´Aqiydah Ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah Juu Ya Qadar

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakawa kati na kati. Wanasema kila kitu kinakuwa kwa Matakwa na Utashi wa Allaah kukiwemo matendo ya waja. Yameumbwa na Allaah na wakati huo huo ni matendo ya mja (aloyafanya) kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe. Kwa kuwa mja ana matakwa na utashi wake. Lakini hata hivyo hayajitoshelezi na Allaah – kama wanavosema Qadariyyah – na hakutenzwa nguvu – kama wanavosema Jabriyyah – bali yeye anafanya matendo kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe. Kwa ajili hiyo ndio maana akapewa thawabu kwa kutenda kheri na kuadhibiwa kwa kutenda uovu. Kwa kuwa ametenda kwa kutaka na kupenda kwake mwenyewe. Lau angelikuwa ametenzwa nguvu asingeliadhibiwa, vipi ataadhibiwa kwa kitu ambacho hakukifanya kwa khiyari yake na kutaka kwake mwenyewe? Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah (Jalla wa ´Alaa) Hamuadhibu mwendawazimu ambaye hafanyi kwa kutaka kwake, hamuadhibu vilevile mtu mwenye kutenzwa nguvu ambaye anafanya si kwa khiyari yake, wala hamuadhibu mwenye kulala ambaye hana mawazo wala akili. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Kalamu imesimamishwa kwa watu (aina) tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.” Kwa nini? Kwa kuwa watu hawa hawana matakwa wala utashi ndio maana wakawa hawaadhibiwi kwa waliyoyatenda wakati ambapo akili yao imepotea na utashi wao. Ama yule mwenye matakwa, utashi na khiyari, anapewa thawabu kwa kutenda mambo ya kheri na anaadhibiwa kwa kutenda maasi. Kwa kuwa ameyafanya kwa khiyari yake na kutaka kwake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ “Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema.” (al-Baqarah:277) “...wakatenda mema”, ameyanasibisha matendo kwao. Anasema: إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا “Hakika wale waliokufuru.” (al-Baqarah:06) Ameinasibisha kufuru kwao. Kwa kuwa ni kutokana na kitendo chao na kutaka kwao. Akasema tena: وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ “Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam.” (al-Jinn:23) Ameyanasibisha maasi kwao. Kwa kuwa ni kutoka na matendo yao. Kwa njia ya kimatendo, ni kitendo cha mja. Ama kwa njia ya Qadar, kimekadiriwa na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ni Qadar ya Allaah na wakati huo huo ni kitendo cha mja kwa kujumuisha baina ya nususi mbili. Hili linatolewa dalili na Kauli Yake (Ta´ala): لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ “Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika njia ya haki). Na hamtotaka isipokuwa Atakaye Allaah Mola wa walimwengu.” (at-Takwiyr:28-29) Kauli Yake: لِمَن شَاءَ مِنكُمْ “Kwa yule atakaye miongoni mwenu.” hii ni Radd kwa Jabriyyah ambao wanapinga matakwa ya mja. Ni dalili inaonesha kuwa mja ananyooka kwa kutaka kwake mwenyewe. Kisha Akasema: وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ “Na hamtotaka isipokuwa Atakaye Allaah Mola wa walimwengu.” hii ni Radd kwa Qadariyyah ambao wanasema kwamba matendo ya mja ni yenye kujitosheleza na mja ndiye ameumba matendo yake. Aayah hii imeraddi mapote yote mawili. Vilevile Aayah inathibitisha madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, ya kwamba utiifu na maasi ni kitendo cha mja na wakati huo huo ni kutokana na Qadhwaa na Qadar ya Allaah. Amewakadiria nayo na wao wakayafanya kwa khiyari yao na kutaka kwao wenyewe na kupenda kwao wenyewe. Kwa ajili hiyo mtu mwenye akili anaweza – ukitoa aliyetenzwa nguvu – anaweza kufanya ´amali, anaweza kuacha kufanya ´amali. Anaweza kusimama akaswali, kutoa Swadaqah, kupigana Jihaad katika njia ya Allaah kama jinsi vilevile anaweza pia kuacha, anaweza kuacha kuswali, kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu, anaweza kuacha kupigana Jihaad katika njia ya Allaah. Anaacha yeye mwenyewe kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe. Anaweza yote mawili kufanya na kuacha. Anafanya uzinzi, kunywa pombe, kula Ribaa kwa khiyari yake kama jinsi akipenda pia anaweza akayaacha. Anaweza kuacha Ribaa, uzinzi na akaacha mambo ya haramu. Ni kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe anafanya haya. Hakuna asiyejua hili. Jabriyyah hawayatendei kazi maneno haya waliyosema katika kila kitu. Lau mtu atawafanyia uadui ima kwa kupiga mmoja wao au kuua mmoja wao, je si wataomba lipizo na kisasi? Kwa nini wataomba hili na wakati wanasema kwamba ametenzwa nguvu na hafanyi kwa khiyari yake? Huu ni mgongano. Vilevile isitoshe wao wanatafuta riziki na wanaoa, ingelikuwa (mtu ametenzwa nguvu) – kama wanavosema – kwa nini basi wanafanya vitendo hivi na wanatafuta kupatikana vitu visivyokuwepo?! Haya madhehebu khabithi (machafu) wao wenyewe hawatendei kazi hili katika maisha yao ya sasa. Kwa ajili hiyo ndio maana wanaomba kisasi, wanaoa na wanatafuta riziki. Hii ni kauli batili na tunaomba kinga kwa Allaah. Hii ndio natija ya kutegemea fikira, akili, maneno na maoni ya watu bila ya kurejea katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna mgongano wa kuamini Qadhwaa na Qadar na kufanya sababu. Wewe unatakiwa kuamini kwamba, Anayotaka Allaah huwa na ambayo Hakutaka hayakukuwa. Usipinge (kufanya) sababu. Unatakiwa kutafuta riziki, uoe, utafute biashara, utawanyike katika ardhi na kutafuta fadhila (riziki) za Allaah. Usiseme kuwa unategemea Qadhwaa na Qadar na kwamba ikiwa nimeshakadiriwa kitu kitanijia tu na kama sikukadiriwa hakitonijia. Hili halisemwi na mtu wa akili. Hata ndege na wanyama – kwa maumbile yake – inaenda kutafuta riziki. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Lau mgelikuwa mnamtegemea Allaah ukweli wa kumtegemea, basi Angelikuruzukuni kama Anavomruzuku ndege. Inaruka hali ya kuwa haina kitu tumboni na inarudi imejaa tumbo (imeshiba).” Hata ndege inafanya sababu inaruka na kwenda kutafuta riziki. Kwa hivyo hakuna mgongano baina ya kuamini Qadhwaa na Qadar na kufanya sababu. Wanaosema hivi ni Jabriyyah. Hata hivyo, kufanya sababu hakujitoshelezi kuleta natija. Msababishaji ni Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hii ni Radd kwa Qadariyyah. Hatupetuki katika kuthibitisha sababu kama wafanyavyo Qadariyyah kama jinsi vilevile hatupetuki katika kuikanusha kama wafanyavyo Jabriyyah. Kufanya sababu ni jambo ambalo linatakikana. Anasema (Ta´ala): فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ “Basi tafuteni riziki kwa Allaah.” (al-´Ankabuut:17) وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ “Na tafuteni katika fadhila za Allaah.” (al-Jumu´ah:10) Allaah Ametuamrisha Swalah, Swawm na mambo mbali mbali ya utiifu. Huku ni katika kufanya sababu. Vilevile Ametukataza kufanya sababu za shari (ovu), kufuru, maasi na ufusaki. Hivyo, haina maana kuamini Qadhwaa na Qadar ukafika unapinga kufanya sababu. Bali unatakiwa kufanya sababu pamoja na kuamini ya kwamba ikiwa Allaah Amekuandikia (kukipata au kukujia) kitu hicho, utakipata. Lakini hakiwezi kukujia na wewe umekaa kitako, bali ni lazima ufanye sababu. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 145-148

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wakawa kati na kati. Wanasema kila kitu kinakuwa kwa Matakwa na Utashi wa Allaah kukiwemo matendo ya waja. Yameumbwa na Allaah na wakati huo huo ni matendo ya mja (aloyafanya) kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe. Kwa kuwa mja ana matakwa na utashi wake. Lakini hata hivyo hayajitoshelezi na Allaah – kama wanavosema Qadariyyah – na hakutenzwa nguvu – kama wanavosema Jabriyyah – bali yeye anafanya matendo kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe. Kwa ajili hiyo ndio maana akapewa thawabu kwa kutenda kheri na kuadhibiwa kwa kutenda uovu. Kwa kuwa ametenda kwa kutaka na kupenda kwake mwenyewe. Lau angelikuwa ametenzwa nguvu asingeliadhibiwa, vipi ataadhibiwa kwa kitu ambacho hakukifanya kwa khiyari yake na kutaka kwake mwenyewe?

Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah (Jalla wa ´Alaa) Hamuadhibu mwendawazimu ambaye hafanyi kwa kutaka kwake, hamuadhibu vilevile mtu mwenye kutenzwa nguvu ambaye anafanya si kwa khiyari yake, wala hamuadhibu mwenye kulala ambaye hana mawazo wala akili. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kalamu imesimamishwa kwa watu (aina) tatu; aliyelala mpaka anapoamka, mtoto mpaka anapobaleghe na mwendawazimu mpaka anapopata akili.”

Kwa nini? Kwa kuwa watu hawa hawana matakwa wala utashi ndio maana wakawa hawaadhibiwi kwa waliyoyatenda wakati ambapo akili yao imepotea na utashi wao.

Ama yule mwenye matakwa, utashi na khiyari, anapewa thawabu kwa kutenda mambo ya kheri na anaadhibiwa kwa kutenda maasi. Kwa kuwa ameyafanya kwa khiyari yake na kutaka kwake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ
“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema.” (al-Baqarah:277)

“…wakatenda mema”, ameyanasibisha matendo kwao. Anasema:

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا
“Hakika wale waliokufuru.” (al-Baqarah:06)

Ameinasibisha kufuru kwao. Kwa kuwa ni kutokana na kitendo chao na kutaka kwao. Akasema tena:

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ
“Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam.” (al-Jinn:23)

Ameyanasibisha maasi kwao. Kwa kuwa ni kutoka na matendo yao. Kwa njia ya kimatendo, ni kitendo cha mja. Ama kwa njia ya Qadar, kimekadiriwa na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ni Qadar ya Allaah na wakati huo huo ni kitendo cha mja kwa kujumuisha baina ya nususi mbili. Hili linatolewa dalili na Kauli Yake (Ta´ala):

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
“Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika njia ya haki). Na hamtotaka isipokuwa Atakaye Allaah Mola wa walimwengu.” (at-Takwiyr:28-29)

Kauli Yake:

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ
“Kwa yule atakaye miongoni mwenu.”

hii ni Radd kwa Jabriyyah ambao wanapinga matakwa ya mja. Ni dalili inaonesha kuwa mja ananyooka kwa kutaka kwake mwenyewe. Kisha Akasema:

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
“Na hamtotaka isipokuwa Atakaye Allaah Mola wa walimwengu.”

hii ni Radd kwa Qadariyyah ambao wanasema kwamba matendo ya mja ni yenye kujitosheleza na mja ndiye ameumba matendo yake. Aayah hii imeraddi mapote yote mawili. Vilevile Aayah inathibitisha madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, ya kwamba utiifu na maasi ni kitendo cha mja na wakati huo huo ni kutokana na Qadhwaa na Qadar ya Allaah. Amewakadiria nayo na wao wakayafanya kwa khiyari yao na kutaka kwao wenyewe na kupenda kwao wenyewe. Kwa ajili hiyo mtu mwenye akili anaweza – ukitoa aliyetenzwa nguvu – anaweza kufanya ´amali, anaweza kuacha kufanya ´amali. Anaweza kusimama akaswali, kutoa Swadaqah, kupigana Jihaad katika njia ya Allaah kama jinsi vilevile anaweza pia kuacha, anaweza kuacha kuswali, kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu, anaweza kuacha kupigana Jihaad katika njia ya Allaah. Anaacha yeye mwenyewe kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe. Anaweza yote mawili kufanya na kuacha. Anafanya uzinzi, kunywa pombe, kula Ribaa kwa khiyari yake kama jinsi akipenda pia anaweza akayaacha. Anaweza kuacha Ribaa, uzinzi na akaacha mambo ya haramu. Ni kwa khiyari na kutaka kwake mwenyewe anafanya haya. Hakuna asiyejua hili.

Jabriyyah hawayatendei kazi maneno haya waliyosema katika kila kitu. Lau mtu atawafanyia uadui ima kwa kupiga mmoja wao au kuua mmoja wao, je si wataomba lipizo na kisasi? Kwa nini wataomba hili na wakati wanasema kwamba ametenzwa nguvu na hafanyi kwa khiyari yake? Huu ni mgongano.

Vilevile isitoshe wao wanatafuta riziki na wanaoa, ingelikuwa (mtu ametenzwa nguvu) – kama wanavosema – kwa nini basi wanafanya vitendo hivi na wanatafuta kupatikana vitu visivyokuwepo?! Haya madhehebu khabithi (machafu) wao wenyewe hawatendei kazi hili katika maisha yao ya sasa. Kwa ajili hiyo ndio maana wanaomba kisasi, wanaoa na wanatafuta riziki. Hii ni kauli batili na tunaomba kinga kwa Allaah. Hii ndio natija ya kutegemea fikira, akili, maneno na maoni ya watu bila ya kurejea katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Hakuna mgongano wa kuamini Qadhwaa na Qadar na kufanya sababu. Wewe unatakiwa kuamini kwamba, Anayotaka Allaah huwa na ambayo Hakutaka hayakukuwa. Usipinge (kufanya) sababu. Unatakiwa kutafuta riziki, uoe, utafute biashara, utawanyike katika ardhi na kutafuta fadhila (riziki) za Allaah. Usiseme kuwa unategemea Qadhwaa na Qadar na kwamba ikiwa nimeshakadiriwa kitu kitanijia tu na kama sikukadiriwa hakitonijia. Hili halisemwi na mtu wa akili. Hata ndege na wanyama – kwa maumbile yake – inaenda kutafuta riziki. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Lau mgelikuwa mnamtegemea Allaah ukweli wa kumtegemea, basi Angelikuruzukuni kama Anavomruzuku ndege. Inaruka hali ya kuwa haina kitu tumboni na inarudi imejaa tumbo (imeshiba).”

Hata ndege inafanya sababu inaruka na kwenda kutafuta riziki. Kwa hivyo hakuna mgongano baina ya kuamini Qadhwaa na Qadar na kufanya sababu. Wanaosema hivi ni Jabriyyah.

Hata hivyo, kufanya sababu hakujitoshelezi kuleta natija. Msababishaji ni Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hii ni Radd kwa Qadariyyah. Hatupetuki katika kuthibitisha sababu kama wafanyavyo Qadariyyah kama jinsi vilevile hatupetuki katika kuikanusha kama wafanyavyo Jabriyyah. Kufanya sababu ni jambo ambalo linatakikana. Anasema (Ta´ala):

فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ
“Basi tafuteni riziki kwa Allaah.” (al-´Ankabuut:17)

وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ
“Na tafuteni katika fadhila za Allaah.” (al-Jumu´ah:10)

Allaah Ametuamrisha Swalah, Swawm na mambo mbali mbali ya utiifu. Huku ni katika kufanya sababu. Vilevile Ametukataza kufanya sababu za shari (ovu), kufuru, maasi na ufusaki. Hivyo, haina maana kuamini Qadhwaa na Qadar ukafika unapinga kufanya sababu. Bali unatakiwa kufanya sababu pamoja na kuamini ya kwamba ikiwa Allaah Amekuandikia (kukipata au kukujia) kitu hicho, utakipata. Lakini hakiwezi kukujia na wewe umekaa kitako, bali ni lazima ufanye sababu.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 145-148


  • Kitengo: Uncategorized , Jabriyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 19th, February 2014