Baadhi Ya Fadhila Za ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu)

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “Wanne wao mbora wa viumbe baada yao ´Aliy anayeshiriki katika ubora”, kisha baada yao katika ubora ni ´Aliy bin Abiy Twaalib, ambaye ni kiongozi wa waumini, mtoto wa ami ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mume wa msichana wake Faatwimah ambaye alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Je, huridhii kuwa na manzilah kwangu kama manzilah alokuwa nayo Haaruun kwa Muusa, isipokuwa tu hakuna Nabii baada yangu?” Hapa ilikuwa katika vita vya Tabuk wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipompa uongozi Madiynah, hakuamini kumfanya yeye kuwa kiongozi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkinaisha na kumwambia: “Wewe manzilah yako kwangu ni kama manzilah ya Haaruun kwa Muusa.” Kwa kuwa Muusa alipoenda katika miadi ya Mola Wake, alimpa (alimuachia) uongozi Haaruun. Alimwambia: اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي “Shika mahali pangu katika (kuwasimamia) watu wangu.” (al-A´raaf:142) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa (alimuachia) uongozi ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) baada yake katika janga hili, hakufanya hivyo kwa sababu ya kwamba yeye ndiye kiongozi baada ya kufa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kama wanavosema Raafidhwah – bali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati alipoenda katika (vita vya) Tabuk kama mfano wa Muusa alivofanya kwa Haaruun (´alayhimas-Salaam) pindi alipoenda katika miadi ya Mola Wake. Anasema (Ta´ala): وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ “Muwsa akamwambia ndugu yake Haaruwn: “Shika mahali pangu katika (kuwasimamia) watu wangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.” (al-A´raaf:142) Hizi ni katika fadhila zake (Radhiya Allaahu ´anhu). Vilevile yeye ndiye aliwapiga vita Khawaarij na akazima fitina yao na Waislamu wakastareheka na shari yao. Ikahakikika kwake bishara ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa yule atakayewaua. Ana fadhila nyingi. Isitoshe, ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) ndiye wa kwanza katika vijana huru waliosilimu. Na wa kwanza katika wanaume huru aliyesilimu ni Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhu). Na wa kwanza katika watawaliwa (mtumwa aliyeachwa huru) wanaume aliyesilimu ni Zayd bin Haarith (Radhiya Allaahu ´anhu). Na wa kwanza katika watumwa kusilimu ni Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu ´anhu). Na wa kwanza katika wanawake kusilimu ni Khadiyjah bint Khuwaylid (Radhiya Allaahu ´anha). ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) ni katika wale waliotangulia mwanzo katika Uislamu, na mke wake msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Faatwimah, na Hasan bin ´Aliy na Husayn bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambao ni viongozi wa vijana Peponi. Ana fadhila nyingi. Vilevile yeye ndiye ambaye alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yake siku ya Khaybar: “Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Allaah na Mtume Wake kama jinsi Allaah pia na Mtume Wake wanampenda.” Maswahabah wote wakawa na shauku kila mmoja anataka kumjua mtu huyu ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa anampenda Allaah na Mtume Wake na Allaah na Mtume Wake pia wanampenda. Ikawa ni ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu). Hizi ni katika fadhila zake kuu na Allaah Awawie radhi wote. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 120-122

Kauli ya mwandishi (Rahimahu Allaah) “Wanne wao mbora wa viumbe baada yao ´Aliy anayeshiriki katika ubora”, kisha baada yao katika ubora ni ´Aliy bin Abiy Twaalib, ambaye ni kiongozi wa waumini, mtoto wa ami ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mume wa msichana wake Faatwimah ambaye alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, huridhii kuwa na manzilah kwangu kama manzilah alokuwa nayo Haaruun kwa Muusa, isipokuwa tu hakuna Nabii baada yangu?”

Hapa ilikuwa katika vita vya Tabuk wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipompa uongozi Madiynah, hakuamini kumfanya yeye kuwa kiongozi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkinaisha na kumwambia:

“Wewe manzilah yako kwangu ni kama manzilah ya Haaruun kwa Muusa.”

Kwa kuwa Muusa alipoenda katika miadi ya Mola Wake, alimpa (alimuachia) uongozi Haaruun. Alimwambia:

اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي
“Shika mahali pangu katika (kuwasimamia) watu wangu.” (al-A´raaf:142)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa (alimuachia) uongozi ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) baada yake katika janga hili, hakufanya hivyo kwa sababu ya kwamba yeye ndiye kiongozi baada ya kufa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kama wanavosema Raafidhwah – bali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati alipoenda katika (vita vya) Tabuk kama mfano wa Muusa alivofanya kwa Haaruun (´alayhimas-Salaam) pindi alipoenda katika miadi ya Mola Wake. Anasema (Ta´ala):

وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ
“Muwsa akamwambia ndugu yake Haaruwn: “Shika mahali pangu katika (kuwasimamia) watu wangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.” (al-A´raaf:142)

Hizi ni katika fadhila zake (Radhiya Allaahu ´anhu).

Vilevile yeye ndiye aliwapiga vita Khawaarij na akazima fitina yao na Waislamu wakastareheka na shari yao. Ikahakikika kwake bishara ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa yule atakayewaua. Ana fadhila nyingi.

Isitoshe, ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) ndiye wa kwanza katika vijana huru waliosilimu. Na wa kwanza katika wanaume huru aliyesilimu ni Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhu). Na wa kwanza katika watawaliwa (mtumwa aliyeachwa huru) wanaume aliyesilimu ni Zayd bin Haarith (Radhiya Allaahu ´anhu). Na wa kwanza katika watumwa kusilimu ni Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu ´anhu). Na wa kwanza katika wanawake kusilimu ni Khadiyjah bint Khuwaylid (Radhiya Allaahu ´anha).

´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) ni katika wale waliotangulia mwanzo katika Uislamu, na mke wake msichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Faatwimah, na Hasan bin ´Aliy na Husayn bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambao ni viongozi wa vijana Peponi. Ana fadhila nyingi.

Vilevile yeye ndiye ambaye alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yake siku ya Khaybar:

“Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Allaah na Mtume Wake kama jinsi Allaah pia na Mtume Wake wanampenda.”

Maswahabah wote wakawa na shauku kila mmoja anataka kumjua mtu huyu ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa anampenda Allaah na Mtume Wake na Allaah na Mtume Wake pia wanampenda. Ikawa ni ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu). Hizi ni katika fadhila zake kuu na Allaah Awawie radhi wote.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 120-122


  • Kitengo: Uncategorized , Maswahabah wa kiume
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014