Chakula Cha Kati Na Kati Katika Ramadhaan

Miongoni mwa adabu za kula na kunywa ni mtu kutokula sana na khaswa mfungaji. Asile na kunywa sana kwa kiasi cha kwamba akajaza tumbo lake mpaka akawa na uzito wa kumuabudu Allaah na khaswa katika Ramadhaan. Kula na kunywa sana kunamzuia mtu kufanya ´ibaadah. Kunamfanya mtu kuwa mzembe wakati wa ´ibaadah. Ale na kunywa kwa kiasi cha kuwa sawa kwenye mgongo na kumuabudu Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: "Kama ukilazimika kula hakikisha theluthi moja ya tumbo lako unaijaza chakula, theluthi moja maji na acha theluthi moja kwa ajili ya hewa.” Bi maana kiasi kidogo cha kumfanya awe sawasawa. Mtu anatakiwa kuwa kati na kati kimaumbile na kidini. Asiwe kama mnyama asiyekuwa na hamu nyingine zaidi ya kula na kunywa. Hali kadhalika kulala. Kunasababisha mwanaadamu kukosa manufaa yake mengi katika Dini na dunia yake. Chakula kidogo ni chenye manufaa kwa njia ya matibabu. Kama jinsi kinavyonufaisha ´ibaadah, kadhalika afya. Maradhi mengi yanatokamana na kula na kunywa sana na maakulati mbali mbali. Kwa ajili hiyo huwa inasemwa huenda mlo mmoja ukazuia milo mingi huko mbeleni. Mtu anatakiwa kuwa mkati na kati. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema: وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ “Na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.” (07:31) وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا “Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo.” (25:67) Kula, kunywa, kulala na mambo mengine yote yanatakiwa kuwa kati na kati. Yana mipaka na kipomo chake. Yanapozidi inakuwa ni madhara kwa mwanaadamu.

Miongoni mwa adabu za kula na kunywa ni mtu kutokula sana na khaswa mfungaji. Asile na kunywa sana kwa kiasi cha kwamba akajaza tumbo lake mpaka akawa na uzito wa kumuabudu Allaah na khaswa katika Ramadhaan. Kula na kunywa sana kunamzuia mtu kufanya ´ibaadah. Kunamfanya mtu kuwa mzembe wakati wa ´ibaadah. Ale na kunywa kwa kiasi cha kuwa sawa kwenye mgongo na kumuabudu Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kama ukilazimika kula hakikisha theluthi moja ya tumbo lako unaijaza chakula, theluthi moja maji na acha theluthi moja kwa ajili ya hewa.”

Bi maana kiasi kidogo cha kumfanya awe sawasawa. Mtu anatakiwa kuwa kati na kati kimaumbile na kidini. Asiwe kama mnyama asiyekuwa na hamu nyingine zaidi ya kula na kunywa. Hali kadhalika kulala. Kunasababisha mwanaadamu kukosa manufaa yake mengi katika Dini na dunia yake.

Chakula kidogo ni chenye manufaa kwa njia ya matibabu. Kama jinsi kinavyonufaisha ´ibaadah, kadhalika afya. Maradhi mengi yanatokamana na kula na kunywa sana na maakulati mbali mbali. Kwa ajili hiyo huwa inasemwa huenda mlo mmoja ukazuia milo mingi huko mbeleni. Mtu anatakiwa kuwa mkati na kati. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ
“Na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.” (07:31)

وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا
“Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo.” (25:67)

Kula, kunywa, kulala na mambo mengine yote yanatakiwa kuwa kati na kati. Yana mipaka na kipomo chake. Yanapozidi inakuwa ni madhara kwa mwanaadamu.