Asali Inasahilisha Kuongea Kwa Mtoto

Ikiwa mtoto ameanza kuongea kwa ufaswaha na mtu akataka kusahilisha maneno yao, mtu anatakiwa kupaka ndimi zao asali na chumvi ya andraaniy[1]. Vitu hivi viwili vinachangia katika ule uzito wa ulimi unaozuia maneno kuondoka. Wakati wanapoweza kuongea mambo, mtu anatakiwa kuwafanya waweze kutamka "Laa ilaaha illa Allaah, Muhammad Rasuulullaah". Wafanye masikio yao kwanza yaweze kusikia elimu kuhusu Allaah (Subhaanahu) na upwekeshaji Wake na kwamba Yuko juu ya ´Arshi Yake na kwamba Anawaona na Kusikia wanayoyasema na kwamba Yuko pamoja nao popote walipo. Wana wa Israel walikuwa mara nyingi wakiwapa watoto wao jina la "Emanuel". Maana yake ni kuwa "Mungu Wetu yuko pamoja na sisi." Ndio maana majina yanayopendwa zaidi na Allaah ni ´Abdullaah na ´Abdur-Rahmaan kwa njia ya kwamba pale ambapo mtoto atakaposikia na kufahamu, aonelee kuwa yeye ni mja wa Allaah na kwamba Allaah ndiye Mola na Mlinzi Wake. ---------------------- (1) Kiarabu. al-Milh al-Andraaniy.

Ikiwa mtoto ameanza kuongea kwa ufaswaha na mtu akataka kusahilisha maneno yao, mtu anatakiwa kupaka ndimi zao asali na chumvi ya andraaniy[1]. Vitu hivi viwili vinachangia katika ule uzito wa ulimi unaozuia maneno kuondoka.

Wakati wanapoweza kuongea mambo, mtu anatakiwa kuwafanya waweze kutamka “Laa ilaaha illa Allaah, Muhammad Rasuulullaah”. Wafanye masikio yao kwanza yaweze kusikia elimu kuhusu Allaah (Subhaanahu) na upwekeshaji Wake na kwamba Yuko juu ya ´Arshi Yake na kwamba Anawaona na Kusikia wanayoyasema na kwamba Yuko pamoja nao popote walipo.

Wana wa Israel walikuwa mara nyingi wakiwapa watoto wao jina la “Emanuel”. Maana yake ni kuwa “Mungu Wetu yuko pamoja na sisi.” Ndio maana majina yanayopendwa zaidi na Allaah ni ´Abdullaah na ´Abdur-Rahmaan kwa njia ya kwamba pale ambapo mtoto atakaposikia na kufahamu, aonelee kuwa yeye ni mja wa Allaah na kwamba Allaah ndiye Mola na Mlinzi Wake.

———————-
(1) Kiarabu. al-Milh al-Andraaniy.


  • Author: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah (d. 751). Tuhfat-ul-Mawduud bi Ahkaam-il-Mawluud, uk. 234
  • Kitengo: Uncategorized , Familia
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 7th, January 2014