Dalili Ya Vidole Vya Allaah

´Abdullaah bin Mas'uud katueleza kwamba kuna mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na kumwambia: “Abul-Qaasim, kwa hakika Allaah Atabeba viumbe katika Kidole, mbingu katika Kidole, ardhi katika Kidole, bahari katika Kidole na nyota katika Kidole.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka dalili ya kuthibitisha kiasi ambacho meno ya magego yakaonekana na Allaah (´Azza wa Jalla) Akateremsha: وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه "Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia." Ibn Mas'uud kasema pia: “Padiri wa kiyahudi alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Muhammad, katika Tawrat tunapata ya kwamba Allaah siku ya Qiyaamah Atakuja kuziweka mbingu katika Kidole, ardhi katika Kidole, milima katika Kidole, nyota katika Kidole na baki ya viumbe katika Kidole. Halafu Atawatikisa na kusema: “Mimi ndiye Maalik.”” Hivyo akacheka Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kiasi ambacho meno yake ya magego yakaonekana ishara ya kuonesha kuwa Padiri kasema kweli. Kisha akasoma: وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه "Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia." Wanachuoni wamekubaliana kwamba Hadiyth hii ni Swahiyh. Wahb bin Munabbih alisema: "Viumbe vyote na ardhi vitaenda sambamba katika Kitanga cha Mkono wa Allaah si lolote zaidi kuliko mbegu ya haradali." an-Nawwaas bin Sam'aan alisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema (katika maana): "Hakuna moyo isipokuwa uko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah ('Azza wa Jalla); Akitaka kuziweka sawa, Anaziweka sawa. Na Akitaka kuzipotosha, Anazipotosha.” Kisha akasema: “Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo, uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako.” Jaabir kasema: "Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema mara nyingi (katika maana): “Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo, uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako.” Kukasemwa: “Ewe Mtume wa Allaah, je una khofu juu yetu ilihali tumekuamini na yale uliyokuja nayo?” Hivyo akasema (katika maana): “Kwa hakika, mioyo iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Mwingi wa Rahmah (´Azza wa Jalla) na Anazigeuza na kuzipeleka namna hii”” – Sufyaan ath-Thawriy kalieleza kwa kidole cha kuashiria (cha shahada) na kidole kirefu na akavitikisa. Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 83-93 Maktabah al-Ghurabaa’ al-Athariyyah, 1414/1994.

´Abdullaah bin Mas’uud katueleza kwamba kuna mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumwambia:

“Abul-Qaasim, kwa hakika Allaah Atabeba viumbe katika Kidole, mbingu katika Kidole, ardhi katika Kidole, bahari katika Kidole na nyota katika Kidole.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka dalili ya kuthibitisha kiasi ambacho meno ya magego yakaonekana na Allaah (´Azza wa Jalla) Akateremsha:

وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه
“Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia.”

Ibn Mas’uud kasema pia:
“Padiri wa kiyahudi alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Muhammad, katika Tawrat tunapata ya kwamba Allaah siku ya Qiyaamah Atakuja kuziweka mbingu katika Kidole, ardhi katika Kidole, milima katika Kidole, nyota katika Kidole na baki ya viumbe katika Kidole. Halafu Atawatikisa na kusema: “Mimi ndiye Maalik.”” Hivyo akacheka Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kiasi ambacho meno yake ya magego yakaonekana ishara ya kuonesha kuwa Padiri kasema kweli. Kisha akasoma:
وما قدروا الله حق قدره والأرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه
“Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia.” Wanachuoni wamekubaliana kwamba Hadiyth hii ni Swahiyh.

Wahb bin Munabbih alisema:
“Viumbe vyote na ardhi vitaenda sambamba katika Kitanga cha Mkono wa Allaah si lolote zaidi kuliko mbegu ya haradali.”

an-Nawwaas bin Sam’aan alisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema (katika maana):
“Hakuna moyo isipokuwa uko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (‘Azza wa Jalla); Akitaka kuziweka sawa, Anaziweka sawa. Na Akitaka kuzipotosha, Anazipotosha.” Kisha akasema: “Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo, uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako.”

Jaabir kasema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema mara nyingi (katika maana): “Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo, uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako.” Kukasemwa: “Ewe Mtume wa Allaah, je una khofu juu yetu ilihali tumekuamini na yale uliyokuja nayo?” Hivyo akasema (katika maana): “Kwa hakika, mioyo iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Mwingi wa Rahmah (´Azza wa Jalla) na Anazigeuza na kuzipeleka namna hii”” – Sufyaan ath-Thawriy kalieleza kwa kidole cha kuashiria (cha shahada) na kidole kirefu na akavitikisa.

Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda
Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 83-93
Maktabah al-Ghurabaa’ al-Athariyyah, 1414/1994.


  • Kitengo: Uncategorized , Vidole vya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013