´Ashaa´irah Kwamba Qur-aan Imechukuliwa Kutoka Kwenye Lawh al-Mahfuudhw

Ama Ashaa´irah wanasema kwamba imeandikwa katika Lawh al-Mahfuudhw na kwamba Jibriyl aliichukua kutoka kwenye Lawh al-Hafuudhw na akaiteremsha kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ni kauli batili. Jibriyl hakuichukua kutoka katika Lawh al-Mahfuudhw, bali ameichukua kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Ni kweli kwamba imeandikwa katika Lawh al-Mahfuudh. Anasema (Ta´ala): بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ ”Bali hii ni Qur-aan tukufu. (Iliyoko) Katika Lawhim-Mahfuudhw (ubao Uliohifadhiwa).” (al-Buruuj:21-22) وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ “Na hakika hii (Qur-aan) iko katika Mama wa Kitabu Kwetu, (Lawhim-Mahfuudhw) bila shaka ni yenye shani ya juu (kimetukuka), yenye hikmah.” (az-Zukhruf:04) yaani Qur-aan. Imeandikwa katika Lawh al-Mahfuudhw bila ya shaka yoyote. Lakini hata hivyo Ibriyl haikuichukua kutoka kwenye Lawh al-Mahfuudhw – kama wanavyosema Ashaa´irah – bali ameichukua kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Inatakiwa kujua haya. Kwa kuwa haya yametajwa katika I´tiqaad za Ashaa´irah. Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) ameradi kauli hii katika kitabu kilichochapishwa - kiko vilevile pamoja na Fataawaa zake – kitabu hicho kinaitwa “Jawaab-ul-Waadhwih al-Mustaqiym fiy kayfiyyatun-un-Nuzuul al-Qur-aan al-´Adhwiym”. Ameraddi kauli hii na kuibatilisha. Kwa kuwa kusema kwamba ameichukua kutoka kwenye Lawh al-Mahfuudhw ni njia inayopelekea kusema kwamba imeumbwa. Bi maana Allaah Ameiumba kwenye Lawh al-Mahfuudhw – kama wanavyosema Jahmiyyah. Hili limechukuliwa kutoka kwa Jahmiyyah. Ni kauli batili. Ni wajibu kuitanabahisha. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 68-69

Ama Ashaa´irah wanasema kwamba imeandikwa katika Lawh al-Mahfuudhw na kwamba Jibriyl aliichukua kutoka kwenye Lawh al-Hafuudhw na akaiteremsha kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ni kauli batili. Jibriyl hakuichukua kutoka katika Lawh al-Mahfuudhw, bali ameichukua kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Ni kweli kwamba imeandikwa katika Lawh al-Mahfuudh. Anasema (Ta´ala):

بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ
”Bali hii ni Qur-aan tukufu. (Iliyoko) Katika Lawhim-Mahfuudhw (ubao Uliohifadhiwa).” (al-Buruuj:21-22)

وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ
“Na hakika hii (Qur-aan) iko katika Mama wa Kitabu Kwetu, (Lawhim-Mahfuudhw) bila shaka ni yenye shani ya juu (kimetukuka), yenye hikmah.” (az-Zukhruf:04)

yaani Qur-aan. Imeandikwa katika Lawh al-Mahfuudhw bila ya shaka yoyote. Lakini hata hivyo Ibriyl haikuichukua kutoka kwenye Lawh al-Mahfuudhw – kama wanavyosema Ashaa´irah – bali ameichukua kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Inatakiwa kujua haya. Kwa kuwa haya yametajwa katika I´tiqaad za Ashaa´irah.

Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) ameradi kauli hii katika kitabu kilichochapishwa – kiko vilevile pamoja na Fataawaa zake – kitabu hicho kinaitwa “Jawaab-ul-Waadhwih al-Mustaqiym fiy kayfiyyatun-un-Nuzuul al-Qur-aan al-´Adhwiym”. Ameraddi kauli hii na kuibatilisha. Kwa kuwa kusema kwamba ameichukua kutoka kwenye Lawh al-Mahfuudhw ni njia inayopelekea kusema kwamba imeumbwa. Bi maana Allaah Ameiumba kwenye Lawh al-Mahfuudhw – kama wanavyosema Jahmiyyah. Hili limechukuliwa kutoka kwa Jahmiyyah. Ni kauli batili. Ni wajibu kuitanabahisha.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 68-69


  • Kitengo: Uncategorized , Ashaa´irah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 13th, February 2014