Chakula Hakitiwi Ila

2064 - Yahyaa bin Yahya, Zuhayr bin Harb na Ismaa´iyl bin Ishaaq alitueleza: Jariyr alitueleza, kutoka kwa al-A'mash, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema: "Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikuwa kamwe hakitii chakula ila. Kama anapenda kitu, hukila, na kama hakipendi, hukiacha." UFAFANUZI: Hii ni katika sifa iliyopendekezwa sana katika meza. Mfano wa kukitia ila chakula ni kama kusema kina chumvi sana au kina chumvi kidogo, ni kikali, khafifu, kinene, hakikuwiva na kadhalika. Ama kuhusiana na Hadiyth ambapo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alisema kwamba hali nyama ya kenge, ni maelezo tu ya kwamba havutiwi na aina hii ya chakula. Mmwandishi: Imaam Muslim bin al-Hajjaaj an-Niysaabuuriy Chanzo: al-Musnad as-Swahiyh (2064) Sherehe: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (d. 677) Chanzo: Sharh Swahiyh Muslim (14/23)

2064 – Yahyaa bin Yahya, Zuhayr bin Harb na Ismaa´iyl bin Ishaaq alitueleza: Jariyr alitueleza, kutoka kwa al-A’mash, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa kamwe hakitii chakula ila. Kama anapenda kitu, hukila, na kama hakipendi, hukiacha.”

UFAFANUZI:

Hii ni katika sifa iliyopendekezwa sana katika meza.

Mfano wa kukitia ila chakula ni kama kusema kina chumvi sana au kina chumvi kidogo, ni kikali, khafifu, kinene, hakikuwiva na kadhalika.

Ama kuhusiana na Hadiyth ambapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema kwamba hali nyama ya kenge, ni maelezo tu ya kwamba havutiwi na aina hii ya chakula.

Mmwandishi: Imaam Muslim bin al-Hajjaaj an-Niysaabuuriy
Chanzo: al-Musnad as-Swahiyh (2064)
Sherehe: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (d. 677)
Chanzo: Sharh Swahiyh Muslim (14/23)


  • Kitengo: Uncategorized , Chakula
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 20th, January 2014