as-Suhaymiy Kuhusu Ugomvi Wa ´Aliy al-Halabiy Na al-Lajnah ad-Daaimah

Wenye haki ni al-Lajnah ad-Daaimah. ´Aliy [bin] Hassan katika qadhiya hii alichanganya mambo. Alikosea kuipiga Radd al-Lajnah. Kwa kuwa hakuyafahamu maneno ya al-Lajnah, kamwe. Alikosea kuipiga Radd al-Lajnah. Alikosea na kaidhulumu nafsi yake. Kafungua njia ya kuikashifu al-Lajnah bila ya kujua. Kafanya kosa, kafanya kosa, kafanya kosa, kosa mara elfu. Yuko na msemo ambao wanaingia humo Murji-ah. Yuko na msemo ambao kunakhofiwa kuutumia Murji-ah. Mfano kwa kusema kwake wakati fulani kuwa kuna kufuru ya matendo na I´tiqaad na mtu hakufuru ila akianguka tu katika kufuru ya I´tiqaad. Hili si sahihi. Hata Shaykh wake, Shaykh [Muhammad] Naaswir-ud-Diyn [al-Albaaniy] pamoja na fadhila zake na hadhi yake, hatukubaliani naye katika qadhiya hii. Kuna kufuru ya matendo ambayo inamtoa mtu katika Uilsamu. Kama kumtukana Allaah na Mtume Wake, kusujudia sanamu, kuikejeli Sunnah. Yote haya ni kufuru inayomtoa mtu katika Uislamu.

Wenye haki ni al-Lajnah ad-Daaimah. ´Aliy [bin] Hassan katika qadhiya hii alichanganya mambo. Alikosea kuipiga Radd al-Lajnah. Kwa kuwa hakuyafahamu maneno ya al-Lajnah, kamwe. Alikosea kuipiga Radd al-Lajnah. Alikosea na kaidhulumu nafsi yake. Kafungua njia ya kuikashifu al-Lajnah bila ya kujua. Kafanya kosa, kafanya kosa, kafanya kosa, kosa mara elfu.

Yuko na msemo ambao wanaingia humo Murji-ah. Yuko na msemo ambao kunakhofiwa kuutumia Murji-ah. Mfano kwa kusema kwake wakati fulani kuwa kuna kufuru ya matendo na I´tiqaad na mtu hakufuru ila akianguka tu katika kufuru ya I´tiqaad. Hili si sahihi. Hata Shaykh wake, Shaykh [Muhammad] Naaswir-ud-Diyn [al-Albaaniy] pamoja na fadhila zake na hadhi yake, hatukubaliani naye katika qadhiya hii. Kuna kufuru ya matendo ambayo inamtoa mtu katika Uilsamu. Kama kumtukana Allaah na Mtume Wake, kusujudia sanamu, kuikejeli Sunnah. Yote haya ni kufuru inayomtoa mtu katika Uislamu.