as-Suyuutwiy Asemae Maadhimisho Ya Maulidi Ni Bid´ah Nzuri

Kuhusiana na nukuu ya ar-Rifaa'iy ya as-Suyuutwiy ambaye kasema: "Maulidi ni katika Bid´ah nzuri ambayo mtu hupewa thawabu juu yake." maneno ya as-Suyuutwiy yanaradiwa na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): "Na shari ya mambo ni [mambo] ya kuzua." na: "Kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni." na: "Yule ambaye atafanya ´amali isiyokuwa humo na mri yetu atarudishiwa mwenyewe." Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kaeleza Bid´ah kuwa ovu na upotofu. Sifa hizi ni mbaya na zimekatazwa. Yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kaeleza pia kwamba matendo yao yanatupiliwa mbali na kwamba yanaingia Motoni. Hii ni dalili ioneshayo ya kwamba mtu wa Bid´ah hapewi ujira kwa Bid´ah yake. Badala yake, kuna khatari ya kupata mtihani na adhabu chungu. Allaah (Ta´ala) Kasema: فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ “Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.” (24:63) Aidha, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni." Mtu anapewa ujira tu wakati anamfuata Mjumbe (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na kuipa kipaumbele uongofu wake kabla ya kila kitu kingine. Allaah (Ta´ala) Kasema: قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ”Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufiria - Mwenye kurehemu).” (03:31) فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ”Basi mwaminini Allaah na Mtume Wake, an-Nabiyyi al-Ummiyy (Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye anamwamini Allaah na Maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka.” (07:158) Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Kafanya watu kupata sehemu ya mapenzi Yake, uongofu Wake na msamaha Wake ikiwa tu watamchukua Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kama mfano mzuri wa kuigwa. Maadhimisho ya Maulidi sio katika uongofu wala Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Ni katika uongofu na Sunnah ya mtawala Irbil na aliishi takriban miaka 600 baada ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Mwandishi: 'Allaamah Hamuud bin 'Abdillaah at-Tuwayjiriy ar-Radd al-Qawiy, uk. 29

Kuhusiana na nukuu ya ar-Rifaa’iy ya as-Suyuutwiy ambaye kasema:

“Maulidi ni katika Bid´ah nzuri ambayo mtu hupewa thawabu juu yake.”

maneno ya as-Suyuutwiy yanaradiwa na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Na shari ya mambo ni [mambo] ya kuzua.”

na:

“Kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni.”

na:

“Yule ambaye atafanya ´amali isiyokuwa humo na mri yetu atarudishiwa mwenyewe.”

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kaeleza Bid´ah kuwa ovu na upotofu. Sifa hizi ni mbaya na zimekatazwa. Yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kaeleza pia kwamba matendo yao yanatupiliwa mbali na kwamba yanaingia Motoni. Hii ni dalili ioneshayo ya kwamba mtu wa Bid´ah hapewi ujira kwa Bid´ah yake. Badala yake, kuna khatari ya kupata mtihani na adhabu chungu. Allaah (Ta´ala) Kasema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.” (24:63)

Aidha, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Kila Bid´ah ni upotofu, na kila upotofu ni Motoni.”

Mtu anapewa ujira tu wakati anamfuata Mjumbe (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kuipa kipaumbele uongofu wake kabla ya kila kitu kingine. Allaah (Ta´ala) Kasema:

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufiria – Mwenye kurehemu).” (03:31)

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
”Basi mwaminini Allaah na Mtume Wake, an-Nabiyyi al-Ummiyy (Mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye anamwamini Allaah na Maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuongoka.” (07:158)

Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Kafanya watu kupata sehemu ya mapenzi Yake, uongofu Wake na msamaha Wake ikiwa tu watamchukua Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kama mfano mzuri wa kuigwa. Maadhimisho ya Maulidi sio katika uongofu wala Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Ni katika uongofu na Sunnah ya mtawala Irbil na aliishi takriban miaka 600 baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Mwandishi: ‘Allaamah Hamuud bin ‘Abdillaah at-Tuwayjiriy
ar-Radd al-Qawiy, uk. 29


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013