Baadhi Ya Fadhila Za ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu)

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “kisha ´Uthmaan... “, wa tatu katika ubora ni ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye ni miongoni mwa mwa wale waliotangulia mwanzoni katika Uislamu na akahijiri Hijrah mbili; alihijiri kwenda Habashah na Madiynah. Vilevile akatoa mapesa katika njia ya Allaah (´Azza wa Jalla) na akawachimbia Waislamu visima. Alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni nani atakayechimba visima hivi na yeye atakuwa na Pepo.” ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ndiye akafanya hivyo kwa ajili ya kuwafanyia Waislamu. Akatayarisha jeshi la ´Usrah kikamilifu kwa mali yake. Yeye ndiye ambaye alichukua uongozi baada ya ´Umar kwa Ijmaa´ ya Maswahabah waliofanya mashauriano ambao walipa ahadi kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu). Wakampa bay´ah wao na Waislamu pia wakampa bay´ah. Isitoshe ni mume wa msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ruqayyah na Umm Kulthuum. Kwa ajili hiyo ndio maana akaitwa Dhun an-Nuurayn, kwa kuwa alioa wasichana wawili wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma Makkah kujadiliana na washirikina, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfanyia bay´ah yeye (´Uthmaan) kwa mkono wake (mwenyewe Mtume). Akasema: “Huu ni wa ´Uthmaan.” Bay´ah ikawa imetimia ilihali hayupo, kwa kuwa alikuwa Makkah. Yeye vilevile ndiye ambaye ameandika Muswhaf al-Imaam – unaoitwa msahafu wa ´Uthmaan – kwa sura (muundo, mchoro) wa ´Uthmaan. Na ndio msahafu ambao tunatumia hivi leo. Fadhila zake ni nyingi (Radhiya Allaahu ´anhu). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 119-120

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “kisha ´Uthmaan… “, wa tatu katika ubora ni ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye ni miongoni mwa mwa wale waliotangulia mwanzoni katika Uislamu na akahijiri Hijrah mbili; alihijiri kwenda Habashah na Madiynah. Vilevile akatoa mapesa katika njia ya Allaah (´Azza wa Jalla) na akawachimbia Waislamu visima. Alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ni nani atakayechimba visima hivi na yeye atakuwa na Pepo.”

´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ndiye akafanya hivyo kwa ajili ya kuwafanyia Waislamu. Akatayarisha jeshi la ´Usrah kikamilifu kwa mali yake. Yeye ndiye ambaye alichukua uongozi baada ya ´Umar kwa Ijmaa´ ya Maswahabah waliofanya mashauriano ambao walipa ahadi kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu). Wakampa bay´ah wao na Waislamu pia wakampa bay´ah. Isitoshe ni mume wa msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ruqayyah na Umm Kulthuum. Kwa ajili hiyo ndio maana akaitwa Dhun an-Nuurayn, kwa kuwa alioa wasichana wawili wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomtuma Makkah kujadiliana na washirikina, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfanyia bay´ah yeye (´Uthmaan) kwa mkono wake (mwenyewe Mtume). Akasema:

“Huu ni wa ´Uthmaan.”

Bay´ah ikawa imetimia ilihali hayupo, kwa kuwa alikuwa Makkah.

Yeye vilevile ndiye ambaye ameandika Muswhaf al-Imaam – unaoitwa msahafu wa ´Uthmaan – kwa sura (muundo, mchoro) wa ´Uthmaan. Na ndio msahafu ambao tunatumia hivi leo. Fadhila zake ni nyingi (Radhiya Allaahu ´anhu).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 119-120


  • Kitengo: Uncategorized , Maswahabah wa kiume
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014