´Aqiydah Ya Khawaarij Na Mu´tazilah – Muislamu Atayeingia Motoni Hatoki Kamwe

Anasema Allaah (´Azza wa Jalla): مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ “Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa (Moto wa) Jahiym.” (09:113) Vipi itajulikana kuwa mtu ni katika watu wa Motoni? Ni wakati atapokufa juu ya kufuru kubwa, Shirki kubwa, unafiki mkubwa, Ilhaad inayomtoa mtu katika Uislamu, yote haya ni mambo yako wazi kuwa mtu amekufa juu ya kufuru na kwa ajili hiyo mtu asimwombee Muislamu huyu. Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuamini Shafaa´ah, uombezi. Dalili katika Qur-aan: وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ “Na wala hawamuombei shafaa’ah (yeyote yule) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia. Nao kutokana na kumkhofu, ni wenye kutahadhari.” (21:28) Masharti ya uombezi: 1- Shari ya kwanza ni kuridhia kwa Allaah (´Azza wa Jalla) kwa muombezi aombee (yaani kutoa idhini). 2- Anayeombewa awe ni katika Waislamu. Huu ndio uombezi wenye kuthibitishwa. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameuamini na Mu´tazilah na Khawaarij wameupinga. Kwa kuwa wanaamini kwamba Muislamu mwenye kumuasi Allaah ataingia Motoni na mwenye kuingia Motoni hatotoka humo. Wanapinga uombezi, adhabu ya kaburi na neema zake juu ya kanuni hii ambayo wanaamini. Nayo si nyingine ni kwamba mwenye kufa hali ya kuwa ni mtenda madhambi ataingia Motoni, na mwenye kuingia Motoni hatotoka humo. Hii ndio ´Aqiydah ya mapote yaliyoangamia Mu´tazilah wakiwa pamoja na Khawaarij. Mwandishi: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn Ibn Qudaamah al-Maqdisiy Chanzo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=887&size=2h&ext=.rm

Anasema Allaah (´Azza wa Jalla):

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ
“Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa (Moto wa) Jahiym.” (09:113)

Vipi itajulikana kuwa mtu ni katika watu wa Motoni? Ni wakati atapokufa juu ya kufuru kubwa, Shirki kubwa, unafiki mkubwa, Ilhaad inayomtoa mtu katika Uislamu, yote haya ni mambo yako wazi kuwa mtu amekufa juu ya kufuru na kwa ajili hiyo mtu asimwombee Muislamu huyu.

Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuamini Shafaa´ah, uombezi. Dalili katika Qur-aan:

وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ
“Na wala hawamuombei shafaa’ah (yeyote yule) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia. Nao kutokana na kumkhofu, ni wenye kutahadhari.” (21:28)

Masharti ya uombezi:

1- Shari ya kwanza ni kuridhia kwa Allaah (´Azza wa Jalla) kwa muombezi aombee (yaani kutoa idhini).

2- Anayeombewa awe ni katika Waislamu.

Huu ndio uombezi wenye kuthibitishwa. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wameuamini na Mu´tazilah na Khawaarij wameupinga. Kwa kuwa wanaamini kwamba Muislamu mwenye kumuasi Allaah ataingia Motoni na mwenye kuingia Motoni hatotoka humo. Wanapinga uombezi, adhabu ya kaburi na neema zake juu ya kanuni hii ambayo wanaamini. Nayo si nyingine ni kwamba mwenye kufa hali ya kuwa ni mtenda madhambi ataingia Motoni, na mwenye kuingia Motoni hatotoka humo. Hii ndio ´Aqiydah ya mapote yaliyoangamia Mu´tazilah wakiwa pamoja na Khawaarij.

Mwandishi: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn Ibn Qudaamah al-Maqdisiy
Chanzo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=887&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Khawaarij
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 3rd, April 2014