Baadhi Ya Fadhila Za ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu)

Baada yake - yaani baada ya Abu Bakr kwa ubora- ni ´Umar-ul-Faaruq (Radhiya Allaahu ´anhu). Ameitwa al-Faaruq (mfarikishaji), kwa kuwa Allaah Amefarikisha kupitia kwake baina ya haki na batili. Wakati aliposilimu Uislamu ulipata utukufu kutokana na Uislamu wake. Kabla ya kusilimu Hamzah na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) Waislamu walikuwa wadhaifu na wenye kujificha katika Daar-ul-Arqam. Wakati aliposilimu Hamzah na ´Umrah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wakatoka pamoja kwenda katika Masjid-ul-Haraam. Hakuna yeyote ambaye alikuwa anawasogelea Hamzah na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Hapo ndipo Uislamu ulipata utukufu kwa watu hawa wawili. Akasema Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu): “Hatukuacha kupata utukufu tangu aliposilimu ´Umar.” Allaah Akaupa utukufu Uislamu kwa kupitia ´Umar. Kwa ajili hiyo ndio maana akaitwa al-Faaruq. Yeye ndio Khaliyfah wa pili na ndio Swahabah bora baada ya Abu Bakr asw-Swiddiyq kama ilivokuja katika al-Bukhaariy na vinginevyo. Hawa wawili ndio mawaziri wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), yaani wenye kushauriana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 118-119

Baada yake – yaani baada ya Abu Bakr kwa ubora- ni ´Umar-ul-Faaruq (Radhiya Allaahu ´anhu). Ameitwa al-Faaruq (mfarikishaji), kwa kuwa Allaah Amefarikisha kupitia kwake baina ya haki na batili. Wakati aliposilimu Uislamu ulipata utukufu kutokana na Uislamu wake. Kabla ya kusilimu Hamzah na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) Waislamu walikuwa wadhaifu na wenye kujificha katika Daar-ul-Arqam. Wakati aliposilimu Hamzah na ´Umrah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wakatoka pamoja kwenda katika Masjid-ul-Haraam. Hakuna yeyote ambaye alikuwa anawasogelea Hamzah na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Hapo ndipo Uislamu ulipata utukufu kwa watu hawa wawili. Akasema Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Hatukuacha kupata utukufu tangu aliposilimu ´Umar.”

Allaah Akaupa utukufu Uislamu kwa kupitia ´Umar. Kwa ajili hiyo ndio maana akaitwa al-Faaruq. Yeye ndio Khaliyfah wa pili na ndio Swahabah bora baada ya Abu Bakr asw-Swiddiyq kama ilivokuja katika al-Bukhaariy na vinginevyo. Hawa wawili ndio mawaziri wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), yaani wenye kushauriana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 118-119


  • Kitengo: Uncategorized , Maswahabah wa kiume
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014