Dalili Ya Kwamba Ashaa´irah Sio Katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah

´Allaamah Muhammad al-Jaamiy: Nitawajia sifa mbili khatari sana mpaka mkinaike ya kwamba sio katika Ah-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Na moja wapo ni Sifa ya al-´Uluw (Allaah Kuwa juu). Katika "Aqiydah as-Sanusiyyah" wanasema: "Allaah Hayuko juu ya ´Arshi, wala chini ya ´Arshi, wala kuliani, wala kushotoni." Nini maana yake? Huku ni kukanusha kabisa kuwepo kwa Allaah. Jahmiyyah nao wanasema: "Allaah Hayuko ndani ya ulimwengu, wala nje ya ulimwengu, wala Hakufungamana na wala Hakutengana na ulimwengu." Anaesema maneno kama haya, kisha anasema Maneno ya Allaah Qur-aan ya kwamba imeumbwa, kama wanavyosema Mu´tazilah. Ashaa´irah wanaafikiana na Mu´tazilah kwa kuamini ya kwamba Qur-aan imeumbwa. Tofauti yao ni kuwa, Ashaa´irahwanathibitisha Maneno yenyewe tu yasiyokuwa na herufi wala sauti. Na Mu´tazilah hawathibitishi chochote. Ina maana Mu´tazilah wanaamini ya kwamba Allaah Anaongea bila ya Maneno. Na Ashaa´irah wamaani ya kwamba Allaah Anaongea kwa Maneno yenyewe yasiyokuwa na herufi wala sauti. Ama Qur-aan hii [tulionayo] imeumbwa na hilo wanakubaliana na Mu´tazilah. Na Salaf wamekubaliana kuamini ya kwamba Qur-aan imeumbwa ni kufuru. Hali kadhalika wamekubaliana yule mwenye kupinga Sifa iliothibiti katika Kitabu na Sunnah ni kafiri, maadamu hakuna vikwazo baina yake yeye na Takfiyr. Ashaa´irah katika Sifa kubwa waliopinga ni Sifa ya ´Uluw (kuwa juu kwa Allaah) na Sifa ya Maneno na kuamini kwamba Qur-aan imeumbwa. Isitoshe, wanaharibu Sifa zote za Allaah. Ar-Rahmah, Ar-Ridhwaa, Al-Mahabbah, Al-Ghadhwab, Sifa zote hizi wanaziharibu. Vipi watakuwa ni katika Ah-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Ni kwelu ya kwamba katika milango mingi wanaafikiana na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, ni katika Inswaaf kusema - kama alivyosema Shaykh-ul-Islaam - ni pote lililo karibu [na Ahl-us-Sunnah], na mtu asisemi ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

´Allaamah Muhammad al-Jaamiy:

Nitawajia sifa mbili khatari sana mpaka mkinaike ya kwamba sio katika Ah-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Na moja wapo ni Sifa ya al-´Uluw (Allaah Kuwa juu). Katika “Aqiydah as-Sanusiyyah” wanasema:

“Allaah Hayuko juu ya ´Arshi, wala chini ya ´Arshi, wala kuliani, wala kushotoni.”

Nini maana yake? Huku ni kukanusha kabisa kuwepo kwa Allaah. Jahmiyyah nao wanasema:

“Allaah Hayuko ndani ya ulimwengu, wala nje ya ulimwengu, wala Hakufungamana na wala Hakutengana na ulimwengu.”

Anaesema maneno kama haya, kisha anasema Maneno ya Allaah Qur-aan ya kwamba imeumbwa, kama wanavyosema Mu´tazilah. Ashaa´irah wanaafikiana na Mu´tazilah kwa kuamini ya kwamba Qur-aan imeumbwa. Tofauti yao ni kuwa, Ashaa´irahwanathibitisha Maneno yenyewe tu yasiyokuwa na herufi wala sauti. Na Mu´tazilah hawathibitishi chochote. Ina maana Mu´tazilah wanaamini ya kwamba Allaah Anaongea bila ya Maneno. Na Ashaa´irah wamaani ya kwamba Allaah Anaongea kwa Maneno yenyewe yasiyokuwa na herufi wala sauti. Ama Qur-aan hii [tulionayo] imeumbwa na hilo wanakubaliana na Mu´tazilah. Na Salaf wamekubaliana kuamini ya kwamba Qur-aan imeumbwa ni kufuru. Hali kadhalika wamekubaliana yule mwenye kupinga Sifa iliothibiti katika Kitabu na Sunnah ni kafiri, maadamu hakuna vikwazo baina yake yeye na Takfiyr. Ashaa´irah katika Sifa kubwa waliopinga ni Sifa ya ´Uluw (kuwa juu kwa Allaah) na Sifa ya Maneno na kuamini kwamba Qur-aan imeumbwa. Isitoshe, wanaharibu Sifa zote za Allaah. Ar-Rahmah, Ar-Ridhwaa, Al-Mahabbah, Al-Ghadhwab, Sifa zote hizi wanaziharibu. Vipi watakuwa ni katika Ah-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Ni kwelu ya kwamba katika milango mingi wanaafikiana na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, ni katika Inswaaf kusema – kama alivyosema Shaykh-ul-Islaam – ni pote lililo karibu [na Ahl-us-Sunnah], na mtu asisemi ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.