´Aqiydah Ya Salafiyyah

Kwa kitu gani mtu atajitakasa kwacho? Kwanza mtu ajitakase kutoka katika Shirki kwa nisba ya uhusiano wake na Allaah. Mtu amuabudu Allaah kwa Ikhlaasw (akimtakasia Allaah ´Ibaadah). Mtu asimuabudu Allaah kwa Riyaa, kwa ajili ya kutafuta sifa, nafasi au uraisi. Afanye yote haya lengo liwe moja tu iwe ni thawabu kwa Allaah na Pepo. Mtu anatakiwa pia kujitakasa kwa kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ina maana mtu asifanye Bid´ah katika Shari´ah yake. Si kwa (Bid´ah) ndogo wala kubwa, siyo katika ´Aqiydah, maneno wala vitendo. Kujitakasa kwa nisba ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nako ni kumfuata bila kufanya Bid´ah, mtu asiegamie kwengine ila kwenye njia ya Salafiyyah ambayo ni njia ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ambao wanaamini kwa kila Alichojisifia Allaah mwenyewe katika Kitabu Chake au kupitia maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika njia (mafunzo) ya Salafiyyah. Ambao hawafanyi Bid´ah katika ´Ibaadah si katika kauli wala matendo. Unaona wanafuata yale yaliyokuja katika Shari´ah. Kinyume na wayafanyayo baadhi ya watu wa Bid´ah katika Adhkaar za Bid´ah, kama wafanyavyo baadhi ya watu wa kupanga, miongoni mwa Suufiyyah na wengineo.