Dalili Ya Uso Wa Allaah (1)

Allaah (Jalla wa 'Azz) Anasema: كل شيء هالك إلا وجهه له الحكم وإليه ترجعون "Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake. Ana Hukumu (ya mambo yote) na Kwake Pekee mtarejeshwa.” Hali kadhalika, Anasema Allaah ('Azza wa Jalla): ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام "Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.” Pia kumetajwa ambayo ni sahihi yamethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), ambayo yanaonesha ya kuwa ni ya uhakika ['Alaa Haqiyqati dhaalik]. Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Anasema (katika maana): "Bustani ya Firdaws ni nne; mbili ni za dhahabu – vipodozi vyake na usaidizi na vile vilivyomo katika hivyo, na mbili ni za fedha – vipodozi vyake na vile vilivyomo humo. Kitu pekee ambacho kipo kati ya watu na uono wa Mola wao, ni pazia ya enzi kwenye Uso Wake katika Bustani ya Edeni". Suhayb amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kafasiriwa Aayah: للذين أحسنوا الحسنى وزيادة "Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa (Pepo) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).”: "Watapata kuona Uso wa Mola wao (Azz wa Jalla)." Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema katika "al-Musnad": "Watapata kuona Uso wa Allaah (Azza wa Jalla)." Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema: "Watapata kuona Uso wa Allaah (´Azza wa ´Alaa)." Hali kadhalika amefasiri Hudhayfah bin al-Yamaan. Jaabir amesema (katika maana): "Sema: “Yeye ni Al-Qaadir (Muweza daima) wa Kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu... " ilipoteremshwa, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): "Najikinga kwa Uso Wako" na “... au kutoka chini ya miguu yenu... " yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): "Najikinga kwa Uso Wako.'" Ibn Mas'uud akasema: "Mola Wenu hana usiku wala siku yoyote. Mwanga wa mbingu unatoka kwenye nuru ya Uso Wake." 'Abdullaah bin Ja'far kasema: "Wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alipokwenda Twaa'if, aliomba (katika maana): "Allaah, naomba kinga kwa nuru ya Uso Wako inayoangaza mbingu.”" Hadiyth hii inatoa dalili kuonyesha maana ya Maneno ya Allaah (Ta´ala): الله نور السماوات والأرض مثل نوره كمشكاة فيها مصباح "Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake kama shubaka (lenye kuwekwa) taa ndani yake. Taa hiyo iko katika gilasi (tungi)." Ibn 'Umar kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuhusu nafasi ya juu watu wa Peponi watafikia (katika maana): "Yule ambaye ana nafasi bora katika wao ni yule ambaye anaangalia Uso wa Allaah (´Azza wa Jalla) mara mbili kwa siku." Allaah ('Azza wa Jalla) Kasema: وجوه يومئذ ناضرة إلى ربها ناظرة "Zipo nyuso siku hiyo zitaong'ara, zinamwangalia Mola Wao." Wafasiri wa Qur-aan kama Ibn 'Abbaas , na Maswahabah wengine na Taabi'uun kama Muhammad bin Ka´b, ´Abdur-Rahmaan bin Saabit, al-Hasan bin Abiyl-Hasan , 'Ikrimah , Abu Swaalih, Sa´iyd bin Jubayr na wengine wamekubaliana kwamba nyuso hizi zitaangalia Uso wa Mola Wao. Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 94-103 Maktabah al-Ghurabaa al-Athariyyah, 1414/1994.

Allaah (Jalla wa ‘Azz) Anasema:

كل شيء هالك إلا وجهه له الحكم وإليه ترجعون
“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake. Ana Hukumu (ya mambo yote) na Kwake Pekee mtarejeshwa.”

Hali kadhalika, Anasema Allaah (‘Azza wa Jalla):

ويبقى وجه ربك ذو الجلال والإكرام
“Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”

Pia kumetajwa ambayo ni sahihi yamethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambayo yanaonesha ya kuwa ni ya uhakika [‘Alaa Haqiyqati dhaalik].

Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) Anasema (katika maana):

“Bustani ya Firdaws ni nne; mbili ni za dhahabu – vipodozi vyake na usaidizi na vile vilivyomo katika hivyo, na mbili ni za fedha – vipodozi vyake na vile vilivyomo humo. Kitu pekee ambacho kipo kati ya watu na uono wa Mola wao, ni pazia ya enzi kwenye Uso Wake katika Bustani ya Edeni”.

Suhayb amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kafasiriwa Aayah:

للذين أحسنوا الحسنى وزيادة
“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa (Pepo) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).”:

“Watapata kuona Uso wa Mola wao (Azz wa Jalla).”

Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema katika “al-Musnad”:
“Watapata kuona Uso wa Allaah (Azza wa Jalla).”

Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:
“Watapata kuona Uso wa Allaah (´Azza wa ´Alaa).”

Hali kadhalika amefasiri Hudhayfah bin al-Yamaan.

Jaabir amesema (katika maana):
“Sema: “Yeye ni Al-Qaadir (Muweza daima) wa Kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu… ” ilipoteremshwa, akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Najikinga kwa Uso Wako” na “… au kutoka chini ya miguu yenu… ” yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Najikinga kwa Uso Wako.'”

Ibn Mas’uud akasema:
“Mola Wenu hana usiku wala siku yoyote. Mwanga wa mbingu unatoka kwenye nuru ya Uso Wake.”

‘Abdullaah bin Ja’far kasema:
“Wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipokwenda Twaa’if, aliomba (katika maana): “Allaah, naomba kinga kwa nuru ya Uso Wako inayoangaza mbingu.””

Hadiyth hii inatoa dalili kuonyesha maana ya Maneno ya Allaah (Ta´ala):

الله نور السماوات والأرض مثل نوره كمشكاة فيها مصباح
“Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake kama shubaka (lenye kuwekwa) taa ndani yake. Taa hiyo iko katika gilasi (tungi).”

Ibn ‘Umar kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuhusu nafasi ya juu watu wa Peponi watafikia (katika maana):
“Yule ambaye ana nafasi bora katika wao ni yule ambaye anaangalia Uso wa Allaah (´Azza wa Jalla) mara mbili kwa siku.”

Allaah (‘Azza wa Jalla) Kasema:

وجوه يومئذ ناضرة إلى ربها ناظرة
“Zipo nyuso siku hiyo zitaong’ara, zinamwangalia Mola Wao.”

Wafasiri wa Qur-aan kama Ibn ‘Abbaas , na Maswahabah wengine na Taabi’uun kama Muhammad bin Ka´b, ´Abdur-Rahmaan bin Saabit, al-Hasan bin Abiyl-Hasan , ‘Ikrimah , Abu Swaalih, Sa´iyd bin Jubayr na wengine wamekubaliana kwamba nyuso hizi zitaangalia Uso wa Mola Wao.

Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda
Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 94-103
Maktabah al-Ghurabaa al-Athariyyah, 1414/1994.


  • Kitengo: Uncategorized , Uso wa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013