na wala (wao) hawawezi kudiriki elimu Yake. Wewe hivi sasa unaliona jua, lakini hulidiriki kwa ukali wake na mpaka wake. Huwezi hilo. Hili ni kwa kitu ambacho ni kiumbe. Vipi kwa Muumba (Subhaanahu wa Ta´ala)? Kukanusha al-Idraak sio kukanusha ar-Ru´yaa. Bali imesemekana kwamba kukanusha al-Idraak kumeonesha dalili ya kwamba ataonekana, lakini haitokuwa al-Idraak, bi maana hatozungukwa (Subhaanahu wa Ta´ala). Kauli ya Allaah kumwambia Muusa: لَن تَرَانِي “Hutoniona!” (al-A´raaf:143) Maanake si kwamba ni ukanushaji wa milele. Bali: لَن تَرَانِي “Hutoniona!” (al-A´raaf:143) yaani duniani. Kwa dalili kwamba imethibiti kuwa ataonekana Aakhirah. Isitoshe watu wa lugha wanasema neno “lan” sio la ukanushaji wa milele bali ni la ukanushaji kwa muda fulani. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 82

Ama Kauli Yake (Ta´ala):

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ
“Macho hayamdiriki (hayamzunguki) bali Yeye Anayadiriki macho.” (al-An´aam:103)

“al-Idraak” sio kuona. Wewe unaliona jua lakini huwezi “al-Idraak”, bi maana huwezi kulizunguka lote. Huwezi kuliona katika kila pande. Hata hivyo unaliona. Kadhalika waumini watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah, lakini hata hivyo hawatomzunguka kutokana na Ukubwa Wake (Jalla wa ´Alaa) na wala (wao) hawawezi kudiriki elimu Yake.

Wewe hivi sasa unaliona jua, lakini hulidiriki kwa ukali wake na mpaka wake. Huwezi hilo. Hili ni kwa kitu ambacho ni kiumbe. Vipi kwa Muumba (Subhaanahu wa Ta´ala)?

Kukanusha al-Idraak sio kukanusha ar-Ru´yaa. Bali imesemekana kwamba kukanusha al-Idraak kumeonesha dalili ya kwamba ataonekana, lakini haitokuwa al-Idraak, bi maana hatozungukwa (Subhaanahu wa Ta´ala).

Kauli ya Allaah kumwambia Muusa:

لَن تَرَانِي
“Hutoniona!” (al-A´raaf:143)

Maanake si kwamba ni ukanushaji wa milele. Bali:

لَن تَرَانِي
“Hutoniona!” (al-A´raaf:143)

yaani duniani. Kwa dalili kwamba imethibiti kuwa ataonekana Aakhirah.

Isitoshe watu wa lugha wanasema neno “lan” sio la ukanushaji wa milele bali ni la ukanushaji kwa muda fulani.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 82


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 14th, February 2014