Bunge Sio Mashauriano Ya Kiislamu

Lau punda ingeliweza kuzungumza basi ingelitoa maoni yake. Kuna tofauti kati ya bunge na mashauriano, Shuaraa´. Upande wa kwanza mashauriano, Shuuraa´, yanafanywa na wanachuoni wenye busara na watawala. Upande wa pili, bunge inakuwa na waombaji ambao hamu yao kubwa ni kupata uongozi, wamiliki wa migahawa bali mpaka wanawake ambao na wao [wanataka] kufikisha mapendekezo yao na wanayofikiri. Je, huu ni Uislamu? Kama ni kweli kuwa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Ibn 'Uthaymiyn wanajuzisha hilo, hivyo mimi nawapinga na kuwakataza. Hata hivyo, kosa lolote linafutwa na wema wao. Kadhalika wanapewa udhuru kwa kuwa wametiwa mchanga wa machoni. Himdi zote ni Zake Allaah kwa vile Ahl-us-Sunnah hawafuati kichwa mchunga. Sisi sio kama mshairi alivosema: Kama mfano wa ng'ombe kipofu anayeongozwa na mchungaji kipofu kwenye njia iliyopinda Tunajisalimisha kwa Allaah na si kwa watu: وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا "Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: “Laiti ningechukua pamoja na Rasuli njia. Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki khalili (mwandani).” Kwa yakini amenipoteza mbali na dhikri (ukumbusho na mawaidha) baada ya kunijia.” Na shaytwaan daima kwa insani ni mwenye kusaliti." (25:27-29) Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy Chanzo: Naswaaih wa Fadhwaaih, uk. 137 Toleo la: 15-12-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Lau punda ingeliweza kuzungumza basi ingelitoa maoni yake. Kuna tofauti kati ya bunge na mashauriano, Shuaraa´.

Upande wa kwanza mashauriano, Shuuraa´, yanafanywa na wanachuoni wenye busara na watawala.

Upande wa pili, bunge inakuwa na waombaji ambao hamu yao kubwa ni kupata uongozi, wamiliki wa migahawa bali mpaka wanawake ambao na wao [wanataka] kufikisha mapendekezo yao na wanayofikiri. Je, huu ni Uislamu?

Kama ni kweli kuwa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn wanajuzisha hilo, hivyo mimi nawapinga na kuwakataza. Hata hivyo, kosa lolote linafutwa na wema wao. Kadhalika wanapewa udhuru kwa kuwa wametiwa mchanga wa machoni. Himdi zote ni Zake Allaah kwa vile Ahl-us-Sunnah hawafuati kichwa mchunga. Sisi sio kama mshairi alivosema:

Kama mfano wa ng’ombe kipofu anayeongozwa na mchungaji kipofu
kwenye njia iliyopinda

Tunajisalimisha kwa Allaah na si kwa watu:

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا
“Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: “Laiti ningechukua pamoja na Rasuli njia. Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki khalili (mwandani).” Kwa yakini amenipoteza mbali na dhikri (ukumbusho na mawaidha) baada ya kunijia.” Na shaytwaan daima kwa insani ni mwenye kusaliti.” (25:27-29)

Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Chanzo: Naswaaih wa Fadhwaaih, uk. 137
Toleo la: 15-12-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Kukufurisha na Kuhukumu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 15th, December 2014